Muhtasari,
ni ufundisho wa mambo yanayofundishwa katika shule au chuo, vidokezo vya somo.
(J.S.Mdee, K. Njogu, Shati A. 2011).
Muhtasari,
ni muongozo unaotaja mambo yote yatakayofundishwa, mbinu za ufundishaji, na
zana za kufundishia.
Mhtasari wa somo,
ni mwongozo unaotaja mambo yatakiwayo kufundishwa kwa kipindi maalumu.
Aidha
muhtasari wa somo la Kiswahili huwa na muundo yaani utangulizi, malengo ya
elimu Tanzania, malengo ya elimu ya sekondari, ujuzi wa jumla wa somo la
Kiswahili katika shule za sekondari, malengo ya jumla ya kufundisha somo la
Kiswahili katika shule za sekondari, ujuzi, malengo na majedwali ya ufundishaji
kidato cha 1 – 4.
Tofauti,
ni ile hali ya kutofanana au kutokuwa sawa. Tofauti inapatikana kwa kuangalia
umbo la kitu, hali ya kitu, kazi ya kitu na hata muda. Tofauti zimejitokeza
katika upande wa utangulizi, ujuzi, na malengo.
Zifuatazo
ni tofauti zilizojitokeza katika muhtasari wa mwaka 2005 na muhtasari wa mwaka
2010, katika kipengele cha utangulizi:-
Utangulizi,
katika kipengele cha utangulizi, muhtasari wa mwaka 2005 wametumia neno muhamo wa ruwaza wakibainisha vipengele
au mambo yaliozingatiwa katika muhtasari huu. Lakini katika muhtasari wa mwaka
2010 wametumia neno mbinu shirikishi
katika kipengele hichohicho kinachopambanua mambo au vipengele vilivyozingatiwa
katika muhtasari huo. Maneno yote hayo mawili yaani muhamo ruwaza na mbinu
shirikishi yana maana inayofanana ambayo ni kuwashirikisha wanafunzi katika
tendo la ufundishaji na ujifunzaji.
Uandishi wa muhtasari,
katika muhtasari wa mwaka 2010 umetajwa vizuri katika jalada la nje kuwa ni
muhtasari wa mwaka 2010 lakini ndani yake katika ukurasa wa iv kwenye kipengele cha utangulizi kuna
kosa la kiuandishi au kiuchapaji ambapo umetajwa kama muhtasari wa mwaka 2005.
Hii inaashiria kuwa kulikuwa na uzembe wakati wa uhariri.
Ushauri wa mwalimu,
kwenye muhtasari wa mwaka 2005 mwalimu anashauriwa kuwa anaweza kutumia kitabu
cha kiada zaidi ya kimoja ili kujiongezea maarifa na kumrahisishia ufundishaji,
lakini katika muhtasari wa mwaka 2010 mwalimu ameshauriwa azingatie kuwa
“Orodha ya vitabu vya kufundishia Kiswahili vitakuwa vikitolewa na wizara ya
elimu na mafunzo ya ufundi. Muhtasari huu wa mwaka 2010, umemfanya mwalimu kama
mtu wa kusubilia tu pasipo kujishughulisha na usomaji wa vitabu tofauti tofauti
ili kuongeza maarifa katika somo la Kiswahili.
Muhtasari
huu wa mwaka 2005 na muhtasari wa mwaka 2010, umetofautiana katika mambo
machache sana tukizingatia vipengele tofauti tofauti vya muhtasari. Lakini pia
muhtasari wa mwaka 2010 na muhtasari wa mwaka 2005 umefanana kwa asilimia
nyingi ukilinganisha na kutofautiana kwake. Muhtasari huu wa 2005 na 2010
umefanana katika muda wa kufundishia, malengo ya elimu Tanzania, madhumuni ya
elimu ya sekondari, ujuzi wa somo la Kiswahili, malengo ya jumla ya kufundisha
somo la Kiswahili kwa shule za sekondari, muundo wa muhtasari, ujuzi wa kila
kidato, malengo ya kila kidato, mada za kila kidato, idadi ya vipindi na masaa.
MAREJELEO
Ø J.S.Mdee,
K. Njogu, Shati A. (2011). Kamusi ya
karne ya 21: Longhorn.
Ø Muhtasari
wa Kiswahili kwa shule za sekondari, kidato cha i-iv (2005).
Ø Muhtasari
wa Kiswahili kwa shule za sekondari, kidato cha i-iv (2010).
Comments
Post a Comment