SWALI.
Kwa
kutumia mifano kutoka katika lugha za makabila ya Tanzania, onyesha utofauti wa
kiisimu na kilahaja katika matumizi ya lugha.
Lugha
ni mpangilio wa sauti na maneno unaoleta maana ambao hutumiwa na watu wa taifa
au kundi fulani kwa ajili ya mawasiliano. Lugha ni maneno pamoja na matumizi
yake. (TUKI 2013).
Lugha;
ni mfumo wa sauti za nasibu zilizokua katika mpango maalumu na zilizokubaliwa
na jamii ya watu fulani ili zitumike katika mawasiliano.
Lahaja ni
tofauti katika matamshi, maumbo, na matumizi ya maneno katika maeneo mbalimbali
kwa lugha yenye asili moja. (TUKI, 2013).
Lahaja ni
vijilugha vinavyoibuka kwa lugha moja kuu kutokana na tofauti za kijiografia,
kitabaka baina ya wazungumzaji wa lugha hiyo. Watu hao hutofautiana kimatamshi,
muundo wa sentensi au msamiati.
Zifuatazo
ni tofauti za kiisimu kutoka katika makabila ya Tanzania katika matumizi ya lugha:-
Lafudhi, hii
ni tofauti mojawapo katika tofauti zinazojitokeza kwenye makabila ya Tanzania.
Ile hali ya upekee wa mtu katika matamshi unaoathiriwa na lugha mama, mazingira
yake ya kijiografia au ujuzi wake wa lugha inapelekea kutokea kwa utofauti. Mfano
wasukuma lafudhi yao imejikita katika ukazaji wa maneno, kwa mfano neno ntakupiga silabi pi hutamkwa kwa mkazo wa hali ya juu.
Kiimbo, ule
upandaji na ushukaji wa sauti katika utamkaji wa maneno hutofautia katika kila
lugha na kila kabila. Mfano mnyakyusa anaposema ugonile herufi u hutamkwa
kwa sauti ya juu ambapo maneno mengine hutamkwa kwa kushusha sauti. Wakati
huohuo wasukuma wanaposema mwangaluka
neno mwa na ka hutamkwa kwa sauti ya juu kuliko maneno ya kati. Hivyo kuna
utofauti mkubwa sana wa kiimbo katika makabila ya Tanzania.
Mkazo, katika
mkazo wa baadhi ya maneno katika utamkaji, makabila mbalimbali yanatamka kwa
mtindo tofautitofauti. Kwa mfano kabila kama wakurya neno ninkutema neno te hutamkwa
kwa mkazo sana kuliko maneno mengine. Lakini pia wanyakyusa utamkaji wao ni
tofauti kidogo, kwa mfano neno ninkukoma
neno ko hutamkwa kwa mkazo kuliko
maneno mengine. Hivyo kuna utofauti mkubwa sana wa kiisimu katika makabila ya
Tanzania.
Toni, makabila
mbalimbali hutofautiana katika toni ambapo kila kabila lina toni yake katika
utamkaji wa maneno. Kile kiwango fulani cha juu au cha chini cha sauti ndicho
kinachotofautisha, mfano kabila la wahaya toni yao huwa ni ya chini
ukilinganisha na toni ya wasukuma ambayo huwa ni ya juu. Wahaya katika neno zebilo(za siku) huwa na toni ya chini,
wakati wasukuma neno jamashiku(za
siku) huwa na toni ya juu. Hivyo kuna utofauti mkubwa wa kiisimu katika
makabila ya Tanzania.
Utamkaji wa maneno,
pia katika utamkaji wa maneno kuna utofauti mkubwa sana kutokana na makabila.
Kwa mfano kabila la wahaya neno ng’ombe
wenyewe husema ngombe, lakini pia
wakurya wametawaliwa sana na matumizi ya r,
kwa mfano neno kula ambacho ni
kitendo wenyewe husema au hutamka kura.
Hivyo kuna utofauti mkubwa sana wa utamkaji wa maneno katika makabila ya
Tanzania.
Msamiati, kila
lugha ina utaratibu wake wa kujisimamia katika msamiati. Hii hupelekea
kutofautiana kwa misamiati katika makabila hapa Tanzania. Kwa mfano neno makande hutamkwa kwa misamiati
tofautitofauti kutokana na kabila lenyewe. Wasukuma husema masangu lakini wanyakyusa husema ingati, hivyo kuna utofauti mkubwa sana kimsamiati.
Baada
ya kuangalia tofauti za matumizi ya lugha kiisimu, ngoja tuone tofauti za kilahaja
katika matumizi ya lugha. Hapa nitajikita zaidi katika kabila la wahaya na kabila la wazinza ambao wametenganishwa na ziwa Victoria:-
Msamiati,
katika msamiati wazinza na wahaya hutofautiana sana. Katika Kiswahili kuna
maji, wazinza husema amenzi na wahaya
husema amaizi. Pia neno kesho wazinza
husema nyencha wakati wahaya husema nyenkya Hivyo katika msamiati kuna
utofauti wa kilahaja kati ya wazinza na wahaya kwani kuna vijitofauti
vidogovidogo vinavyojitokeza katika maneno yaani msamiati.
Sentensi,
kuna tofauti ya kilahaja katika sentensi za kizinza na zile za kihaya.
Kwa mfano katika
Kiswahili: mama amelala
Kihaya: mai
yanyamile.
Kizinza: maa
yalyamile
Hapo
tunaona katika sentensi kuna tofauti ndogondogo zinazojitokeza, mpangilio wa
maneno upo sawa lakini tofauti ipo kwenye nomino mai kwa wahaya na maa kwa
wazinza. Na katika kitenzi yanyamile
kwa wahaya, na yalyamile kwa wazinza.
Mofolojia,
katika hii taaluma inayohusika na maumbo wazinza na wahaya hutofautiana kwa
kiasi kidogo sana.
Kwa mfano:
Kiswahili-anasoma
Kihaya- nashoma
Kizinza- nasoma
Kwa
kuangalia mifano hiyo tunaweza kuona kwamba katika kutenganisha viambishi
hufuata kanuni moja, kwa mfano kinapokaa kiambishi cha njeo kwenye kihaya ndipo
pia hukaa katika kizinza isipokua hutofautiana katika mzizi. Kihaya mzizi ni shom na kizinza mzizi ni som.
Matamshi, katika
matamshi wahaya hutamka maneno ya mwanzo kwa juu na kumalizia kwa kushusha
sauti wakati wazinza hutamka kwa sauti iliyo lala.
Kwa mfano Kiswahili-
jembe
Kihaya- enfuka
Kizinza- enfuka
Neno
“e” kwa wahaya hutamka kwa juu sana na kumalizia maneno mengine kwa sauti ya
chini sana, wakati wazinza hutamka kwa sauti ya kulala.
Kiujumla
kila lugha inatofautiana na lugha nyingine katika Nyanja mbalimbali zikiwemo
matamshi, maumbo, msamiati na maana ya maneno. Hivyo ni vizuri kwa kila
watumiaji wa lugha(makabila) watumie lugha kutokana na eneo wanaloishi kwani
kuna baadhi ya maneno yakitumiwa katika mazingira mengine hubadili maana.
MAREJELEO
Msanjila,
Kihole, Massamba(2011): IsimuJamii Sekondari Na Vyuo. TUKI, UDSM.
TUKI
(2013): Kamusi ya Kiswahili sanifu.
Chuo kikuu cha Dar es Salaam.
Comments
Post a Comment