AINA ZA USHAIRI (BAHARI) Bahari; hii ni aina mahususi ya ushairi yenye sifa fulani kiumbo na pengine hata kimaudhui na kimatumizi na zinazoipambanua na aina nyingine ya ushairi. S.A Kibao (2003) anasema, ushairi wa Kiswahili umegawanyika katika sehemu kuu tatu ambazo ni: shairi, utenzi na ngonjeara. Anaendelea kusema, aina zote hizi kanuni zake ni za pamoja isipokuwa utenzi ambao una mpangilio wa namna ya pekee. S. Robert na Amri Abeid (1954) wanasema zipo bahari tatu tu za ushairi nazo ni:wimbo, shairi na utenzi. A.S. Nabhany na wenzake wameainisha bahari 13 za ushairi na kusema kuwa utungo wowote lazima uingie katika bahari mojawapo. Bahari hizo ni hizi zifuatazo: 1. Ushairi; Ni utenzi wenye mishororo minne na vipande viwili kila msitari. Kila mstari una mizani 16 na kila kipande kina mizani 8. Maudhui yake yanatokana na jambo lolote lile analoliona mtunzi. 2....