Habarini marafiki,mlofunga hongereni, Nitakuwa mnafiki,nikijifanya sioni, Siyo ishara ya dhiki,bali mwongozo wa dini, Zaidi ya kutokula,funga ina mengi mambo. Wagonjwa na wengineo,mlioshindwa kufunga, Myafanye megineyo,itakavyo yenu funga, Sio kucheka wenzio,eti yule hakufunga, Zaidi ya kutokula,funga ina mengi mambo. Wewe usiye husika,naomba acha makwazo, Sije mtu kwazika,wewe ukawa ni chanzo, Mtu dini kaishika,kwako liwe kubwa funzo, Zaidi ya kutokula,funga ina mengi mambo. Na humu mitandaoni,si sehemu ya dhihaka, Eti nani simuoni,siyo lazima kwandika, Si mtafute simuni,siyo humu kuanika, Zaidi ya kutokula,funga ina mengi mambo. Pia ule unafiki,kujifanya umefunga, Waenda kwa marafiki,kuharibu yako funga, Mola hilo haafiki,ni bora usingefunga, Zaidi ya kutokula,funga ina mengi mambo. Liombeeni taifa,msisahau dunia, Tuyaepuka maafa,mola atawasikia, Pia wale walokufa,huko naijeria, Zaidi ya kutokula,funga ina mengi mambo.... |
USHAIRI NI NINI ? Shaaban Robert katika uandishi wa ushairi ameandika Tenzi na mashairi ya kimapokeo. Tenzi : Ni aina ya mashairi ya kimapokeo wenye sifa zifuatazo: Kimaudhui ; Ni utungo wenye maudhui yanayosimulia kwa urefu tukio fulani maalum. Waweza kuwa wasifu wa mtu au jambo la kihistoria. Mfano; S. Robert ameandika utenzi wa vita vya Uhuru, ameeleza kuhusu historia. Pia katika Mapenzi Bora, ameeleza kuhusu sifa za mapenzi bora. Utenzi ni utungo wa pili kati tungo za ushairi zenye beti nyingi. Utungo wa kwanza unaoongoza kuwa na beti nyingi kuliko zote katika ushairi ni Tendi. Lakini hapa tutaangazia tenzi zaidi. Utenzi hauna mizani nyingi aghalabu mizani nane, hauna mshororo bali una nusu mshororo/kipande mstari. Vilevile katika utenzi kipande mstari hakigawiki. Pia katika kipande mshororo kuna vipande vinne kwa kila ubeti. Mistari mitatu ya kwanza huwa na vina vyenye urari na kipande mstari cha mwisho/cha nne huwa...
Comments
Post a Comment