Hii dunia si kitu, bila wewe amini,
Si utu siyo mtu, kufika yako thamani,
Si jiwe wala msitu, cha kukuzidi ni nini?
Tangu haujazaliwa, deni lilionekana,
Dunia ilidaiwa , kulipa lazima sana,
\hapana kudhulumiwa, dhuluma hushindikana,
Bila ya uwepo wako,dunia itadaiwa.
Siku waliona jua,mbingu na nchi zilicheka,
Siyo kuja kuungua, bali ni kuneemeka,
Wewe muhimu tambua, hili ichwani weka,
Bila ya uwepo wako,dunia itadaiwa.
Pia wewe ni mzuri, mzuri mzuri sana,
Nikiuandika uzuri, nitaandika sana mbona,
Sauti na sura nzuri,na rangi ing’aayo sana,
Bila ya uwepo wako, dunia itadaiwa.
Mama namsifu sana, ndugu na jamaa zako,
Mola asifiwe jana, leo na kesho yako,
Na nani walingana, hayupo mahali pako,
Bila ya uwepo wako,dunia itadaiwa.
Nini kitachokuliza,na kujitoa thamani?
Nani hatokuliwaza, kufanya ujiamini?
Na nini utachowaza, hadi useme kwa nini?
Bila ya uwepo wako,dunia itadaiwa.
Hii dunia si kitu, bila ya uwepo wako,
Wewe mtu siyo kitu, hakuna badala yako,
Kwetu tungesema mbwitu,sitaki machozi yako,
Bila ya uwepo wako, dunia itadaiwa.
Wewe ni wa pekee sana ,mama unalitambua,
Na wewe tutaungana, furaha kuuvumbua,
Popote hutogombana, wache tutawaumbua,
Bila ya uwepo wako,dunia itadaiwa.
Wewe upo ni mmoja, mmoja na wa pekee,
Itakuwa ni kiroja, cheko lako lipotee,
Sitaki kusema ngoja, upenbdo uungojee,
Bila ya uwepo wako,dunia itadaiwa.
Mapenzi matamu mama, ya mume ama mama,
Ila usije simama, kujaribu paso pema,
Kwa mola ukaungama, eti sitorudi nyuma,
Bila ya uwepo wako,dunia itadaiwa.
Mama asubiri ndoa, ndoa iliyo halali,
Bridgita kuzogoa, najua wako kimwali,
Marcus akikuboa, wala usiwe mkali,
Bila ya uwepo wako,dunia itadaiwa.
Leo miaka kadhaa, tangu waliona jua,
Wala siapate hadaa, za wanojifaya kujua,
Ukwepeshwe mabalaa, Vai mama kamua,
Dunia si chochote,bila ya uwepo wako.
Nmazuri sana mashairi
ReplyDeleteasante sana ucjal tupo pamoja
Delete