MADHARA YA MATUMIZI YA KARATASI ZA OMR KATIKA KUJIBIA MITIHANI.
Na
LEONARD RENATUS, 0759392855
Tasinifu hii ni kwa Ajili ya Kukamilisha Masharti ya kukamilisha
Stashahada ya elimu ya msingi Chuo cha Ualimu Marangu.
SURA YA KWAZA
UTANGULIZI
Utafiti huu umekusudia kuchunguza madhara na changamoto zitokanazo na karatasi za OMR katika kujibia mitihani inayotolewa na baraza la matihani Tanzania (NECTA) .
Katika sura hii utafiti huu utaangalia vipengele vifuatavyo:-
Utangulizi.
Usuli wa tatizo.
Tamko la utafiti.
Lengo kuu la utafiti.
Malengo mahsusi yautafiti.
Umuhimu wa utafiti.
Mawanda ya utafiti.
Tafsiri za istlahi zilizotumika
1.2 USULI WA TATIZO
OMR ni kifupi cha maneno ya Optical Mark Reader ni mashine ambayo inatumika kusahihishia karatasi za wanafunzi waliofanya mitihani. Kwa hapa Tanzania karatasi hizi hutumika katika kujibia mitihani ya kumaliza elimu ya msingi kwa darasa la saba .
Njia hii ya kusahihishia mitihani kwa kutumia mashin e ni nzuri kwa upande wa kuokoa gharama tu. Kwa kupititia utafiti huu utaonyesha madhara yatokanayo na matumimzi ya mashine hizi katika kusahihisha karatasi za kujibia kwa wanafunzi wa darasa la saba.
Utafiti huu utaangalia kwa namna ggani mwanafunzi anapimwa stadi ya kuandika na kujieleza kupitia mfumo huu.
Katika matumimzi ya karatasi hizi mwanafunzi hutakiwa kuweka kivulikatika herufi ambayo ndio jibu sahihi.
Utafiti huu utafanyika katika nchi ya Tanzania ,mkoa wa Tabora ,wilaya ya Uyui katika shule za msingi na sekondari za serikali.
Kuna kampuni la Uingereza ambalo ndiyo linatengeneza mashine hizi na kuzileta nchini Tanzania katika kutumika kwa mfumo huu kuna wadau wa elimu ambao wanaukubali mfumo huu wa usahihishaji wa mashine na wengine wanaukataa mafumo huu Kwa upande wa Samatha Jones (2000) kupitia kampuni yake ya mauzo ya mashine hizi anaeleza kuwa Solution Sales Consultant(DRS) ilianza kutumika huko ulaya miaka 12 iliyopita.
1.3 TAMKO LA UTAFITI
Kulingana na utafiti huu utasaidia Baraza la Mtihani Tanzania kubadilisha mfumo huu wa upimaji wa wanafunzi wanaomaliza elimu ya msingi kwani utaonyesha madhara hayo.
Utafiti huu utaishauri sherikali kupitia mfumo huu na kufanya mabadiliko ya upimaji wanafunmzi kwa kusahihisha karatasi hizi za majibu kwa kutumia mashine.
Utafiti huu utasaidia hata nchi nyingine zinazotumia mfumo huu kubaini madhara ya tokanayo nautafiti huu ili kubadilisha mfumo huu au kuuboresha zaidi.
Utafiti huu utasaidia katika kuwapata wanafunzi wenyesifa stahili za kuendelea na elimu ya sekondari kwa wale wenye sifa .
1.4 LENGO LA UTAFITI
Ni kubaini madhara yatikanayo na matumizi ya karatasi za kujibia mitihani OMR katika mtihani wa kumaliza elimu ya msingi.
1.5 MALENGO MAHSUSI YA UTAFITI
Kubainisha madhara yatokanayo na matumizi ya OMR katika kujibia mitihani.
Kubaini changamoto zitokanazo na matumizi ya OMR katika kujibia mtihani.
1.6 MASWALI YA UTAFITI
Kuna madhara gani ya kutumia karatasi za kujibia za OMR katika kujibia mitihani?
Kuna changamoto gani wakati wa kutumiakaratasi za OMR?
Nini .matokeo ya matumizi ya mfumo huu?
1.7 UMUHIMU WA UTAFITI
Utafiti huu utakuwa na umuhimu mkubwa sio tu kwa mkoa wa Tabora tu bali kwa Taifa na dunia kwa ujumla .
Utapanua mawanda ya tafiti zilizofanyia au zitakazofanyika.
Utafiti huuu utaishauti serikali kutumia njia nyingine ya usahihishaji .
Utafimti huu utasaidia kupata wasomi wazuri wenye uwezo wa kujieleza vizuri kwa maandishi.
Utafiti huu utasaidia kuzuia wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika kuchaguliwa kuendelea na elimu ya sekondari.
1.8 MAWANDA YA UTAFITI
Utafiti huu umejikita zaidi kufanyika katika mkoa wa tabora,wilaya ya Uyui katika nchi ya Tanzania kwa shule za msingi na sekondari za serikali.
Utafiti huu unaweza kufanyika katika mkoa wowote hapa Tanzania katika kubaini madhara ya matumizi za kujibia za OMR.
Utafiti huu pia ungeweza kufanyika ulaya ambako ndiko kiwanda cha kutengeneza mashine hizi kinapatikana.
Utafiti huu unaweza kufanyika sehemu yoyote Dunia ambako swala la upimaji wa wanafunzi wanaopata mafunzo Fulani lazima litendeke.
1.9 TAFSIRI ZA ISLAHI ZILIZOTUMIKA
OMR-Optical Mark Reader
NECTA-National Examination Council of Tanzania.
CWT- Chama cha Walimu Tanzania.
DRS- wauzaji wa mashine za OMR Ulaya.
ICT- International Communication Technology .
SURA YA PILI
MAPITIO YA VITABU NA MACHAPISHO
2.1 Utangulizi
Sura hii itajadili marejeo ya vitabu na machapisho yanayohusiana na mada ya utafiti huu. Itaonesha mtazamo wa watalaam mbalimbali ulimwenguni kuhusu matumizi ya karatasi za OMR. Kwa kupitia utafiti huu naangalia maana na tafsiri ya OMR kwa undani. Sehemu ya kwanza ya sura hii ni utangulizi, inafuatiwa na sehemu ya pili, ambayo ni mapitio ya vitabu na machapisho na sehemu ya mwisho ni hitimisho.
Katika sehemu hii inaangalia wataalamu mbalimbali waliozunumzia matumizi haya ya OMR katika kujibia mitihani na kuwapima wanafunzi.
2.2 Mapitio ya Vitabu na Machapisho
Katika swala nzima la kuwapima wanafunzi tunahitaji kuzingatia vigezo kadhaa ambavyo ni umri wa mwanafunzi,darasa,mada na kuangalia malengo yaliyowekwa ili kuwezesha upimaji huo kwenda katika lengo lililokusudiwa. Katika upimaji wa mwanafunzi ni vyema kuhakikisha unagusa Nyanja zote sita za kujifunza kulingana na malengo yaliyo wekwa.
Katika nchi nyingi kwanautaratibu wa kuwapima wanafunzi mfano kwa upande wan chi ya Kenya wanafunzi wa shule za msingi hupiwa kwa mtihani wa taifa na kwa upande wa Tanzania wanafunzi hupimwa kwa mtihani wa taifa kwa kupitia Baraza la Mtihani Tanzania(NACTE). Katika mitihani ya elimu ya msingi Tanzania katika kumpima mwanafunzi tunaweza kumpima hata stadi ya kuandika. Kuptia stadi ya kuandika unaweza kuangalia uwezo wa mwanafunzi kupanga mawazo yake katika mtiririko na muundo wa herufi.
Kuna baadhi ya viongozi wa serikali ambao wanaunga mkono matumizi ya karatasiza OMR katika kuwapima wanafunzi wa shule za msingi Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es salaam Bi. Theresia Mmbado (2014) anasema matumizi ya OMR yameleta mafanikio makubwa sana katika mkoa wake
“ Nikiwa mwenyekiti wa usimamizi wa mitihani wa mkoa wa Dar es salaam kwa mwaka 2013 nakiri kuwa mkoa wetu umepata fomu mafanikio makubwa katika usimamizi wa mitihani na kupunguza udanganyifu kwa sababu ya hizi”
Kupitia kauli ya viongozi inaonyesha kuwa karatasi hizi zinapunguza udanganyifu katika mitihani lakini hakuelezea inapungunguzaje udanganyifu huo.
Katika swala hili kuna wadau mbalimbali wa elimu ambao ni walimu wametoa mchango wao katika kubaini changamoto na faida za karatasi hizi. Afisa Elimu wa mkoa wa Dar es salaam, Bw. Raymond Mapunda(2014) anasema
“Karatasi hizi zimepunguza makosa ya kibinadamu na gharama za usahihishaji na kuongeza kuwa baadhi ya changamoto za baadhi ya karatasi kujikunja, kuchafuka na kutoboka na pia baadhi ya wanafunzi kushindwa kuweka vivuli kwenye vyumba husika vya majibu waliyochagua zinaendelea kufanyiwa kazi katika maeneo husika”.
Hivyo katika kuziunga mkono mdau huyu wa elimu ameangalia zaidi kuwa inapunguza gharama ya kusahihisha mitihani hiyho bila kuangalia lengo mahususi la kumpima mwanafunzi.
Katika kipindi kingine kwa elimu ya Tanzania kumekuwa na siasa katika swala nzima la kuwapima wanafunzi wa shule za msingi katika chombo cha habari ambaco ni gazeti la Mwananchi la tarehe 10 mwezi wa 9 siku ya jumanne mwaka 2013liliandika habari kuwa,
“Necta mbioni kutumia teknolojia ya kusahihisha maswali ya kujieleza”
Kupitia vyombo hivyo vya habari huweza kuonyesha kuwa swala la upimaji wa mwanafunzi limekuwa siasa. Hata katika habari hii kuanzia mwaka 2013 hadi mwaka 2015 ni miaka minne lakini bado watahiniwa wanaplijta tu bila kupimwa stadi ya mwandiko na kujieleza kwa maandishi.
Wadau wengine wa elimu wanatoa maelekezo na kukosoa mfumo huu unaotumika kuwapima wanafunzi chama cha walimu Tanzania kupitia naibu katibu mkuu wa chama hicho mwalimu Ezekiah Oluoch (2012)anasema Kutahini kunakwenda sambamba na kubaini uwezo wa mwanafunzi kujieleza na kuhangaisha akili yake katika utafuta na kukokotoa majibu, lakini mfumo huu ambao Serikali imeuweka hauna tija kabisa na madhara yake ni makubwa.
Katika upimaji wadau wa elimu wameonyesha kuwa katika shule nyingi mfumo huu hautakuwa mzuri katika kuwapima wanafunzi .
Naye katibu mkuu wa baraza la mitihani Tanzania mwaka 2012 alilonyesha kutoa msisitizo wa maelekezo ya utumiaji wa karatasi hizi kutokana na miundombinu yetu ilivyo mibovu ya madawati inahitaji umakini mkubwa, Dr Jocye Ndalichako (2012) anasema ,
“Tumesisitiza umakini zaidi wakati wa mtihani, lakini baraza tumejiandaa kukabiliana na changamoto zitakazojitokeza kwenye mtihani na kuhakikisha kuwa haki itatendeka kwa kila mwanafunzi,”
Pia katika masharti ya kujibia mtihani huu mashine hizi mara nyingi hutambua alama ambazo zimewekewa kivuli tu.
Katika matumizi ya mashine hizi zinauwezo wakutambua majibu ya maswali ya kuchagua jibu sahihi tu hivyo basi katika maswali ya kujieleza hazina uwezo wa kusoma .
Pyayung, M (2016) ni mtafiti kutoka China anasema kwamba mashine hizi zinauwezo wa kusoma karatasi za kujibia zenye aina ya maswali ya kuchagua jibu sahihi kwa umakini na uhakika zaidi na alisema uwezo wa mashine hizi kukosea ni 1 kati makosa 1000 au ni asilimia 0.1% tu.
Katika matumizi haya ya karatasi hizi za OMR zinaweza kusababisha mabadiliko katika upimaji wa mwanafunzi mabadiliko hayo yanaweza kuwa hasi au chanya .
(Kaffash, Kargiban1, & Kargiban, 2010) wanasema kuwa katika matumizi ya ICT yatasaidia ufundishaji na upimaji,anaeleza katika upimaji wa elimu ICT itasaidia katika kuboresha upimaji.
Upimaji mzuri wa mwanafunzi ni ule unaozingatia na kutumia stadi mbalimbali alizozipata mwanafunzi katika maisha ya kikila siku.
Katika nchi ya India Mhadhiri Jain,N.C (2014) wanatumia mfumo katika maelekezo ya kufanya mtihani wa utafiti tarehe 28 desemba 2014 wanatoa maelekezo kuwa katika maelekezo ya matumizi ya karatasi hizi huruhusiwi kukunja au kuweka kivuli zaidi ya marambili katika kila swali maana mashine inayosoma karatasi hizi husoma kivuli.
Hivyo kwa kupitia maelekezo haya mwanafunzi atakuwa anaelekeza akili nyingi kuwa makini na karatasi badala ya kufikiria kwa kina majibu ya swali alilopewa.
NECTA(2009) moja ya changamoto ambazo baraza hili zililieleza ni namba za OMR kuingiliana na namba za orodha za watahiniwa wa mtihani wa kumaliza elimu ya msingi.
Ricketts and Wilks (2002)wanasema wanafunzi waliofanya mitihani ya OMR ambayo ilikuwa yakuchagua jibu sahihi hawakufanya vizuri.
Katika utafiti wa wataalamu hawa wamegundua mashine zinaweza kuwakosesha wanafunzi alama.
Brown, S., Race, P., and Bull, J (Eds) (1999) wanasema kuwa mashine za OMR zisipo endeshwa na watu wenye ujuzi zinaweza kusahihisha vibaya na wanavunzi wakakosa haki katika taaluma .
SURA YA TATU
MBINU ZA UTAFITI
3.1 Utangulizi
Sura hii ya tatu inajadili mbinu mbalimbali zilizotumika katika utafiti huu. Mbinu hizo za utafiti ni kama kubainisha na kuelezea eneo la utafiti, sampuli ya utafiti, taratibu za usampulishaji, mbinu za ukusanyaji wa data na taratibu zilizotumika katika kuchambua data. Kadhalika, mkabala uliotumika pamoja na kiunzi cha nadharia kilichotumika katika utafiti huu vimeelezwa. Pia usanifu wa utafiti huu umeelezwa katika sura hii.
3.2 Muundo wa Utafiti
Utafiti huu, kwa sehemu kubwa, ni wa uwandani na sehemu ndogo ilifanyika maktabani.. Hivyo muundo wa utafiti ni mpangilio wa taratibu zinazotumika kukusanya na kuchambua data kwa namna inayounganisha data zinazopatikana na malengo ya utafiti. Mbinu za ukusanyaji wa data zilizotumika ni mahojiano, usaili na dodoso. Mbinu hizi inawezesha upatikanaji wa data za kutosha kwa urahisi na kwa haraka. Mbinu ya uchambuzi matini pia ilitumika kupata data za msingi ambazo zilipatikana maktabani kwa kusoma matini mbalimbali zinazohusiana na mada ya utafiti huu. Data zilizopatikana zilichambuliwa kulingana na malengo ya utafiti huu.
3.3 Eneo la Utafiti
Utafiti huu ulifanyika mkoa wa Tabora. Kutokana na malengo ya utafiti, data zilizotakiwa zilipatikana kwa kuwahoji baadhi ya walimu wa shule za Msingi na sekondari katika wilaya ya Uyui za serikali tu. Ambapo hapa ni sehemu ya wanafunzi na wadau wa elimu kwa Tanzania na mitihani hii hufanyika katika nchi nzima na wilaya zote za Tanzania . Katika eneo la Tabora wilaya Uyui ni moja ya wilaya ya Tabora ambayo iko katika maeneo ya vijijini na mfumo huu unaonyesha kuwa ni kitu kigeni sana katika nchi yetu ukilinganisha na mazingira ya kitanzania. Eneo jingine la utafiti huu ni mkoa wa Dar es Salaam katika ofisi ya Katibu Mkuu Baraza la Mitihani Tanzania. Wahojiwa 5 toka Baraza la Mitihani Tanzanoa ili kupata data zaidi. Pia data zilipatikana maktabani na shuleni, Ofisi za ukaguzi wa elimu za wilaya na wizara ya elimu ili kupata taarifa za kuuhusu sababu za kuweka na kupitisha mpango huu na taarifa zaidi.
3.4 Sampuli ya Utafiti na Usampulishaji
Babbie (1992) anasema sampuli ni sehemu ya idadi watu ambayo mtafiti anavutiwa nayo katika kupata taarifa na kutoa hitimisho la utafiti wake. Pia Kombo na Tromp (2006) wanasema jambo la msingi ni kuanza na idadi kubwa na kadri utafiti unavyoendelea, mtafiti atabaki na eneo husika la utafiti ambamo data zitakusanywa. Katika utafiti huu nitatumia sampluli lengwa na sampluli ya bahati nasibu. Sampuli lengwa itatumika kwa sababu kuna ambao wanafusika moja kwa moja na kuanzisha na kusimamia mfumo huu na bahati nasibu kwa sababu kuna kundikubwa ambalo lilipitia mfumo huu na litakalopitia mfumo huu Katika kufanya utafiti huu nitahusisha shule za msingi na sekondari za serikali tu. Kwa hiyo, jumla ya shule ambazo nitazitazitafiti ni shule 20 za msingi kwa kila kata shule moja na shule ya sekondari 10 za serikali . Wahojiwa waligawanywa kama ifuatavyo:
Kwa kila shule ya msingi wahojiwa walimu 5 wakike 2 wakiume2 mkuu wa shule 1
Kwa kila shule ya sekondari walimu 4 wakike 2 na wakuime 1 na mkuu wa shule 1.
Shule ya msingi wahojiwa wanafunzi 20 wakike 10 na wakiume 10 wa darasa la saba.
Shule ya sekondari wahijiwa wanafunzi 20 wakike 10 wakiume 10 wakidato cha kwanza tu.
Ofisi ya mkaguzi wa shule wilaya ya uyui wahojiwa Mkaguzi mkuu wa wilaya na Mkaguzi mmoja.
Kutoka mkoa wa Baraza la mitihani Tanzania sampuli ilikuwa na wahojiwa wanne (4). Wahojiwa watatu (3) ni wanaume na mmoja (1) mwanamke,Ambao wamefanya kazi baraza la mitihani kwa muda usiopungua miaka 10. Katika Wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi wahojiwa ni Katibu Mkuu wa wizara na watumishi 3 wa wizara ya elimu wakike 1 na wakiume 2 ambao wamefanya kazi hapo kwa muda usiopungua miaka 4.Hivyo jumla ya wahojiwa wote ni hamsini na nane (58). Idadi hii ilikidhi malengo na mahitaji ya utafiti.
Wahojiwa hawa ambao ni hamsini na nane (58) inatosha katika kuwakilisha wanafunzi na walimu washule za msingi na sekondari nchini. Kama utafiti huu ukifanyika nchi nzima ya Tanzania basi itachukua miaka mingi na pia hutumia gharama kubwa maana itabidi kuhiji walimu wote na shule zote Tanzania kza serikali.
Gomm, R.(2000) anasema kwa tafuta sampuli ndogo ambayo inaweza kupata taarifa zilizokusudiwa kuliko kutafuta sampuli kubwa ambayo haina taarifa sahihi.
3.5 Vifaa vya Kukusanyia Data
Vifaa vya utafiti vitaandaliwa kulingana na mada na malengo ya utafiti. Vifaa hivi vilimwezesha mtafiti kukusanya data husika na kupata taarifa sahihi za utafiti . Katika utafiti huu, data na taarifa zilikusanywa kwa kutumia vifaa mbalimbali, vifaa hivyo ni pamoja na dodoso, tepurikoda, kamera, kompyuta, shajara na kalamu.
Vidadisi na majedwali katika zana hii nitakuwa na majedwali ya matokeo ya mitihani ya taifa ya kumaliza elimu ya msingi kila mwaka kwa miaka mitatu mfululizo.
Hojaji ni maswali yaliyoandaliwa na mtafiti kwa lengo la kumhoji mtafitiwa, na maswali haya yanafungamana na malengo ya utafiti husika. Mtafiti alitumia maswali hayo kama mwongozo wake katika kupata data husika kutoka kwa mtafitiwa. Hivyo, hojaji ilimwezesha mtafiti kupata data za msingi . Hojaji zitakazotumika katika utafiti huu zitakuwa zimeambatanishwa katika utafiti.
Dodoso dodoso ni maswali ambayo yameandaliwa na mtafiti akitaka watafitiwa kujaza kwa kutumia maandishi yao wenyewe mara nyingi huwa mtafitiwa haandiki jina . utafiti utatumia zana hii kwa sababu wahojiwa hawa wote wanajua kusoma na kuandika vizuri.
Kalamu: Vifaa hivi vitasaidia mtafiti katika kunukuu na kuhifadhi baadhi ya data za msingi kama vile tarehe, majina ya wahojiwa na majina ya shule ambazo zitahojiwa .
Tepurikoda ni kifaa kinachotumika katika kunasa na kurekodi sauti wakati wowote katika maeneo yote. Katika utafiti huu, tepurekoda nitaitumia tu katika kuchambua data tu na siyo kwa ajili ya kiambatanisho katika utafiti huu ili kupata taarifa zilizokusudiwa .
Kamera ni kifaa kilichotumika katika kupata taarifa mbalimbali za kuona ambazo haziko katika maandishi. Kwa mfano picha za wahojiwa na maeneo mbalimbali ambayo yanahusiana na mada husika. Kwa mfano miundombinu ya madawati na na hali ya kuandikia katika meza na madawati hayo kama yanaendana na masharti ya karatasi OMR.
Kompyuta ilitumika katika kutafutia matini kutoka katika tovuti na wavuti na pia kuhifadhi taarifa mbalimbali ambazo zinahusu utafiti . Data zilizohifadhiwa zilichambuliwa na kutolewa mahitimisho kisha kuandaa ripoti ya utafiti. Pia kompyuta ilitumika kama sehemu ya maktaba tembezi.
Karatasi za OMR miamoja (100) hizi ni karatasi ambazo zitatumika katika kuangalia zinavyo jazwa kwa wanafunzi ambao watakuwa bado hawazifahamu kwa wale wa shule ya msingi darasa la saba. Pia zitatumika katika mbiunu ya uchunguzi ili kubaini matokeo.
Penseli za HB Hizi ni penseli maalumu katika kujaza karatasi za OMR na zitatumika katika kujaza karatasi hizi. Remark Products Group(2000) ni kampuni ambalo linahusika na uandaaji wa mashine hizi na wanasema karatasi hizi zijazwe kwa penseli.
Pia katika muongozo wa chuo na (PROSPECTUS 2014 –2015) chuo hiki cha kilimo India wametoa maelekezo na masharti ya kutumia fomu hizi ni mengi sana ukiangalia mwanafunzi wa kitanzania kuyafuata kikamiifu ni changamoto
Rejea
Rickets,C. and Wilks, S.J (2001).Improving Students Performance through computer based assessment .Insights from recent Research.
Brown, S., Race, P., and Bull, J (Eds) (1999) Computer assisted assessment in high Education,London
Necta (2009) Evaluation of the conduct of primary school leaving examination (PSLE) in Tanzania Mainland
Prof. Jain, N.C, (2014) Directions for the candidates for b.ed. (special education) Entrance examination, India.
Kaffash,R.H.,Kargiban1,A.Z.,Kargiban,A.S.(2010).Undersecretary information and communication technology,Research and Educational Planning Organization, Ministry of Education, Iran.International Journal of Instruction, Vol.3, No.2. pp.65
Pyayung, M (2016) Scanner-Based Optical Mark Recognition ,Chatree Saengtongsrikamon*, Phayung Meesad**, Sunantha Sodsee* China.
Babbie, E. 1992. The practice of social research.(6thEd.). Belmont, CA: Wadsworth Publishing Company.
Kombo, D and Tromp, A. (2006): Proposal and Thesis Writing: an introduction Nairobi: Paulines publications Africa.
Gomm, R. (Eds.) (2000)Case study method:key issues, key texts. London: Sage Publications.
Remark Products Group(2000) Remark Office OMR Version 8 User‟s Guide , Remark Products Group 301 Lindenwood
Gazeti la Mwananchi “Necta mbioni kutumia teknolojia ya kusahihisha maswali ya kujieleza” la tarehe 10 mwezi 9 mwaka 2013 siku ya Jumanne Toleo la 5874 ISSN 0856-6978
http://www.tanzaniatoday.co.tz/news/usahihishaji-wa-mitihani-shule-za-msingi-kwa-kutumia-kompyuta-wapata-mafanikio-jijini-dar

Asante kwa kielelezo hiki muhimu. hongera sana
ReplyDelete