SHAIRI: NI TAA YA AFRICA

Yang'aa kila dakika, na kuburudisha moyo,
Wachache waaliofika, umewatoka uchoyo,
Yeyote atamwalika, akaliwazike moyo,

Hii taa ya labuka, kaiweka hapa kwetu,
Ni kama kaisimka, na miale  yake butu,
Haitakuja zimika, wala kuja shika kutu.

Kama mtu anacheka, meno yake ya  kung’aa,
Siku jua likiwaka, waweza ukazubaa,
Wengi wameweweseka, kuiona hii taa.

Ulaya na Amerika, sifa zake zasikika,
Wametamani kufika, nao wakasuuzika,
Wachache waliofika,wamependa Afrika,

Nami nilihamanika, awali nilipoona,
Homa iliyonishika, walai sikuiona
Kweli niliweweseka, ile taa kuiona.

Ndoto zilikamilika, kwa watu nilijivuna,
Kuishika nilitaka, japo ipo juu sana,
Nguvu ziliongezeka, kila nilipoiona.

Picha ndani nimeweka, wanangu waje ziona,
Yeyote akizitaka, nitampa kuziona,
Na yeye nitamtaka, aende haraka sana.

Twende bila ya kuchoka, ili iwe kumbukumbu,
Hata wao wakifika, wasitwone mambumbumbu,
Waijue Afrika, si bara la mbumbumbu,

Hii taa itawaka,tukitunza kwa makini,
Mafuta haitataka, babda wetu umakini,
Tuipitishe miaka, wabaki waitamani,

Hii taa inawaka ,tuitunze vema sana,
Mwangaza ukitoweka, tutalaumiwa sana,
Majirani watacheka, aibu tutaiona.

Comments

Popular posts from this blog

NOTES ZA USHAIRI

MBINU ZA KUFUNDISHIA

DHANA YA USHAIRI ILIVYOFAFANULIWA NA WATAALAMU MBALIMBALI