Mbinu za kufundishia,
ni miongozo mbalimbali atumiayo mwalimu wakati wa kufundisha somo aliloliandaa
kwa wanafunzi wake. Walimu wanapaswa kuamua kwa kuchagua kwa makini njia na
mbinu bora za kufundishia ili wanafunzi wake waweze kujifunza kwa ufanisi. Ziko
njia nyingi za kutengeneza mazingira ya mtoto aweze kujifunza na pia ziko mbinu
nyingi za kufundishia. Pamoja na wingi huo tunaweza kuzigawa katika makundi
makuu mawili kadri ya jinsi zinavyowashirikisha watoto katika tendo la
kujifunza, ambazo tunaweza kuziita shirikishi
na zisizo shirikishi.
Zifuatazo
ni baadhi ya mbinu shirikishi na zisizo shirikishi za kufundishia pamoja na
faida na hasara zake:-
Njia ya majadiliano,
njia hii imekuwa ikitumika katika ufundishaji kwa muda mrefu. Katika
kujadiliana mwanafunzi mmoja mmoja hupata nafasi ya mawazo aliyonayo kuhusu
suala linalojadiliwa na yeye pia huweza kupata mawazo yaw engine. Katika
majadiliano mwanafunzi hupata ujuzi mpya nje na ule aliokuwa nao kabla
hajashiriki katika majadiliano.
Mambo
ya kuzingatia.
·
Kazi iwe na changamoto ya kutosha
kuhitaji majadiliano ili wahusika wafikie uamuzi wa pamoja.
·
Kazi ilenge wahusika kutoa mawazo na
hatimae kupata ujuzi mpya kutokana na majadiliano.
·
Yawepo malengo yanayoeleweka vizuri na yanayotekelezeka. Ni muhimu malengo
haya yawekwe wazi kwa wahusika.
Faida
za mbinu.
Ø Kukuza
mahusiano ya wahusika.
Ø Kuwafanya
wahusika wafurahie na kulipenda somo.
Ø Kukuza
stadi za ubunifu na mawasiliano.
Ø Kujenga
uwezo wa wahusika wa kuamini na kuvumiliana.
Ø Huleta
ujuzi na uongozi.
Ø Kila
mmoja huweza kutoa mchango wake na mawazo yake kwani watu ni wachache katika
kundi.
Ø Husaidia
kujenga kumbukumbu kwa wanafunzi.
Hasara
za mbinu hii.
Ø Kama
hakuna usimamizi na utaratibu mzuri njia hii inaweza isiwe tofauti na mhadhara
kwani mtu mmoja tu au kiongozi anaweza kutawala uwanja wa mazungumzo.
Ø Kama
kiongozi si imara, kundi linaweza kushindwa kujadili mada waliopewa na hivyo
kujadili nje ya mada.
Ø Hujenga
uhasama kati ya kundi na kundi, wanafunzi na wanafunzi.
Njia ya mhadhara,
hii ni njia ya kufundishia kitu kwa kutumia hotuba ndefu. Lengo la kutumia njia
hii ni kuwazoeza wanafunzi kuwa wasikivu na kuzingatia mambo muhimu na yenye
msingi tu kati ya maelezo mengi yanayotolewa na mhadhiri.
Mambo
ya kuzingatia katika mbinu hii.
·
Njia hii itumike kwa wanafunzi
waliopevuka kimawazo.
·
Njia hii itumike katika kuanzisha mada
mpya ikiwa tu itaonekana haipo njia nyingine ya kufundishia mada hiyo.
Faida
za mbinu hii.
Ø Huwezesha
kufundisha mambo mengi kwa wakati mmoja.
Ø Humjengea
mwanafunzi tabia ya kuchambua taarifa na kuzingatia mambo muhimu tu.
Ø Inapima
usikivu wa mwanafunzi kuhusu mada inayofundishwa.
Hasara
za mbinu hii
Ø Haiwashirikishi
sana wanafunzi katika tendo la kujifunza.
Ø Huwachosha
wanafunzi kwa sababu watoto hawawezi kuwa wasikivu kwa muda mrefu.
Ø Wanafunzi
huchoka kusikia sauti ya mtu mmoja tu muda wote.
Ø Ni
mtu mmoja tu anayetoa mawazo yake na wengine yaani wanafunzi hupokea tu, hivyo
hujenga utegemezi kwa wanafunzi.
Kazi mradi,
wanafunzi na walimu wengi wameelekea kuamini kuwa mbinu ya kazi mradi ni ya
utendaji wa mda mrefu. Kwa wengi kazi mradi inatumika tu kwa kuwatathimini
wanafunzi kwa muda huo mrefu. Kwa mtazamo wa sasa kazi mradi yaweza kufanyika
hata kwa kipindi kimoja tu cha darasani. Katika utendaji wanafunzi huunda maana
zao binafsi kutokana na jinsi nadharia husika zinavyojitokeza katika maisha
halisi ya kila siku.
Mambo
ya kuzingatia katika mbinu hii.
·
Mwalimu lazima abainishe kuwa anatumia
njia hii katika hatua gani ya mada husika na kuna umuhimu gani wa kutumia njia
hii na isiwe nyingine.
·
Wanafunzi wapewe fursa ya kuchagua mambo
ya kufanya katika kazi mradi wakishirikiana na mwalimu.
·
Wanafunzi wanatakiwa wajue nini cha
kufanya na utendaji wao unatakiwa uwe wa kiwango gani na kwa muda gani.
·
Mwalimu wasaidie wanafunzi katika
kuunganisha taarifa na kuzijazia maana.
Faida
za mbinu hii.
Ø Kukuza
stadi mbalimbali za kufikiri.
Ø Kujenga
tabia ya kuhusisha mambo wanayojifunza na maisha yao ya kila siku.
Ø Kujiamini
na kupenda kujifunza kwa kujitegemea.
Hasara
ya mbinu hii.
Ø Ni
vigumu kuchagua mada ifaayo kufundisha kwa njia hii.
Ø Kama
haikuandaliwa vizuri maarifa au ujenzi wa maana uliokusudiwa hushindwa
kuwafikia walengwa.
Njia ya ziara, hii
ni safari inayopangwa kwa madhumuni fulani. Hii ni dhiara ya kielimu ambayo
hufanywa kwa njia ya kutembelea na kuona mahali ua vitu halisi kwa njia ya
kujifunza. Katika mazingira ya kishule waalimu hufanya ziara na wanafunzi wao
kutembelea sehemu mbalimbali zenye mambo yanayohusiana na mada wanazofundisha
shuleni. Wanafunzi wanaweza kutembelea sehemu kama vyanzo vya mito, madimbwi,
viwanda, benki, posta na mbuga za wanyama.
Mambo
ya kuzingatia katika mbinu hii.
·
Mwalimu afanye uchunguzi wa kina kuhusu
sehemu ya kufanyia ziara kuona kama ina jambo linalokusudiwa kufundishwa.
·
Yawekwe malengo ya ziara hiyo wazi kwa
kila mmoja.
·
Kuamua iwapo watafanya kazi kwa vikundi
au mmoja mmoja na mwalimu agawe majukumu kwa kila mmoja au kila kundi.
·
Mwongozo au maswali ya kusaidia kupata taarifa
zinazotakiwa zitolewe mapema kwa wanafunzi ili uwasaidie wakati wa ziara.
·
Vifaa na jinsi ya kukusanya taarifa
wakati wa ziara. Vifaa kama daftari, kamera na vinasa sauti vinaweza
kutayarishwa.
Faida
za mbinu hii.
Ø Humpa
mwanafunzi nafasi ya kuwa katika mazingira halisi wakati wa kujifunza.
Ø Hufanya
dhana dhahania kueleweka kwa kina zaidi.
Ø Huongeza
motisha na kumuwezesha mwanafunzi kupenda kujifunza zaidi.
Ø Huondoa
utata unaoweza kuwepo kutokana na mawazo ya awali ya wanafunzi na kuwafanya
wajenge dhana kamilifu zaidi.
Ø Hushirikisha
wanafunzi wote.
Ø Wanafunzi
hutegemea katika kupata taarifa inayotakiwa badala ya kumtegemea mwalimu.
Hasara
ya mbinu hii.
Ø Gharama
huwa kubwa – usafiri.
Ø Matayarisho
huchukua muda mrefu.
Ø Usimamizi
huwa mgumu hasa kama darasa lina wanafunzi wengi na mahali pa ziara ni mbali.
Ø Sio
rahisi kuendesha somo kwa kipindi kimoja tu.
Onyesho mbinu, ni
uwasilishaji unaofanywa wa matendo kuhusu jambo au dhana fulani. Onesho mbinu
huambatana na maelezo ya ana kwa ana, Matumizi ya zana na maswali na majibu
ambayo huwezesha wanafunzi kujifunza stadi mpya.
Mambo
ya kuzingatia katika mbinu hii.
·
Andaa dhana mahususi za somo au mada.
·
Andaa vifaa vyote vinavyotakiwa katika
onyesho.
·
Fanya zoezi la onyesho lako kabla ili
kuona kuwa onyesho lako linafanikiwa.
·
Waeleze hatua zitakazo fuata katika
onyesho.
·
Washirikishe wanafunzi wako kila mara na
kila hatua inayofanywa.
·
Toa nafasi kwa wanafunzi kufanya onesho
wenyewe.
·
Toa muhtasari wa maelezo kuhusu dhana
uliojifunza mala baada ya onesho.
Faida
za mbinu hii.
Ø Kujifunza
kwa kuona kuna mahamasisho makubwa katika kujifunza.
Ø Kujenga
ari ya kujifunza.
Ø Wanafunzi
hujifunza kwa kutenda chini ya kiongozi au mtaalamu.
Ø Njia
hii huwezesha kufanya masahihisho ya moja kwa moja katika kujifunza.
Hasara
za mbinu hii.
Ø Maandalizi
makini hutakiwa na muda mwingi wa vitendo hutakiwa.
Ø Hairuhusu
idadi kubwa ya wanafunzi.
Ø Maandalizi
mabaya yanaweza kupotosha maana ya onesho.
Kwa
kuhitimisha, inaweza kusemwa kuwa mbinu au njia za kufundishia na kujifunzia ni
ujanja anoubuni mwalimu kila awapo darasani, kwa lengo la kurahisisha
uelewekaji wa somo husika katika tendo la ufundishaji na ujifunzaji. Hivyo basi
kila suala au jambo analolifanya mwalimu wakati wa somo darasani huweza kusemwa
kuwa ni mbinu au njia ya kufundishia na kujifunzia.
MAREJELEO
Ø Mgombele
J.Mwiga (2003). Mbinu za kufundishia na kujifunza: mwandiga bookshop.
Ø Jiandae.wordpress.com/zana
za kufundishia.
Ø Paulmeela.wordpress.com/mbinu
za kufundishia Kiswahili.
Hakika kazi hii ina muwaka na mvuto wa aina yake. Ni utungo wenye manufaa zaidi
ReplyDeleteasante sana mwl.
DeleteNimefurahi na nimependa kwa kuwa walimu wa walimu.
ReplyDeleteProudly to be a teacher
Asante sana
DeleteMambo yanaenda Sawa kupitia Rejea MBALIMBALI tunamshukuru Kwa MCHANGO wako
ReplyDeleteasante sana
DeleteNaomba kuuliza swali hili .ufundishaji ni fani? Naomba maeleze
ReplyDeleteNimejifunza mengi,asante
ReplyDeleteNimependa namna hizi mbinu zilivyochambuliwa
ReplyDeleteHujambo?
ReplyDeleteNaomba unifae na jinsi ya kulijibu swali hili👉
Ukirejelea hadithi moja tu katika ''TUMBO LISILOSHIBA'', Elezea wewe kama mwalimu jinsi utakavyoifunza darasani🤝🙏🙏🙏🙏Naitwa Levy
Una mambo kweli kweli, yaani umeshafika huku!
Deletenashukuru,kwa kazi njema.i
ReplyDeleteItanifaidi sana hasa sasa najifunza mbinu za ufundishaji
Mbinu ya fikiri- jozisha-wasilisha inatumikaje
DeleteNmeipenda km mwalm
ReplyDeleteKazi njema; napata mwongozo kikamilifu unaonisaidia katika kuyajibu maswali ya kazi tunazopewa na mhadhiri. Asante
ReplyDeleteNaitaji kujua mbinu ya igizo dhima
ReplyDeleteNaomba msaada kuhusu mbinu za kazimradi Katika ufundishaji wa ujifunzaji wa somo la kiswahili
ReplyDeleteAhsanteni kwa mambo hapo juu
ReplyDeleteKazi nzuri
ReplyDeleteLakini pia naomba tofauti ya onyesho mbinu na igizo dhima
Mola awabariki Kwa kazi bunifu kama hii
ReplyDelete