SWALI.
“Lugha
haina uhusiano wowote na jamii hali kadhalika jamii haina uhusiano wowote na
lugha”. Jadili kauli hii.
Lugha;
ni mfumo wa sauti za nasibu zilizokua katika mpango maalumu na zilizokubaliwa
na jamii ya watu fulani ili zitumike katika mawasiliano.
TUKI
(2013),kamusi ya Kiswahili sanifu,
Lugha ni mpangilio wa sauti
na maneno unaoleta maana ambao hutumiwa na watu wa taifa au kundi fulani kwa
ajili ya mawasiliano. Lugha ni maneno pamoja na matumizi yake.
Jamii
ni mkusanyiko wa watu wanaoishi kwa pamoja katika eneo moja la kijiographia
wakiunganishwa na historia yao na wakitambuliwa kwa utamaaduni wao,lugha, mila
na desturi,
Uhusiano
ni hali ya ukalibu ujirani, urafiki au ushirikiano unaojengeka baina ya ndugu ,
jamaa au marafiki. Uhusiano ni hali ya kuwa pamoja kifikira ,kimwili
kimawasiliano , kiimani, kimaendeleo, kikazi, kijamii na kimichezo.
Hakuna
ukweli wowete kuhusu kauli isemayo kwamba’’ lugha haina uhusiano wowote na
jamii , hali kadhalika jamii haina uhusiano woote na lugha’’ bali kuna uhusiano mkubwa unaojitokeza baina
ya pande hizi mbili kama ifuatavyo:-
Lugha ni zao la jamii, kwani
chanzo cha lugha ni pale tu binadamu walipoanza kuishi pamoja na kukabiliana na
mazingira yao, ambapo binadamu alibuni namna ya kuwasiliana. Kwa upande
mwingine lugha ni sehemu ya utamaduni wa
jamii husika pia ni njia inayotumiwa na wanajamii ili kueleza na kusambaza utamaduni.
Hutambulisha kazi za jamii,
katika muktadha ya shughuli mbalimbaili
huwepo istilahi na misamiati anuai ambayo wahusika wa kazi au shughuli hizo
hutumia wakati wanaposhughulika. Istilahi na misamiati hiyo huwafanya waonekane
kuwa tofauti na wanajamii wanaofanya kazi nyinginezo. Mfano istilahi
zinazotumiwa na watu wanaofanya kazi hotelini (chai mbili, wali ng’ombe),
hospitalini (mbili kutwa mara tatu kwa siku tatu yaani - 23, wachungaji au mashekhe
(bwana Yesu asifiwe, assallam-alleikum, tak-biir) na makuli (lugha za matusi). Lugha hizi
hufanya hata watu wengine watambue shughuli zao.
Lugha hurejelea mazingira ya jamii
husika, lugha ina tabia ya kurejelea au kusadifu mazingira
halisi ya jamii fulani aghalabu jamii za pwani, huzungumzia zaidi mazingira ya
kipwani kutokana na shughuli zinazofanywa na watu wa pwani kama uvuvi. Kwa
mfano mzaramo au mndengeleko wa pwani badala ya kuzungumza lugha zinazohusu
uvuvi na michezo ya bao, huzungumza lugha zinazohusu ufugaji awapo umasaini
Arusha au usukumani Shinyanga.
Lugha huongoza mawazo ya jamii, kwa
kawaida mtu hujenga fikra kichwani kwa kutumia lugha. Aghalabu wazo hilo
analolifikiria huundwa kwa lugha yake ya msingi, kwa mantiki hiyo hata mtu
akiwa mahili wa lugha zaidi ya moja huanza kujenga wazo kwa lugha yake ya
kwanza ndipo alitoe wazo hilo kwa lugha ya pili. Kwa mfano watanzania walio
wengi ambao lugha yao ya kwanza ni Kiswahili, huwaza kwa Kiswahili kwanza ndipo awasilishe mawazo yake katika
lugha hiyo ngeni.
Luhga huhifadhi amali za jamii,
lugha hutumika kutunza mila na desturi ambazo ndizo amali za jamii husika. Katika
kazi za kisanaa kama vile fasihi simulizi na fasihi andishi ambapo lugha
hutumika kuzielezea amali hizo kupitia aina hizo mbili. Katika tamthiliya ya
Kinjekitile inaonesha ni jinsi gani jamii zilivyohusika katika vita ya majimaji,
hivyo huonesha historia ya jamii husika.
Lugha ni chombo cha kufundishia
jamii, kwa mfano jamii ambazo zinajihusisha na masuala ya
jando na unyago, vijana hupewa mafunzo kutokana na jinsia zao. Kwenye unyago
vijana wa kike hupewa mafunzo ya jinsi gani ya kuishi na familiya zao, na
vijana wa kiume hupewa mafunzo ni jinsi gani ya kuishi na familiya zao.
Lugha huishikamanisha jamii, wanajamii
kwa kawaida hutumia lugha katika kufanya ushirikiano kwenye shughuli mbalimbali
zihuzo maisha yao ya kila siku. Ni katika shughuli za nyanja zote za maisha, yaani; kisiasa,
kiuchumi, kiutamaduni,na hata kiitikadi kwa kawaida lugha kama chombo cha
mawasiliano ndiyo inayowafanya kushirikiana au kushikamana. Kwa mfano wanasiasa
katika majukwaa ya kampeni hutumia lugha kuwaalika watu wakusanyike na kuwaomba wawapigie kura wakati wa uchaguzi,
pia katika mikusanyiko ya kidini lugha ndiyo inayowakusanya na kuwashikamanisha
wanajamii katika suala hilo la kiitikadi.
Lugha hutambulisha jamii, wanajamii
wengi huathiriwa na lugha zao mama hususani lafudhi. Yaani hatakama mwanajamii
atakuwa anajua na kutumia lugha zaidi ya moja kwa kawaida hujikuta akitumia
lafudhi yake ya lugha mama kuzungumzia
lugha nyinginezo. Jambo hili huwafanya watu hawa kutambulika hata wanapofanya
mazungumzo na watu wengine wasio wa makabila yao. Mfano wasukuma, wachaga,
wahaya, wamakonde na wamasai hujulikana wanapozungumza hata na watu wasio wa makabila hayo.
Lugha hurithisha mila na desturi za
jamii, hii ni kutokana na baadhi ya tamaduni za jamii
husika kutumia lugha kuwafundisha au kuwapa elimu vijana wa jamii hiyo waweze
kutambua mila na desturi za jamii yao. Kupitia lugha vijana huweza kutambua
masuala mbalimbali yanayowahusu hasa yanayofaa kutendwa na jamii yao na yapi
yasiofaa kutendwa na jamii yao. Kwa mfano baadhi ya makabila huwakataza watoto
wao wasioe au kuolewa na kabila fulani kwa sababu mbalimbali wanazozijua wao.
Kwa
ujumla lugha haiwezi kutenganishwa na jamii hata kidogo, hii ni kutokana na
lugha kuwa muhimili ulio imara wa jamii. Kwa hivyo yaweza kusemwa kuwa, bila
lugha jamii haiwezi kuwepo kwa kuwa lugha hutumika katika suala zima la kujenga
jamii. Kwa mfano jamii ya watu wa afrika mashariki pengine isingekuwepo kama
kusingekuwa na lugha ya kuwafanya wawe jamii.
MAREJELEO.
Ø King’ei,
K. (2010). Misingi ya isimu jamii.
Taasisi ya taaluma za Kiswahili: chuo kikuu cha Dar es salaam. Tanzania.
Comments
Post a Comment