Jiandae na BTP shule za msingi na sekondari

  1. Taja mambo mawili unayoangalia ili mwanafunzi wako ayaweze unapomfundisha msamiati.
  2. Eleza unavyoelewa istilahi zifuatazo katika somo la Kiswahili;
    1. Ufaraguzi
    2. Kongamano
    3. Tathimini
    4. Msamiati
  3. Eleza shabaha mbili (2) za kufundisha vitendawili katika shule za msingi.
  4. Eleza sifa mbili (2) za Vitendawili.
  5. Maandalio ya Somo ni nini?
  6. Orodhesha vyanzo vitatu tu vya maandalio ya somo
  7. Ni mambo gani muhimu yanayosaidia kuzungumza na kusikiliza kuwepo (Misingi ya kusikiliza na kuzungumza). Taja manne (4) tu.
  8. Eleza kwa kifupi mambo yanayofanyika katika ngazi ya matayarisho ya kufundisha kusoma.
  9. Zipo sababu nyingi zinazofanya wanafunzi washindwe kusoma katika viwango mbalimbali. Ukirejea mtoto wa darasa la tatu, unafikiri sababu hizo ni zipi? Taja sababu zinazotokana na mazingira ya shuleni.
  10. Wewe kama mwalimu katika darasa la tatu unafikiri hati nzuri ni ipi?
  11. Eleza utafundishaje nahau “Unga mkono” kwa mbinu ya maelezo katika darasa la sita.
  12. Eleza Mazoezi matano (5) yafaayo kutolewa kwa wanafunzi wa darasa la saba baada ya kufundisha usimulizi wa hadithi Fulani.
  13. Unapofundisha wanafunzi wa darasa la tano juu ya uandishi wa barua rasmi unatakiwa kuzingatia na kusisitiza juu ya mambo muhimu kumi (10) ili wayafahamu. Yataje.
  14. Fafanua sababu na hatua za kufundisha mwandiko katika darasa la kwanza.
  15.  Lugha ni nini?
  16. Taja sifa zisizopungua sita (6) za lugha yeyote ile.
  17. Taja malengo mawili (2) ya kufundisha Kiswahili kwa wanachuo wa kozi ya ualimu daraja la A.
  18. Taja vifaa vya mtaala vya somo la Kiswahili viwili (2) vinavyomhusu zaidi mwanafunzi wa shule ya msingi katika harakati za kujifunza somo hilo.
  19. Eleza matumizi mawili (2) tu ya Muhtasari wa somo la Kiswahili kwa mwalimu afundishaye somo hilo katika shule za msingi.
  20. Taja stadi kuu nne (4) za lugha ya Kiswahili kwa mfululizo au mpangilio wa ufundishaji na ujifunzaji wake.
  21. Andika methali tatu (3) zinazofanana na hii ifuatayo; “Asiyesikia la mkuu huvunja guu”.
  22. Taja matumizi matatu (3) ya kitabu cha kiongozi cha mwalimu wa somo la Kiswahili.
  23. Mbinu za kufundishia na kujifunzia zifuatazo hazifai kufundishia Kiswahili, “ziara” na “majadiliano”. Eleza kwa nini?
  24. Kwa nini Mwalimu wa somo la Kiswahili katika shule za msingi lazima azingatie malengo ya somo kwa wanafunzi wake?
  25. Taja na fafanua nyanja tatu (3) za Elimu katika somo la Kiswahili.
  26. Eleza muundo wa muhtasari wa somo la Kiswahili wa shule za msingi.
  27. Eleza madhara yampatayo mwanafunzi afundishwaye na mwalimu bila kuwa na muhtasari wa somo la Kiswahili.
  28. Fafanua nadharia mbili (2) zinazoelezea dhana ya kufundisha.
  29. Kufundisha ni nini?
  30. Taja mambo manne (4) yanayoangaliwa wakati mwanafunzi anapofundishwa kusoma kwa sauti.
  31. Tunga sentensi moja moja kwa kutumia Nahau zifuatazo kuonesha dhana yake:
    1. i)  Moyo            iii) Tia fora
    2. ii) Anika juani  iv) Bega kwa bega
  32. Taja zana nne (4) unazodhani zinafaa kufundishia kusoma katika darasa la Pili.
  33. Bainisha makundi manne (4) ya Barua.
  34. Kwa nini Somo la Imla hufundishwa katika Shule za msingi. Toa sababu mbili tu.
  35. Kwa kutumia michoro ya mishale onesha utawafundishaje wanafunzi wa darasa la Kwanza kuandika herufi na namba zifuatazo:-
    1. i)  a                     iii) 8
    2. ii)  s                      iv) 5
  36. Taja namna utakavyomwezesha mwanafunzi wa darasa la Kwanza kukuza Stadi ya kuzungumza.
  37. Taja namna fasihi inavyojitokeza katika somo la Kiswahili katika Shule za Msingi.
  38. Ainisha maneno yaliyounda sentensi ifuatayo:- “Gari langu jana limeharibika vibaya sana sana”.
  39. Eleza hatua za kufuata katika kufundisha Utungaji (maelezo ya picha) ukitumia mbinu ya mazungumzo.
  40. Eleza utafundishaji mada ya Ufahamu kwa wanafunzi wa darasa la nne lenye wanafunzi 60 huku ukiwa na vitabu sita vya kiada.
  41. Fafanua matumizi ya Stadi ya Kuandika katika maisha ya kila siku ya kijana aliyehitimu vema Elimu ya Msingi.
  42. Eleza hatua za kufuata wakati wa kufundisha mada ya Kiswahili kwa kutumia mbinu ya Igizo.
  43. “Uchaguzi wa mbinu nzuri ya kufundisha jambo Fulani katika Kiswahili, hutegemea sana vigezo mbalimbali avichunguzavyo Mwalimu wa somo”. Jadili.
  44. Bainisha vipengele vyote muhimu vlivyomo kwenye andlio la somo
  45. Taja mambo manne (4) yanayozingatiwa wakati wa kufundisha kusoma kwa sauti katika shule za msingi.
  46. Taja vifaa vitatu (3) vya mtaala wa somo la Kiswahili vitumikavyo kufundishia katika shule za msingi na uvitolee maelezo mafupi.
  47. Andika mbinu tatu (3) utakazotumia kufundishia msamiati darasa la III na VII.
  48. Eleza sababu tatu (3) za umuhimu wa kufundishia stadi za kuzungumza na Kusikiliza.
  49. Taja malengo mawili (2) ya kufundisha Kiswahili shule za msingi nchini Tanzania.
  50. Taja sifa tano (5) za madhumuni mahususi. Ainisha sifa hizo kwa kuhusisha mfano mmoja wa lengo mahususi la Kiswahili.
  51. Mwanafunzi wa lugha ya Kiswahili huweza kujifunza na kumudu haraka lugha hii kwa kutumia stadi zipi za lugha?
  52. Ikiwa unahitaji kufundisha mada ndogo ya “Msamiati” katika darasa la tano:
    1. Taja mada utakayotumia.
    2. Lengo mahususi utakalolitekeleza ni lipi?
    3. Taja rejea mojawapo utakayotumia.
  53. Shule za msingi huzingatia madhumuni yaliyowekwa na Taifa katika ufundishaji wa somo lolote.
    1. Taja madhumuni mawili tu ya kufundisha Kiswahili katika shule za msingi.
    2. Eleza kwa ufupi madhumuni ya kufundisha Kiswahili darasa la saba. Taja mawili tu.
  54.  (a) Kwa kutumia mifano eleza maana za nomino, kivumishi, kielezi na kihisishi.
     (b) Eleza hatua utakazofuata katika kufundisha Imla kwa darasa la tatu.
55. Fafanua dhana “Zana za kufundishia” pamoja na dhima zake tano (5).
56. (a) Taja matatizo manne (4) yanayomkabili mwalimu wa somo la Kiswahili wa shule za msingi.
      (b) Eleza utatatuaje matatizo mawili (2) kati ya uliyotaja ili kufanikisha tendo la kufundisha na wanafunzi kujifunza bila shida.
57. Andika andalio la somo la dakika 40 kwa wanafunzi wa darasa la V ukionesha hatua za kufundisha mada yoyote ya darasa hilo.
58. Mjadala ni moja ya mbinu za kufundishia Kiswahili. Eleza;
  • Maana yake.
  • Jinsi mbinu hii inavyotumika.
  • Jinsi mbinu hii inavyotumika.
  • Faida tatu (3) za mbinu hiyo.
  • Dosari tatu (3) za mbinu hiyo.
59. Fafanua matumizi ya stadi ya kuandika katika maisha ya kila siku ya kijana aliyehitimu vema elimu ya msingi.
60. Eleza makusudi ya kufundisha kusoma kimya na kwa sauti katika shule za msingi.

Comments

Popular posts from this blog

NOTES ZA USHAIRI

MBINU ZA KUFUNDISHIA

DHANA YA USHAIRI ILIVYOFAFANULIWA NA WATAALAMU MBALIMBALI