SHAIRI: KUMBUKUMB YA HAYATI MORINGE SOKOINE


LEO UNGEKUWA NANI?
Sasa miongo mitatu,wajina hatukuoni,
Wanalalamika watu,kama wewe hawamwoni,
Kuvaa vyako viatu,katu haiwezekani,
Leo ungekuwa nani,Moringe wa sokoine,


Wengi wasema raisi,wa muungano wetu,
Eti nawe ungeasi,kukiacha chama chetu,
Angekuona raisi,utunge katiba yetu,
Leo ungekuwa nani,Moringe wa sokoine.


Alokufwata monduli,tunaambiwa fisadi,
Chamani hawamjali,yuko bize na miradi,
Ilikuua ajali,kukukosa ilibidi,
Leo ungekuwa nani,Moringe wa sokoine.

Nimefika morogoro,ulipopata ajali,
Kule kuna mogogoro,leo ardhi mali,
Ninapatwa na kihoro,kuhusu yako ajali,
Leo ungekuwa nani,Moringe wa sokoine.

Nitakuja kutazama,mahali ulipolala,
Kisha nende Butiama,nyerere alipolala,
Moyoni inanichoma,sijakuona mahala,
Leo ungekuwa nani,Moringe wasokoine.

Najuta sijakuona,mie wale wa tisini,
Nimepewa lako jina,nalitumia shuleni,
Kwenye picha nakuona,nimetunza chumbani,
Ulazwe pema peponi,Moringe wa jina wangu......

Comments

  1. Habari bloga kwa kuzingatia kanuni ya umiliki wa kazi za kibunifu....naomba uyaondoe mashari yote ya mteja wangu likiwemo hili kabla ya kufikishana kwenye vyombo vya sheria

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

NOTES ZA USHAIRI

MBINU ZA KUFUNDISHIA

DHANA YA USHAIRI ILIVYOFAFANULIWA NA WATAALAMU MBALIMBALI