Skip to main content

SHAIRI: NMPE NINI MAMANGU?

Alinilea mapema,kabla ya kuona jua,
Ninamheshimu mama,kweli nimemsumbua,
Hadi leo nasimama,na kuongea najua,
Mama nitakuheshimu,umefanya mengi kwangu.

Usiku haukulala,mie waniangalia,
Waja kujua hujala,wengine wamesinzia,
Mie nikigalagala,shuka lako nafunua,
Mama ninakushukuru,sijui nikupe nini.

Mama wewe unapika,mie kukaa sipendi,
Mama yangu umechoka,mie kulia hupendi,
Mama umeshughulika,mama wewe ni mshindi,
Mama wewe ni shujaa,mola anakutambua.

Baba karudi usiku,wewe wamfungulia,
Kanywa pombe wamshuku,ila hujamnunia,
Huko amekula kuku,wengine kanunulia,
Mama umevumilia,ushindi utakujia.

Leo baba hanywi pombe,na pia akusifia,
Kimwona ana kikombe,maziwa anajinywea,
Kikumbuka usiombe,baba yangu atalia,
Mama nikulipe nini,ishi nami siku zote.

Mama unachechemea,ulipigwa wanambia,
Kweli sikutegemea,mama unavumilia,
Mungu wamtegemea,muumba waniambia,
Mama umebarikiwa,mbinguni tapokelewa.

Si kwamba nakusifia,baba nimemchukia,
Yeye pia kanilea,siwezi kumchukia,
Heshima nampatia,yeye anihudumia,
Mama yangu nakupenda,wewe ni shujaa wangu.

Mama mungu akulinde,wewe umebarikiwa,
Matatizo uyashinde,mjukuu waletewa,
Pia baba umpende,mama utabarikiwa,
Mama yangu wewe bora,utabaki kuwa bora..

Comments

Popular posts from this blog

NOTES ZA USHAIRI

USHAIRI     NI    NINI ? Shaaban Robert katika uandishi wa ushairi ameandika Tenzi na mashairi ya kimapokeo. Tenzi : Ni aina ya mashairi ya kimapokeo wenye sifa zifuatazo: Kimaudhui ; Ni utungo wenye maudhui yanayosimulia kwa urefu tukio fulani maalum. Waweza kuwa wasifu wa mtu au jambo la kihistoria. Mfano; S. Robert ameandika utenzi wa vita vya Uhuru, ameeleza kuhusu historia. Pia katika Mapenzi Bora, ameeleza kuhusu sifa za mapenzi bora. Utenzi ni utungo wa pili kati tungo za ushairi zenye beti nyingi. Utungo wa kwanza unaoongoza kuwa na beti nyingi kuliko zote katika ushairi ni Tendi. Lakini hapa tutaangazia tenzi zaidi. Utenzi hauna mizani nyingi aghalabu mizani nane, hauna mshororo bali una nusu mshororo/kipande mstari. Vilevile katika utenzi kipande mstari hakigawiki. Pia katika kipande mshororo kuna vipande vinne kwa kila ubeti. Mistari mitatu ya kwanza huwa na vina vyenye urari na kipande mstari cha mwisho/cha nne huwa na kina tofauti na vipande vya mw

DHANA YA USHAIRI ILIVYOFAFANULIWA NA WATAALAMU MBALIMBALI

Ushairi kama moja kati ya tanzu za fasihi inayowasilishwa katika namna zote aidha kwa lugha ya maandishi au kwa lugha ya masimulizi una mchango au nafasi kubwa sana katika kunufaisha au kustawisha maisha ya binadamu kwa kumuelimisha, kumsisimua, kutunza na kuhifadhi amali zake pamoja na kukuza na kuendeleza lugha yake kama moja kati ya vipengere muhimu maishani mwake. Ushairi kama nudhumu katika fasihi simulizi hujumuisha nyimbo, ngonjera, tenzi na mashairi yenyewe. Ushairi wa Kiswahili waweza kuainishwa katika tanzu au katika kumbo mbalimbli kama asemavyo Mulokozi (1996) kuwa zipo kumbo kuu tatu ambazo ni ushairi wa kijadi au kimapokeo, ushairi wa mlegezo au huru na ushairi wa maigizo. Wanazuoni wafuatao wa mashairi ya kimapokeo wametoa maana za ushairi kama ifuatavyo:- Shaaban Robert (1958:37). “Ushairi ni sanaa inayopambanuliwa kama nyimbo, mashairi na tenzi. Zaidi ya kuwa na sanaa ya vina, ushairi una ufasaha wa maneno machache au muhtasari…, mawazo, maoni na fikra za ndani zi

KISWAHILI FORM 1: FASIHI SIMULIZI

KISWAHILI Form 1 Topic 4 FASIHI SIMULIZI Fasihi simulizi ni moja kati ya tanzu za fasihi inayohifadhiwa na kurithishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine kwa njia ya mdomo. Katika mada hii utajifunza na kisha utaweza kubainisha tanzu na vipera vya fasihi simulizi pamoja na ufafanuzi wake. Na pia utaweza kutofautisha kati ya kipera na kipera au kati ya utanzu na utanzu. Ubainishaji wa Tanzu za Fasihi Simulizi Tanzu za Fasihi Simulizi Bainisha tanzu za fasihi simulizi Fasihi Simulizi ni kazi ya fasihi inayohifadhiwa na kurithishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine kwa njia ya mdomo kama vile; hadithi, ngoma na vitendawili. Tanzu za Fasihi Simulizi ni pamoja na hizi zifuatazo: Masimulizi/hadithi Semi Ushairi Mazungumzo Maigizo Ngomezi Ufafanuzi wa Vipera vya Tanzu za Fasihi Simulizi Vipera vya Hadithi Fafanua vipera vya hadithi SIMULIZI/ HADITHI Masimulizi ni fasihi yenye kusimulia habari fulan