Sintaksia ni utanzu wa sarufi unaojishughulisha na uchanganuzi wa mpangilio wa maneno katika sentensi na uhusiano wa vipashio vyake. Katika utanzu kinachochunguzwa ni zile sheria au kanuni ambazo hazina budi kufuatwa katika kuyapanga maneno ya lugha katika mfuatano (neno moja baada ya jingine) kwa namna ambayo itafanya maneno hayo yalete maana inayokubalika na kueleweka katika lugha inayohusika (Massamba na wenzake 2001).
Sintaksia ni utanzu wa isimu unaoshughulikia muundo wa sentensi na elementi zingine zinazounda sentensi kama vile kategoria za maneno, vikundi na vishazi (Habwe na Karanja 2004).
Sintaksia ni tawi la isimu linalojihusisha (linalohusika) na muundo wa uchanganuzi wa taratibu na kanuni za uhusiano baina ya maneno katika tungo. (TUKI 2015).
Hivyo basi, sintaksia ni utanzu wa sarufi unaojihusisha na uchunguzi wa mpangilio wa maneno katika sentensi na uhusiano wa vipashio vyake.
Katika fasili ya lugha, lugha ni mfumo wa sauti za nasibu ambazo hutumiwa na jamii kwa madhumuni ya mawasiliano kati yao. (Massamba na wenzake 1999). Kwa fasili hii vipengele vinavyounda sarufi ya lugha ya Kiswahili ni fonolojia, mofolojia, sintaksia na semantiki.
Kwa hiyo tunasema kwamba, kigezo cha kisintaksia si bora kuliko vigezo vingine (fonolojia, mofolojia, semantiki) kwa kuwa kila kigezo hutegemea kigezo kingine ili kuleta ukamilifu katika sarufi ya Kiswahili kama ifuatavyo:-
Sintaksia na fonolojia, ambapo fonolojia ni tawi la isimu ambalo hushughulikia uchambuzi wa mfumo wa sauti katika lugha. Hivyo tunaangalia namna vitamkwa vinavyoungana kuunda neno.
Kwa mfano, neno anacheza limeundwa na viambajengo kama vile a-n-a-c-h-e-z-a ambavyo ndiyo fonolojia ya neno anacheza. Kwa mantiki hiyo muundo wa neno hilo umetegemea sauti mbalimbali ambazo zimekamilisha neno zima anacheza, vile matamshi hubadili maana endapo msemaji au mtamkaji akitamka vitamkwa tofauti atabadili maana ya neno lililokusudiwa. Mfano wapare neno samani wao hutamka thamani, neno thamani ikiwa na maana ya ubora wa kitu badala ya samani ikiwa na maana ya vitu vilivyotengenezwa kwa mbao kama vile kabati, viti, vitanda na meza. Vilevile fonolojia husaidia kuelewa matamshi sahihi ya neno katika sintaksia, lakini pia fonolojia ina hazina ya vitamkwa na vitamkwa ndivyo vinavyounda sentensi. Kwa hiyo sintaksia si bora kuliko fonolojia bali hutegemeana na kukamilishana.
Sintaksia na mofolojia, ikiwa mofolojia ni tawi la isimu ambalo hujishughulisha na uchambuzi wa kanuni na mifumo inayohusu upangaji wa mofimu mbalimbali ili kuunda maneno katika lugha. Kwa fasili hiyo ya mofolojia inaonesha wazi kabisa jinsi inavyohusiana na sintaksia kwa sababu maumbo ya kimofolojia na kisintaksia huathiriana katika baadhi ya vipengele kwenye sentensi yaani upande wa kiima na kiarifu.
Kwa mfano, 1- mtoto/ ameanza kutembea.
2- watoto/ wameanza kutembea. Katika mfano namba moja, mofimu m katika upande wa kiima imeathiri utokeaji wa mofimu a katika upande wa kiarifu. Vilevile katika sentensi namba mbili mofimu wa imeathiri utokeaji wa mofimu wa katika upande wa kiarifu. Ili sentensi iwe katika muundo unaokubalika katika lugha ya Kiswahili lazima maumbo yake yaweze kuathiriana katika upande wa kiima na kiarifu. Hivyo sintaksia si bora kuliko mofolojia kwani hutegemeana na kukamilishana.
Sintaksia na semantiki, tukifafanua semantiki kama tawi la isimu ambalo hujishughulisha na uchambuzi wa lugha katika kiwango cha maana, tunaweza kusema muundo wa sentensi unakubalika katika lugha ya Kiswahili endapo tu sentensi hiyo imeleta maana.
Kwa mfano, 1- mtoto anachezea maji. 2- maji anachezea mtoto. Katika sentensi namba moja muundo uliotumika unakubalika katika lugha ya Kiswahili kwa vile umeleta maana kamili. Wakati katika sentensi namba mbili muundo wake haupo sahihi katika lugha ya Kiswahili na ni nguma kupata maana. Semantiki huchunguza maana katika kiwango cha sauti-neno-kirai-kishazi-sentensi. Kazi ya sintaksia ni kuunda sentensi na kazi ya semantiki ni kuangalia maana ya sentensi hiyo. Hivyo sintaksia si bora kuliko semantiki kwa kuwa hutegemeana na kukamilishana
Kwa kuhitimisha tunaweza kusema uhusiano uliopo baina ya vigezo au matawi hayo ya sarufi (fonolojia, mofolojia, sintaksia na semantiki), hakuna kigezo chochote kati ya hivyo kinachoweza kusimama peke yake na kukamilisha sarufi ya lugha ya Kiswahili. Hii ni kwa sababu vyote hutegemeana, kuathiriana na kukamilishana.
MAREJELEO
Habwe, J & Karanja P (2004): Misingi ya Sarufi ya Kiswahili. Nairobi: Phoenix Publishers Ltd.
Massamba na Wenzake (2001): Sarufi Miundo ya Kiswahili Sanifu Sekondari na Vyuo. TUKI. Dar es Salaam.
Massamba, D.P.B (1999): Sarufi Miundo ya Kiswahili Sanifu Sekondari na Vyuo. Dar es Salaam. TUKI.
TUKI (2005): Kamusi ya Kiswahili Sanifu. Dar es Salaam. Oxford University Press.

Comments
Post a Comment