Tuanze uhakiki huu, kwa kuanza na : KIPENGELE CHA MAUDHUI Dhamira Hili ni wazo kuu au mawazo mbalimbali yanayojitokeza katika kazi ya fasihi. Na katika diwani hii kuna dhamira kuu na dhamira ndogondogo ambazo zimejitokeza, kwa kuanza tunaanza na; Dhamira kuu Dhamira kuu ni wazo kuu linalojitokeza katika kazi za fasihi, na katika diwani hii, wazo kuu ni ukombozi wa jamii, sasa tuanzekuangalia ukombozi huo wa jamii, namna unavyojadiliwa katika diwani hii: Ukombozi wa jamii Dhamira kuu inayojitokeza katika diwani hii ni ukombozi wa jamii, mwandishi amejadili ukombozi huo katika Nyanja mbalimbali kama vile ukombozi wa kisiasa, kiuchumi na kiutamduni. Ukombozi wa kisiasa Kwa kiasi kikubwa mwandishi amejadili ukombozi wa kisiasa, mwandishi anaona kuwa ili jamii iweze kujikomboa kisiasa, jamii hiyo haina budi kuondokana na matatizo ya kiungozi [uongozi mbaya] uongozi ambao hauwajali wananchi zaidi ya kujali matumbo yao na maisha yao huku wakiwaacha wananchi waliowengi wakiishi maish...