Kama ndiko kufanana,ni zaidi ya mayai,
Unaweza kugombana,jibu lako kulidai,
Si urefu si upana,kasoro huing'amui,
NI KIPELE JIPU CHANGA,WALIMU NIAMBIENI.
Wapo walopata sifa,kudai ni jipu changa,
Nasi wasaka marifa,twashindwa kipi kulonga,
Vichwa vinapata nyufa,fikra zikijigonga,
NI KIPELE JIPU CHANGA,WALIMU NIAMBIENI.
Wengine ni kaupele,kovu lake halidumu,
Wala huhitaji shule,wala siyo jambo gumu,
Hutotoa ukelele,kukamua siyo sumu,
NI KIPELE JIPU CHANGA,WALIMU NIAMBIENI.
Huenda likawa jipu,tusubiri tukajua,
Sije sema chupu chupu,jipu lingejiotea,
Na msindi tumpe supu,jibu akilipatia,
NI KIPELE JIPU CHANGA,WALIMU NIPENI JIBU.
Jipu huliacha kovu,kovu kubwa la kidonda,
Kama macho ni mabovu,tapapasa ukipenda,
Ama kwa wako uchovu,uliza acha kuponda,
NI KIPELE JIPU CHANGA,WALIMU NIAMBIENI.
Wengine ni kaupele,kovu lake halidumu,
Wala huhitaji shule,wala siyo jambo gumu,
Hutotoa ukelele,kukamua siyo sumu,
NI KIPELE JIPU CHANGA,WALIMU NIAMBIENI.
Huenda likawa jipu,tusubiri tukajua,
Sije sema chupu chupu,jipu lingejiotea,
Na mshindi tumpe supu,jibu akilipatia,
NI KIPELE JIPU CHANGA,WALIMU NIPENI JIBU
Comments
Post a Comment