Skip to main content

tofauti kati ya muhtasari wa 2005 na ule wa 2010



Muhtasari, ni ufundisho wa mambo yanayofundishwa katika shule au chuo, vidokezo vya somo. (J.S.Mdee, K. Njogu, Shati A. 2011).
Muhtasari, ni muongozo unaotaja mambo yote yatakayofundishwa, mbinu za ufundishaji, na zana za kufundishia.
Mhtasari wa somo, ni mwongozo unaotaja mambo yatakiwayo kufundishwa kwa kipindi maalumu.
Aidha muhtasari wa somo la Kiswahili huwa na muundo yaani utangulizi, malengo ya elimu Tanzania, malengo ya elimu ya sekondari, ujuzi wa jumla wa somo la Kiswahili katika shule za sekondari, malengo ya jumla ya kufundisha somo la Kiswahili katika shule za sekondari, ujuzi, malengo na majedwali ya ufundishaji kidato cha 1 – 4.
Tofauti, ni ile hali ya kutofanana au kutokuwa sawa. Tofauti inapatikana kwa kuangalia umbo la kitu, hali ya kitu, kazi ya kitu na hata muda. Tofauti zimejitokeza katika upande wa utangulizi, ujuzi, na malengo.
Zifuatazo ni tofauti zilizojitokeza katika muhtasari wa mwaka 2005 na muhtasari wa mwaka 2010, katika kipengele cha utangulizi:-
Utangulizi, katika kipengele cha utangulizi, muhtasari wa mwaka 2005 wametumia neno muhamo wa ruwaza wakibainisha vipengele au mambo yaliozingatiwa katika muhtasari huu. Lakini katika muhtasari wa mwaka 2010 wametumia neno mbinu shirikishi katika kipengele hichohicho kinachopambanua mambo au vipengele vilivyozingatiwa katika muhtasari huo. Maneno yote hayo mawili yaani muhamo ruwaza na mbinu shirikishi yana maana inayofanana ambayo ni kuwashirikisha wanafunzi katika tendo la ufundishaji na ujifunzaji.
Uandishi wa muhtasari, katika muhtasari wa mwaka 2010 umetajwa vizuri katika jalada la nje kuwa ni muhtasari wa mwaka 2010 lakini ndani yake katika ukurasa wa iv kwenye kipengele cha utangulizi kuna kosa la kiuandishi au kiuchapaji ambapo umetajwa kama muhtasari wa mwaka 2005. Hii inaashiria kuwa kulikuwa na uzembe wakati wa uhariri.
Ushauri wa mwalimu, kwenye muhtasari wa mwaka 2005 mwalimu anashauriwa kuwa anaweza kutumia kitabu cha kiada zaidi ya kimoja ili kujiongezea maarifa na kumrahisishia ufundishaji, lakini katika muhtasari wa mwaka 2010 mwalimu ameshauriwa azingatie kuwa “Orodha ya vitabu vya kufundishia Kiswahili vitakuwa vikitolewa na wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi. Muhtasari huu wa mwaka 2010, umemfanya mwalimu kama mtu wa kusubilia tu pasipo kujishughulisha na usomaji wa vitabu tofauti tofauti ili kuongeza maarifa katika somo la Kiswahili.
Muhtasari huu wa mwaka 2005 na muhtasari wa mwaka 2010, umetofautiana katika mambo machache sana tukizingatia vipengele tofauti tofauti vya muhtasari. Lakini pia muhtasari wa mwaka 2010 na muhtasari wa mwaka 2005 umefanana kwa asilimia nyingi ukilinganisha na kutofautiana kwake. Muhtasari huu wa 2005 na 2010 umefanana katika muda wa kufundishia, malengo ya elimu Tanzania, madhumuni ya elimu ya sekondari, ujuzi wa somo la Kiswahili, malengo ya jumla ya kufundisha somo la Kiswahili kwa shule za sekondari, muundo wa muhtasari, ujuzi wa kila kidato, malengo ya kila kidato, mada za kila kidato, idadi ya vipindi na masaa.















                                        MAREJELEO
Ø  J.S.Mdee, K. Njogu, Shati A. (2011). Kamusi ya karne ya 21: Longhorn.
Ø  Muhtasari wa Kiswahili kwa shule za sekondari, kidato cha i-iv (2005).
Ø  Muhtasari wa Kiswahili kwa shule za sekondari, kidato cha i-iv (2010).

Comments

Popular posts from this blog

NOTES ZA USHAIRI

USHAIRI     NI    NINI ? Shaaban Robert katika uandishi wa ushairi ameandika Tenzi na mashairi ya kimapokeo. Tenzi : Ni aina ya mashairi ya kimapokeo wenye sifa zifuatazo: Kimaudhui ; Ni utungo wenye maudhui yanayosimulia kwa urefu tukio fulani maalum. Waweza kuwa wasifu wa mtu au jambo la kihistoria. Mfano; S. Robert ameandika utenzi wa vita vya Uhuru, ameeleza kuhusu historia. Pia katika Mapenzi Bora, ameeleza kuhusu sifa za mapenzi bora. Utenzi ni utungo wa pili kati tungo za ushairi zenye beti nyingi. Utungo wa kwanza unaoongoza kuwa na beti nyingi kuliko zote katika ushairi ni Tendi. Lakini hapa tutaangazia tenzi zaidi. Utenzi hauna mizani nyingi aghalabu mizani nane, hauna mshororo bali una nusu mshororo/kipande mstari. Vilevile katika utenzi kipande mstari hakigawiki. Pia katika kipande mshororo kuna vipande vinne kwa kila ubeti. Mistari mitatu ya kwanza huwa na vina vyenye urari na kipande mstari cha mwisho/cha nne huwa...

Mpangilio wa sura katika utafiti

MADHARA YA MATUMIZI YA KARATASI ZA OMR KATIKA KUJIBIA MITIHANI. Na LEONARD RENATUS, 0759392855 Tasinifu hii ni kwa Ajili ya Kukamilisha Masharti ya  kukamilisha  Stashahada ya elimu ya msingi Chuo cha Ualimu Marangu. SURA YA KWAZA UTANGULIZI Utafiti huu umekusudia kuchunguza madhara na changamoto zitokanazo na karatasi za OMR  katika kujibia mitihani inayotolewa na baraza la matihani Tanzania (NECTA) . Katika sura hii utafiti huu utaangalia vipengele vifuatavyo:- Utangulizi. Usuli wa tatizo. Tamko la utafiti. Lengo kuu la utafiti. Malengo mahsusi yautafiti. Umuhimu wa utafiti. Mawanda ya utafiti. Tafsiri za istlahi zilizotumika 1.2    USULI WA TATIZO OMR ni kifupi cha maneno ya Optical Mark Reader ni mashine ambayo inatumika kusahihishia karatasi za wanafunzi waliofanya mitihani. Kwa hapa Tanzania karatasi hizi hutumika katika kujibia mitihani ya kumaliza elimu ya msingi kwa darasa la saba . Njia hii ya kusahihishia miti...

MBINU ZA KUFUNDISHIA

Mbinu za kufundishia , ni miongozo mbalimbali atumiayo mwalimu wakati wa kufundisha somo aliloliandaa kwa wanafunzi wake. Walimu wanapaswa kuamua kwa kuchagua kwa makini njia na mbinu bora za kufundishia ili wanafunzi wake waweze kujifunza kwa ufanisi. Ziko njia nyingi za kutengeneza mazingira ya mtoto aweze kujifunza na pia ziko mbinu nyingi za kufundishia. Pamoja na wingi huo tunaweza kuzigawa katika makundi makuu mawili kadri ya jinsi zinavyowashirikisha watoto katika tendo la kujifunza, ambazo tunaweza kuziita shirikishi na zisizo shirikishi . Zifuatazo ni baadhi ya mbinu shirikishi na zisizo shirikishi za kufundishia pamoja na faida na hasara zake:- Njia ya majadiliano , njia hii imekuwa ikitumika katika ufundishaji kwa muda mrefu. Katika kujadiliana mwanafunzi mmoja mmoja hupata nafasi ya mawazo aliyonayo kuhusu suala linalojadiliwa na yeye pia huweza kupata mawazo yaw engine. Katika majadiliano mwanafunzi hupata ujuzi mpya nje na ule aliokuwa nao kabla hajashiriki kat...