Skip to main content

Posts

Showing posts from December, 2017

RIWAYA YA MOTO WA MIANZI

MOTO WA MIANZI MAUDHUI SWALI:  Chambua Maudhui ya Riwaya ya Moto wa Mianzi Historia fupi ya Mwandishi na utunzi wa kazi yake : RIWAYA YA MOTO WA MIANZI; ni riwaya iliyoandikwa na mwandishi aitwaye Mugyabuso Mulokozi. Alizaliwa tarehe 7 Juni mwaka 1950. Mugyabuso Mulokozi ni muhadhiri katika chuo kikuu cha Dar es Salaam. Mwandishi huyu pia ameweza kuandika kazi mbalimbali. Baadhi ya kazi zake ni: ·           Mashairi ya kisasa aliyoandika kwa kushirikiana na K.K Kahigi. ·           Malenga wa Bara aliyoandika pamoja na K.K Kahigi ·           Mukwava wa Uhehe ·           Kunga za Ushairi na Diwani yetu aliyoandika pamoja na K.K Kahigi ·           Ngome ya Mianzi ·           Ngoma  ya Mian...

TAHAKIKI YA RIWAYA YA KUSADIKIKA

UTANGULIZI  Katika kujadili vipengele mbalimbali vya Fani na maudhui vilivyotumiwa katika riwaya ya kusadikika iliyoandika na Shaaban Robert Washiriki hatukujikita zaidi katika kujadili maana ya riwaya za wataalamu mbalimbali bali tuliweza kujadili kazi hii kwa kuchambua vipengele vya fani na maudhui kutokana na masimulizi ya nchi ya Kusadikika.  Masimulizi ya kitabu kwa kifupi.  Riwaya ya kusadikika ni kitabu kinachoelezea masimulizi ya nchi ya kusadikika ambayo mwandishi ameanza kwa kusimulia tukio la kushitakiwa kwa Karama ambaye ndiye Mhusika mkuu kwa tuhuma za kuihujumu serikali ya Kusadikika. Kwa maelezo ya Waziri Majivuno aliwasilisha mashitaka haya mbele ya Mahakama eti kwa sababu Karama alikuwa akitoa elimu ya sheria ambayo kwa Mtazamo wa Waziri huyu alidai kuwa angewafanya raia wa kusadikika kuelewa haki zao ambako kungepelekea wananchi hao kutotii serikali au kwa namna nyingine kungekomesha unyanyasasaji, uonevu na uongozi mbaya wa watawala wa kusadikika na hi...

TAHAKIKI YA RIWAYA YA NAGONA NA MZINGILE (KEZILAHABI)

UCHAMBUZI WA RIWAYA ZA “NAGONA” NA “MZINGILE” 1.0 Utangulizi Katika makala haya tutachambua riwaya za ‘Nagona’ na ‘Mzingile’. Katika kuchambua riwaya hizi tutajikita katika kuangalia baadhi ya vipengele kama dhamira, falsafa, lugha, mtindo wa usimulizi, wahusika, motifu na suala la ontolojia. 2.0 Maelezo kuhusu mwandishi na riwaya zake 2.1 Maelezo kuhusu mwandishi Euphrase Kezilahabi alizaliwa mwaka 1944 katika kijiji cha Namagondo kilichoko kisiwani Ukerewe katika ziwa Victoria nchini Tanzania. Alipata elimu ya msingi huko kijijini Ukerewe na baadaye alijiunga na seminari ndogo ya Nyegezi kwa ajili ya masomo ya upili. Baada ya kumaliza alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es salaam mnamo mwaka 1967. Katika masomo yake alijishughulisha na nadharia mbalimbali zihusuzo falsafa (Wamitila 1991:64). Mnamo mwaka 1976 alitunukiwa shahada ya umahiri ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam, kabla ya kutunukiwa shahada nyingine ya umahiri ya Chuo Kikuu cha Wisconsin-Madison mwaka 1982. Mwaka 1985, Kez...