TAFSIRI NA UKALIMANI MWASOKO NA WENZAKE (2006) 1.DHANA YA TAFSIRI. TAFSIRI IMEFASILIWA KUWA, NI KUTOA MAWAZO KUTOKA KATIKA LUGHA MOJA KWENDA LUGHA NYINGINE BILA YA KUBADILISHA MAANA. [TUKI 2002: 271] MWANSOKO NA WENZAKE (2006), WANAFASILI TAFSIRI KUWA NI ZOEZI LA UHAWILISHAJI WA MAWAZO KATIKA MAANDISHI KUTOKA LUGHA MOJA HADI NYINGINE. CATFORD [1965:20] ANASEMA TAFSIRI NI, “KUCHUKUA MAWAZO YALIYO KATIKA MAANDISHI KUTOKA LUGHA MOJA {LUGHA CHANZI} NA KUWEKA BADALA YAKE MAWAZO YANAYOLINGANA KATIKA LUGHA NYINGINE {LUGHA LENGWA}. AS-SAFI AKIMNUKUU DUBOIS (1974), ANAELEZA KUWA TAFSIRI NI UELEZAJI KATIKA LUGHA NYINGINE AU LUGHA LENGWA WA KILE KILICHOELEZWA KATIKA LUGHA NYINGINE (LUGHA CHANZI) IKIHIFADHI MAANA NA MTINDO WA MATINI CHANZI. MAANA ZOTE HIZO TULIZOZIANGALIA, UTAONA KUWA, KUNA MAMBO MATATU MUHIMU YANAYOJITOKEZA, MAMBO HAYO NI: (I) MAWAZO YANAYOTAKIWA KUTAFSIRIWA SHARTI YAWE KATIKA MAANDISHI. (II) MAWAZO AU UJUMBE KATI YA LUGHA CHANZI NA LUGHA LENGWA SHARTI YALINGANE. (II...