Dunia Uwanja wa Fujo ni riwaya iliyoandikwa na Euphrase Kezilahabi mwaka wa 1975 . Ni riwaya ambayo inasawili maisha ya wanadamu hususani waishio Afrika Mashariki , hasa hasa katika nchi ya Tanzania . “Dunia Uwanja wa Fujo” inaelezea jinsi maisha yaliyopo duniani ni sawasawa na fujo, kwani kila mtu anayekuja duniani huleta fujo zake na baadaye kutoweka. Mwandishi anaelezea kwamba kila mtu anafanya fujo zake na kusababisha matatizo mbalimbali katika jamii yake kama vile mauaji , ukabila , umalaya , uchawi , ubakaji , ulevi wa kupindukia n.k. Hivyo basi mwandishi anaamini kwamba katika dunia kila mtu anakuja na fujo zake na kutoweka. Kwa mfano, mhusika Tumaini katika riwaya hii ameleta fujo zake kama vile umalaya, mauaji na mengine mengi na baadaye kutoweka. MBINU ZA KIFANI Fani za kijadi ndizo zilizosababisha riwaya izalike. "...