Skip to main content

FORM 3: UHAKIKI WA KAZI ZA FASIHI 123

KISWAHILI Form 3 Topic 4
UHAKIKI WA KAZI ZA FASIHI ANDISHI
Fasihi andishi ni tawi la fasihi linalotumia sanaa ya maneno kufikisha ujumbe kwa hadhira kwa njia ya maandishi. Zipo aina nyingi za fasihi andishi, miongoni mwa hizo ni pamoja na hadithi fupi, riwaya, tamthiliya na mashairi.

Maana ya Uhakiki
Dhana ya Uhakiki
Fafanua dhana ya uhakiki
Uhakiki ni kitendo cha kutathimini, kueleza, kuainisha na kutoa maoni juu ya kazi fulani ya fasihi kwa kuongozwa na kaida maalum. Hii ina maana kwamba uhakiki wa kazi za fasihi hautoki katika ombwe, kuna kanuni na taratibu mbalimbali zinazoongoza kufanya uhakiki, na hii ndio sababu kuna nadharia kadha wa kadha za uhakiki wa kazi za kifaishi. AU kwa lugha rahisi tunaweza kusema, uhakiki ni uchambuzi wa kina wa kazi za fasihi kama vile riwaya, tamthiliya na mashairi kwa lengo la kufafanua vipengele vya fani na maudhui.
Misingi ya Uhakiki
Elezea misingi ya uhakiki
Kwa ujumla mhakiki wa kazi za fasihi anapofanya uhakiki wa kazi za kifasihi, huwa analenga vipengele viwili. Pengine analenga kuhakikifaniya kazi husika aumaudhuiya kazi hiyo na wakati mwingine vyote viwili. Kwa hiyo kupitia vipengele hivi ndipo atachambua vitu vingi kama vile ujumbe, falsafa, matumizi ya lugha, dhamira, mandhari na kadhalika.
Kuhakiki Fani
Katika utunzi wa kazi za kifasihi, Fani hutumika kama nyezo ya kuwasilisha mawazo ya mwandishi kwa njia ya kisanaa zaidi. Fani ni mbinu anayoitumia mwandshi ili kufikisha ujumbe kwa watu aliowakusudia.
Vipengele vya fani ni pamoja nawahusika, mandhari, lugha, muundonamtindo.
Mtindo
Mtindo ni mbinu ya kipekee kifani na kimaudhui, zinazotofautisha msanii mmoja na mwingine. Kwa mfano, namna msanii anavyotumia lugha, anavyoteua msamiati, namna anavyosimulia hadithi yake (anaweza kutumia nafsi ya kwanza, ya pili au ya tatu). Kwa mfano katika riwaya ya “Barua Ndefu kama hii” iliyoandikwa na Mariama Ba ametumia mtindo wa barua ya kirafiki kuanzia mwanzo hadi mwisho, hii pia inaonesha mtindo wake wa kipekee.
Muundo
Muundo ni mpangilio wa kiufundi anaoutumia mwandishi katika kupangilia kazi yake. mpangilio na mtiririko wa kazi ya fasihi, kwa upande wa visa na mtukio.
Kuna aina mbili za kupangilia matukio
Msago; hii ni namana ya moja kwa moja ya kusimulia matukio, yaani kuanzia tukio la kwanza hadi la mwisho kwa namna yalivyotukia. Huu ni muundo wa moja kwa moja.
Urejeshi; huu ni usimuliaji wa kurukaruka hatua, yaani msimuliaji anaweza kuanzia katikati, akaja mwisho na kumalizia na mwanzo
Wahusika
Wahusika; ni watu au viumbe ambavyo mwandishi wa fasihi huwatumia ili kufanikisha ujumbe kwa jamii husika. Katika kazi ya fasihi mwandishi huwagawa wahusika katika makundi mawili yaani wahusika wakuu na wahusika wadogo.
Wahusika wakuu ni wale ambao wanajitokeza kuanzia mwanzo mpaka mwisho wa kazi ya fasihi. Wahusika wadogo ni wale wote ambao wanajitokeza sehemu mbalimbali katika kazi ya fasihi kwa mfano, mwanzoni mwa kitabu hadi mwishoni mwa kitabu.

Wahusika hawa wawe ni wakuu au wadogo wanaweza kugawanyika katika makundi yafuatayo:

Mhusika mviringo ni mhusika ambaye anabadilika kitabia na kimawazo kulingana na hali halisi ya maisha. Kwa mfano wanaweza kuanza kama watu wema lakini hali ya maisha ikawabadilisha na kuwa watu wabaya au wanaweza kuanza kama watu wabaya na hali ya maisha ikawabadilisha na kuwa watu wema.
Mhusika bapa ni mhusika ambaye habadiliki kulingana na hali halisi ya maisha. Mfano; kama ni mwema basi atakuwa mwema kuanzia mwanzo wa hadithi hadi mwisho na kama ni mbaya basi atakuwa mbaya kuanzia mwanzo wa hadithi hadi mwisho.
Mhusika shinda yuko katikikati ya mhusika papa na mviringo. Huongozwa na matendo ya hao wahusika wawili. Hajitokezi na msimamo wake imara.
Mandhari
Mandhari; hii ni sehemu ambayo matukio ya hadithi au masimulizi hutokea. Mandhari huweza kuwa halisi kama vile baharini, njiani, msituni, kijijini, mijini au ya kufikirika kama vile kuzimu, mbinguni, peponi n.k.
Lugha
Lugha ndio nyenzo kubwa ya msanii katika kazi za fasihi, miongoni mwa vipengele vya lugha ni tamathali za semi pamoja na semi.
Fani za Lugha
Tanakali za Sauti:Ni mbinu ya kutumia maneno yanayoiga sauti au hali fulani au namna kitendo kilivyofanyika.

Tashbiha: Hii ni mbinu ya lugha inayolinganisha vitu au hali mbili tofauti kwa kutumia maneno ya kulinganisha; ‘kama’, ‘mithili ya’, ‘sawa na’, ‘ja’. mfano, Mwembamba kama sindano.

Tashihisi: Hii ni mbinu ya kupatia kitu kisicho hai sifa za kiumbe mwenye uhai (sifa za kibinadamu). Mfano, "Sungura aliposhindwa, akasema sizitaki hizi mbichi".

Takriri: Ni mbinu ya kurudiarudia neno moja au kifungu cha maneno ili kusisitiza ujumbe fulani. Mfano, alikimbia, alikimbia, alikimbia hadi akashika nafasi ya kwanza.

Ukinzani: Ukinzani ni mbinu ya kusisitiza ujumbe kwa kuambatanisha maneno ya kinyume au yanayokinzana.

Sitiari: Ni mbinu ya kulinganisha vitu viwili moja kwa moja kwa kutumia kiungo ‘ni’ ama ‘kuwa’. Mfano; Maisha ni mlima, juma ni mwamba.

Taswira: Ni matumizi ya lugha/maneno yanayojenga picha ya hali au jambo fulani kwa msomaji.

Taashira: Ni matumizi ya lugha ya ishara kuwakilisha ujumbe fulani. Jina au kitu fulani kinatumika kumaanisha kitu kingine chenye uhusiano na kile kilichotumiwa.

Jazanda: Ni kulinganisha vitu viwili moja kwa moja bila kutumia viunganishi.

Majazi: Majazi ni pale tabia za wahusika zinapoambatana na majina yao halisi.

Lakabu: Ni mbinu ya mhusika kupewa/kubandikwa jina na wahusika wengine ama yeye mwenyewe kujibandika jina linalooana na tabia/sifa zake.

Chuku: Ni kutumia maneno yaliyotiliwa chumvi ili kusisitiza ujumbe fulani au kusifia kitu, kutilia Chumvi.

Semi
Ni fungu la maneno linapotumika kutoa maana nyingine, badala ya ile ya maneno yaliyotumika. Semi hutumika kuficha ukali wa maneno au kupamba lugha. Kuna aina mbili za semi:

Nahau – ni usemi unaotumia maneno ya kawaida kwa lengo la kufikisha maana iliyotofauti na maana ya kawaida ya maneno hayo. Nahau huwa na vitenzi.

Misemo – ni semi fupifupi ambazo hutumiwa mara kwa mara kwa lengo la kuleta maana maalumu. Misemo haina vitenzi.
Maswali ya Balagha: Tashititi au maswali ya balagha ni maswali yanayoulizwa na msimulizi au mhusika ambayo hayahitaji jibu.

Uzungumzi Nafsiya: Mhusika hujizungumzia, ama kwa kuongea au kuwaza, bila kukusudia kusikika na yeyote.

Ritifaa: Mbinu ya kuzungumza na mtu aliyekufa (au asiyekuwepo) kana kwamba yuko pamoja nawe.

Kuchanganya Ndimi: Kuweka maneno yasiyo ya Kiswahili katika sentensi ya Kiswahili. Mfano, "alisimama kwanza kwa muda, before he went aliniambia nisimwambie mtu yeyote yule, you know!"

Kuhamisha Ndimi: Ni kuingiza sentensi ya lugha nyingine katika kifungu cha lugha ya Kiswahili. Kinyume na Kuchanganya ndimi (ambapo mwandishi huchanganya maneno katika sentensi moja, katika kuhamisha ndimi, sentensi kamilifu ya lugha nyingine hutumika miongoni mwa sentensi za Kiswahili sanifu. Mfano: Kazi hii ni ngumu sana, sitaweza kuifanya. People are trying to convince me to stay here but I think I can't, I must go!
Mathali: Methali ni misemo ya hekima yenye maana iliyofumbwa. Mhusika, mwandishi wa fasihi anaweza kutumia methali kupitisha ujumbe.

Mbinu nyingine za Kisanaa
Kinaya: Kinaya ni mambo katika sanaa kuwa kinyume na matarajio ya hadhira.
Kejeli; Kejeli ni mbinu ya sanaa inayotumia maneno kudharau au kukemea kitendo au mtu fulani.
Taharuki; Taharuki ni mbinu ya kusimulia au kuandika riwaya/hadithi kwa kufanya hadhira na/au wahusika wajawe na hamu ya kutaka kujua kitakachotokea baadaye; hamu ya kutaka kuendelea kusoma/kusikiliza. Baadhi ya hadithi huishia kwa taharuki na kuilazimisha hadhira yake ijikamilishie au ibaki ikijiuliza maswali.
Sadfa; Sadfa ni kugongana kwa vitendo viwili vinavyohusiana kana kwamba vilikuwa vimepangwa, japo havikuwa vimepangiwa.
Kisengere Nyuma; Mwandishi ‘hurudi nyuma’ na kuanza kusimulia kisa kilichokuwa kimetendeka kabla ya alichokuwa akisimulia. Aidha, mwandishi hubadilisha wakati wa masimulizi na kuwa wakati wa kisa hicho. Hutumika sana kuonyesha mhusika anapokumbuka kitu, au kutupatia msingi wa jinsi mambo yalivyoanza.
Kisengere Mbele; Mwandishi anapobadilisha wakati na kusimulia mambo yatakavyokuwa siku za usoni; au kutumia lugha isiyo moja kwa moja kutabiri yatakayojiri. Utabiri.
Kuhakiki Maudhui
Maudhui; Maudhui katika kazi ya fasihi ni jumla ya mawazo yote yanayozungumzwa pamoja na mtazamo wa mwandishi juu ya mawazo hayo. Maudhui hujumuisha mawazo pamoja na mafunzo mbalimbali yaliyomsukuma msanii hadi akatunga na kusanii kazi fulani ya kifasihi. Vipengele vya maudhui ni pamoja na dhamira, migogoro, falsafa ujumbe na msimamo.
Dhamira; hili ni wazo kuu au mawazo mbalimbali yanayojitokeza katika kazi ya fasihi. Dhamira ni sehemu tu ya maudhui na aghalabu dhamira kuu ndio hujenga kiini cha kazi ya fasihi. Dhamira zimegawanyika katika makundi mawili, kuna dhamira kuu na dhamira ndogondogo.
Migogoro; hii ni mivutano na misuguano mbalimbali katika kazi za fasihi. Migogoro inaweza kuwa kati ya wahusika, familia zao, matabaka yao, au hata katika nyadhifa mbalimbali. Vilevile migogoro yaweza kuwa ya kiuchumi, kijamii, mogogoro ya nafsi, na migogoro ya kisiasa ambayo hujitokeza katika mitazamo tofauti kulingana na mtiririko wa visa na matukio yanavyopangwa na mwandishi.
Ujumbe; mwandishi anapoandika kazi yake huwa na ujumbe ambao hutaka uifikie jamii aliyoikusudia. Ujumbe katika kazi fasihi ni mafunzo mbalimbali ambayo hupatikana baada ya kusoma kazi ya fasihi. Katika kazi ya fasihi dhamira kuu hubeba ujumbe wa msingi na dhamira ndogondogo hubeba ujumbe ambao husaidia kuujenga au kuupa uzito zaidi ujumbe wa msingi.
Msimamo; katika kazi ya fasihi, mawazo, mafunzo na falsafa ya msanii hubainisha msimamo wake kuhusu masuala mbalimbali ya kijamii. Msimamo ni ile hali ya mwandishi kuamua kufuata na kushikilia jambo fulani. Jambo hili huweza kukataliwa na wengi lakini akalishikilia tu. Msimamo ndio huweza kuwatofautisha wasanii wawili au zaidi wanaoandika kuhusu mazingira yanayofanana. Kwa mfano, katika tamthilia ya “Pesa zako zinanuka” mwandishi anamsimamo wa kimapinduzi kwani amejadili matatizo yanayochangia kukwama kwa ujenzi wa jamii mpya.
Falsafa ni mawazo ya busara yenye kutawaliwa na misingi mahususi juu ya asili na maana ya ulimwengu na maisha ya mwanadamu. Ni msimamo wa msanii katika maisha juu ya utatuzi wa matatizo katika jamii. Falsafa ya mwandishi inaweza kujulikana kwa kusoma kazi zake zaidi ya moja.
Mtazamo ni hisia au uelewa wa mwandishi juu ya jambo fulani. Kwa mfano anaweza kutazama jambo fulani kwa mtazamo wa kidini, au anaweza kutazama jambo fulani kwa mtazamo wa kisiasa au kisayansi.
Mafunzo; ni mawazo ya kuelimisha yanayopatikana katika dhamira mbalimbali za kazi ya fasihi.
Kufaulu na Kutofaulu kwa mwandishi
Kufaulu au kutofaulu kwa mwandishi kunategemea jinsi alivyoweka uwiano mzuri kati ya fani na maudhui kwa namna ambavyo inaleta uhalisia. Mfano, endapo msanii atakuwa na mhusika Mkongo lakini akawa anazungumza kiswahili kilichojaa misemo na nahau alafu kimenyooka kama mtu wa pwani itakuwa vigumu kusema amefaulu kwani hakuna uwiano mzuri kati ya mhusika mwenyewe na lugha anayoitumia. Kiswahili cha Kongo ni tofauti kabisa na kiswahili kinachozungumzwa na watu wa pwani (Tanzania).


Uhakiki wa Fani katika Kazi za Fasihi Andishi
Uhakiki wa Fani katika riwaya ya Takadini
Hakiki fani katika riwaya ya Takadini
MWANDISHI: BEN J. HANSON
WACHAPISHAJI: MATHEWS BOOKSTORE AND STATIONARIES
MWAKA: 2004
JINA LA KITABU
Jina la kitabu TAKADINI lina maana ya “Sisi tumefanya nini”. Hili ni jina ambalo Sekai alimpa mwanae mara baada ya kumzaa. Jina hili lilitokana na majonzi aliyokuwa nayo juu ya kutaka kuuawa kwa mwanae na yeye ilihali hawakuwa na hatia, ila tu kwa sababu ya mila za jamii yake zilivyotaka. Jina hili la kitabu ni sadifu kwani linasawiri vyema maudhui yaliyomo katika kitabu hiki. “Sisi tumefanya nini?’ ni swali ambalo linatokana na ukosefu wa haki ya kuishi, kubaguliwa kutopendwa, na hata kutengwa kwa watu wenye matatizo katika jamii. Swali hili linawalelekea wanajamii ambao bado wanashikilia mila potofu zinazowakandamiza na kuwanyanyasa watu wenye matatizo mfano, ulemavu wa ngozi, wagonjwa nk. Jina hili pia ni sadifu kwa maisha ya jamii yetu ya watanzania kwani watu bado wanashikilia mila potofu ambazo si nzuri. Mwandishi ametumia jina hili makusudi ili kutaka kuionesha jamii hali halisi ya vilio vya albino, wasichana wadogo wanaolazimishwa kuolewa nk. Kuwa huu sasa ni muda mwafaka wa jamii kuyaacha na kutupilia mbali mambo hayo.
MUUNDO
Muundo alioutumia mwandishi wa riwaya hii ni muundo wa msago au kwa jina lingine muundo wa moja kwa moja. Ameyapanga matukio katika mtiririko sahili kwani ameanza kutuonesha toka mwanzo mpaka mwisho wa maisha ya kijana Takadini “Msope”.Toka kutungwa kwa mimba yake, kuzaliwa kwake na kuishi kwake, matatizo na changamoto zinazomkumba na jinsi anavyokabiliana nazo na hatma ya maisha yake.
Mgawanyo wa visa na mtukio umepangwa katika sura ambapo visa vimejengwa kwa ufundi na kuvifanya vijengane na kukamilishana kuelekea kilele cha masimulizi. Matukio haya yamewekwa katika sura kumi na tatu.
Sura ya Kwanza:Sura hii inaanza kutuelezea kuhusu mwanamke Sekai anavotunga mimba, pia tunaelezwa kuhusu mtazamo mbaya wa wake wenzie juu ya mimba hiyo baada ya Sekai kukaa kwa muda mrefu bila ya kujaliwa mtoto.
Sura ya Pili:Hapa tunasimuliwa jinsi Sekai anavyofanikiwa kujifungua salama. Lakini kwa bahati mbaya kwa kawaida ya jamii yao anajifungua mtoto Zeruzeru ambaye kwa mila zao mtoto huyo ni laana. Hivyo alipaswa kutupwa mara moja ama kuuawa. Hakuna ambaye alikuwa tayari kumpokea mtoto yule kwani si baba yake wala jamii yake ila mama yake pekee.
Sura ya Tatu:Jamii bado haipo tayari kumpokea mtoto Sope, wanawake wenza wa Sekai wanasubiri kwa hamu kuona tukio la kutupwa kwa Takadini litakavokuwa, kwani ndio jinsi mila na taratibu za mababu zilivyotaka. Kutokana na hali hii ndipo Sekai anapata wazo la kutoroka. Anaamua kuondoka kwenda mbali ili kukinusuru kichanga kisicho na hatia kwani alisubiri kwa hamu na uchu wa muda mrefu kupata mtoto.
Sura ya Nne:Sekai anafanikiwa kutoroka na mwanae Takadini ili kumuepusha na kifo, jamii na Mtemi wanapata habari ya kutoroka kwake. Upelelezi unafanyika lakini juhudi hazikuzaa matunda kumpata Sekai na mwanae mchanga waliotakiwa kuuawa. Sekai anasafiri mbali na kufikia kijiji kingine na kupokelewa na mzee Chivero.
Sura ya Tano:Sekai anapokelewa katika kijiji cha mzee Chivero, jamii na wazee wanashitushwa sana na ujio huo lakini wanalazimika kumpokea tu baada ya malumbano ya muda mrefu. Kwani mila ziliwataka kutowatelekeza wageni katika kijiji chao, na hiyo ndiyo inakuwa mwanzo wa matumaini ya Sekai kuhusu kuishi kwa mwanae ambaye alionekana kuwa ni laana ya mababu na hakupaswa kuishi.
Sura ya sita:Baada ya Sekai kupokelewa katika kijiji cha mtemi Masasa, habari za ujio wake zinaenea kwa wanakijiji wote na wanaonekana kushtushwa sana, si hivo tu bali pia wanajiapiza katu kutomsogelea Sope kwani waliamini amelaaniwa. Lakini kwa juhudi za mzee Chivero baba mpya mlezi wa Takadini Sekai anapata rafiki. Tendai mke wa mtemi Masasa. Anajengewa kibanda cha kuishi yeye na mwanae na maisha yanaanza.
Sura ya saba:Sekai anaanza kujishughulisha na shughuli za kawaida kama mama na mwanamke, analima bustani na kufanya kazi ndogo za nyumbani. Siku moja katika safari ya kurudi nyumbani kwa bahati mbaya wanavamiwa na nyuki na kujeruhiwa vibaya yeye na mwanae, anaamua kumtupia mwanae kichakani ili kumuokoa na yeye kujitumbukiza mtoni. Wote wawili wanafanikiwa kutibiwa na kupona majeraha.
Sura ya nane:Taratibu Takadini anaanza kukua lakini anagundulika kuwa hawezi kutembea vyema kwa mguu mmoja, hii ilitokana na kuvunjika Mguu baada ya kurushwa kichakani na mamaye kama juhudi za kumwokoa. Hali hii inamhuzunisha zaidi Sekai na Chivero kwani walimpenda sana. Hapa ndipo mapenzi ya Chivero yalianza kudhihirika rasmi kwa Takadini kwani alijenga urafiki naye na kumpenda kama mwanae. Alimfundisha utabibu wa dawa za kienyeji na mambo mengine mengi. Pia tunaona watoto jinsi walivyombagua Takadini kutokana na hali yake, kwani waliambiwa na wazazi wao wasicheze naye amelaaniwa hivo hawakuthubutu.
Sura ya tisa:Katika sura hii, Mzee Masasi anafariki dunia na kumuacha mzee Chivero katika majonzi makuu. Hali ya mzee Chivero nayo inaanza kuzorota kwa uzee. Anampa Takadini usia mbalimbali na kumfunza. Pia tunaelezwa juu ya fikra mpya za Takadini za kupiga “mbira” kifaa cha muziki cha kijadi, hii baada ya kuvutiwa na sanaa hiyo aliposhiriki sherehe za mavuno za mwaka. Jamii bado ilimtenga Takadini na kumbagua, walimwona si binadamu bali mzuka tu! Na kwa bahati mbaya mzee Chivero naye aliaga dunia na kuacha simanzi kuu kwa Sekai na Takadini mbao alikuwa ni tegemeo na faraja kwao.
Sura ya kumi:Baada ya kifo cha mzee Chivero, Takadini anapata mwalimu maarufu mpiga mbira mzee Kutukwa, anamfundisha kupiga mbira, Takadini anaonesha juhudi kuu na kufanikiwa. Pia anmsaidia kifaa cha kumsaidia kutembea kutokana na mguu wake mbovu, hii inakuwa ni faraja kubwa kwa Takadini na mamaye.
Sura ya kumi na moja:Hapa tunaelezwa juu ya kijana Nhamo adui mkuu wa Takadini kwani hakumpenda na alimdhihaki na kumdhalilisha mara kwa mara. Kijana huyu anaonekana kuwa ni shujaa katika jamii yake kwa kitendo cha kumuua simba mla mifugo. Hiyo inamletea sifa kubwa na majivuno mengi hivo wasichana wengi kumtamani awaoe, hali ni tofauti kwa Shingai ambaye anaonesha hisia za mapenzi kwa Takadini pamoja na hali yake ya “Usope”. Chemchemi za mapenzi ya Takadini kwa Sekai zinaanza kumea jambo ambalo linamkera sana Nhamo na kuzidisha chuki kwa Takadini kwani pia alitamani kuwa na Shengai binti mrembo. Jamii inafanya kikao kujadili suala la Shengai kumpenda Takadini na wanalipinga vikali suala hilo.
Sura ya kumi na mbili:Nhamo anakata shauri na kwenda kumposa Shengai, wazazi wa pande zote mbili wanaliunga suala hilo mkono asilimia zote. Kwani hilo lingewanusuru aibu ya mwanao kuolewa na Sope, kwani walijua fika Shingai alimpenda Takadini na hakumtaka Nhoma. Nhoma anamuonya vikali Takadini kuwa asiendelee na lolote kwa Shengai. Pia hapa zinafanyika sherehe ya kijadi ya kumkaribisha hayati mzee Chivero tena nyumbani.
Sura ya kumi na Tatu:Wakati wa sherehe ya mavuno, binti Shengai anashindwa kuvumilia na kuamua kumfuata Takadini kibandani kwake. Anaamua kuvunja mila za kwao kwani alimpenda kwa dhati Takadini, pamoja na dharau, kejeli, kubaguliwa, ulemavu wake na kuonekana kuwa ni mtu aliyelaaniwa. Wazazi wake wanamtenga na kutomtambua kama ni mtoto wao tena. Suala hilo linatikisa jamii ya watu wa kijiji kile na hata kutaka kuwafukuza Sekai na mwanae lakini wanaokolewa na maamuzi ya busara ya wazee kwa kuwacha Shengai na mpenziwe Takadini waishi hali wakisubiri matokeo! Kuwa je mtoto atazaliwa sope? Na kuongeza ukoo wa masope na kijiji chao kuwa cha masope? Hapa ndio inapojulikana hatma ya Takadini na mkewe kwani anapata ujauzito na kufanikiwa kujifungua mtoto salama asiye Sope. Ilikuwa furaha kuu kwa mama na mtoto na wote pia. Wanaamua kurudi kijijini kwao walikotoroka ili kwenda kuwadhihirishia kuwa hata sope anaweza kuishi hapaswi kubaguliwa na kutengwa
MTINDO
Mwandishi ametumia mitindo kadha wa kadha ili kuipamba kazi yake na kuifanya ivutie wasomaji; mfano matumizi ya nafsi mbalimbali, matumizi ya nyimbo nk.
Matumizi ya nafsi
Kwa kiasi kikubwa yametawala matumizi ya nafsi ya tatu umoja na wingi katika sura zote.Mfano.uk. 30. “ aliingia ndani na kuanza kazi.”Piauk.3 “ Sekai alikoka moto nje ya kibanda, akaketi na kuzungumza na Pindai”.
Matumizi ya nafsi ya pili au dayalojia
Mfano uk 29 - 30. Mazungumzo kati ya Chivero na Sekai:“je umelala salama?“je umelala salama?Sijambo mwanangu, sijui wewe?Sijambo Sekuru,Na mwanao je?Naye hajambo.”
Matumizi ya nafsi ya kwanza. Mfano uk. 82 na 83
“lakini ghafla nilipata nguvu mpya”;“nilikuwa na nguvu kama kijana….”
Pia mwandishi ametumia nyimbo katika baadhi ya sura ili kuwaburudisha na kuliwaza wasomaji. Mfano uk. 2 wimbo aliouimba mke mwenza wa Sekai Rumbdzai.
“Mashamba yetu yamelimwa mbegu nazo zimepandwa zimechipua na kumea, sisi watatu tumepanda mavuno yetu; mheshimiwa wetu amemiliki mavuno kwa mikono yake halisi kutoka mashamba yetu yote lakini ni kipi alichoambulia kutoka ardhi ile isiyomea kitu?”pia ametumia wimbo uk. 34, 57, 85.
Matumizi ya hadithi ndani ya hadithi pia ni mtindo mwingine wa usimulizi alioutumia mwandishi.Mfanouk82Kutukwa alisimulia vijana hadithi enzi ya ujana wake na jinsi alivopambana na maadui vitani.
Matumizi ya Lugha
Lugha aliyotumia mwandishi ni lugha fasaha na rahisi inayoeleweka kwa wasomaji wake. Ametumia pia lugha nyinginezo kama vile lugha za kikabila.Maneno kama vile“Amai”,lenye maana yamama, “Sope”lenye maana yazeruzeru, “shumba”- simba, “mbira” – chombo cha asili cha muziki, “gudza” – blanketi lililotengenezwa kwa nyuzi za magome ya miti.nk.Hivyo mwandishi ametumia lugha hii ili kuwaleta wasomaji kwenye mazingira halisi ya kiutamaduni ya jamii ile.
Matumizi ya tamathali za Semi
Tashibiha:Mfanouk. 6 “ muda huenda polepole mithili ya mwendo wa kakakuona Uk.15 “ habari njema huchechemea kwa mguu mmoja lakina mbaya hukimbia kama Sungura”Uk.16 “….. alibaki kama kinyago cha mpingo”.Uk.28 “ sio kufurika kama Chura”Uk.33 “aligeuza shingo yake sawa na Mbuni”Uk.42 “ nywele kama vinyweleo vya mahindi yaliyokaribia kukomaa”Uk.82 “muziki ulikuwa kama chemchemi ya maji mwilini mwake”
Tashihisi:Mfanouk. 5 “ndege mbalimbali wakiimba kuikaribisha siku mpya”Uk. 7 “vivuli vya jioni viliongezeka urefu”Uk. 18 “maneno yananila mifupa yangu”Uk 25 “kifo kilinukia”
Tafsida:Mfano, uk. 83 “sehemu zake za siri”
Sitiari:Mfano, uk. 88 “Tapfumaneyialigeukambogo” Uk.97“mwana Mbwa hakuiba mfupa”, Tawanda mfupa ulikwenda wenyewe kuchezanaye.” Hapa mfupa umefananishwa na Shingai na Takadini ndio mwanambwa
Matumizi ya Semi
Methali:Uk. 45 “ kipofu huwa hachagui shimo la kutegea wanyama”uk.33 “ moyo mwema utakufanya uuwawe”
Misemo:Mfano.Uk. 12 “kufikiri katika siri ni sawa na safari ya mbwa”Uk. 100 “kanga hawezi kutua juu ya bua la mtama”Uk.101 “kibuyu kikubwa hakikosi mbegu ndani”Uk. 125 “fuvu la nyanilimekuwa kijiko kwa mlo wa mahindi”
Nahau:uk. 27 “ penzi langu kwake halikufua dafu”Uk. 88 “kutiana moyo wa ari”
Matumizi ya mbinu nyinginezo za kisanaa
Nidaa:Mfano,Uk.4 “Ha!” , “Ha! Atimuliwe tena? Mchawi?” Uk.16 “Mai, Wee!” Uk.39. “Ha! Iwe! Ha!”
Mdokezo:MfanoUk.3 “ndiyo Pindai, ninaogopa……….” Uk.42 “mtu mzima kama watu wenine ameamua………”
Takriri:Mfano,uk 57 “ mwanangu, mwanangu, mwanangu, wamekufanya nini?”
Wahusika
Sekai
Ni mke wa Makwati wa kwanza.
Ni mwanamke jasiri.
Anapinga mila potofu na mbaya za jamii yake.
Ni mvumilivu.
Ni mchapakazi mzuri.
Anajifungua mtoto zeruzeru ambaye ni laana kwa jamii yake.
Ni mtiifu na mwenye adabu.
Ana huruma na mnyenyekevu.
Ana mapenzi ya dhati.
Anafaaa kuigwa na jamii.
Takadini
Ni mtoto anayezaliwa na ulemavu wa ngozi( albino)
Anasadikika kuwa ni laana kwa jamii yake hivyo kupaswa kuuawa au kutupwa mbali.
Anaokolewa na mama yake kwa kutoroshewa katika kijiji kingine.
Anapokua anakua kijana jasiri.
Hapendwi na jamii.
Anabaguliwa na jamii, hana rafiki.
Ni mvumilivu na msikivu mwenye heshima.
Alimpenda Chivero sana.
Alikuwa mpiga mbira (chombo cha muziki cha kijadi) maarufu.
Alimuoa Shingai na kupata mtoto asiye Sope.
Makwati
Mume wa Sekai.
Ameoa ndoa ya mitara ana wake wanne.
Anashikilia mila na desturi potofu.
Hana mapenzi ya dhati kwa mwanae.
Hafai kuigwa na jamii.
Dadirai na Rumbidzai
Wake wengine wa mzee Makwati.
Wana wivu.
Hawampendi Sekai.
Wana roho mbaya kwani wanamwombea Sekai mabaya.
Ni katili kwani wanashinikiza Sekai na mwanae wauawe bila huruma.
Wasengenyaji.
Hawafai kuigwa na jamiii.
Pindai
Mke wa pili wa Makwati.
Ana upendo wa dhati kwa Sekai.
Ni mkweli.
Hana wivu.
Ni mshauri mzuri.
Anafaa kuigwa na jamii.
Chivero
Ni mzee wa kijiji cha mzee Masasa.
Anawapokea Sekai na mwanae baada ya kutoroka kwao kwa ukarimu mkubwa.
Ni mwenye roho nzuri.
Ana huruma sana.
Ni mganga wa tiba za asili.
Ana mapenzi ya dhati kwa Takadini na Sekai.
Anamrithisha Takadini uganga.
Ana busara na hekima.
Ni mshauri mkuu wa Mtemi Masasa.
Anafaa kuigwa na jamii.
Mtemi Masasa
Ana busara na hekima.
Ana huruma.
Anafuata mila na desturi ya jamii yake.
Ni msikivu.
Ni rafiki mkubwa wa Chivero.
Ni kiongozi bora.
Nhamo
Ni kijana katika kijiji cha mtemi Masasa.
Ana majivuno na jeuri.
Hampendi Takadini kwani alimbagua kumpiga na hata kumdhalilisha.
Hafai kuigwa n ajamii.
Tendai
Mke mdogo wa mwisho wa mtemi Masasa.
Aliolewa bila kupenda, hakumpenda mtemi Masasa kwani alimzidi umri.
Alikuwa rafiki mzuri wa Sekai.
Ana mapenzi ya dhati kwa Takadini.
Ana bidii na mvumilivu.
Nhariswa na mkewe
Ni wazazi wa Shingai
Wanashikilia mila desturi potofu
Hawakupenda kabisa kitendo cha mtoto wao kumpenda Takadini
Walimlazimisha kuolewa na Nhamo kwani walitaka sifa na maujiko
Walimtenga Shingai baada ya kutoroka na kuolewa na Takadini
Si wazazi wazuri
Hawafai kuigwa na jamii
Kutukwa
Ni mzee katika kijiji cha mtemi Masasa
Ni mpigaji mbira maarufu
Alimfundisha Takadini kupiga mbira
Alitoa mtazamo mbaya kwa wanakijiji wenzake kwa kuwaeleza sifa nzuri za Takadini
Alimpenda Takadini. Anafaa kuigwa na jamii
Mandhari
Mandhari aliyotumia Ben J Hanson ni mandhari ya kijijini kwani maisha ya watu na mazingira yanayoelezwa ni ya kijijini, masuala kama ya kilimo, ufugaji, sherehe za mavuno, makazi ya watu kukaa katika jumuiya ya pamoja kijamaa inayoongozwa na mtemi mmoja. Mfano mtemi Masasa, yote haya ni viashiria kuwa mandhari ni ya kijini. Mandahari ambayo mwandishi ameijengea mawazo yake na kuyaibua ni sadifu na halisi. Kwani maeneo ya vijijini ndiko kulikokithiri mambo ya imani potofu na za kishirikina kama vile kuwaua watoto Sope au albino.
Fani katika Riwaya ya Joka la Mdimu
Hakiki fani katika Riwaya ya Joka la Mdimu
MWANDISHI: ABDALLAH J. SAFARI
MCHAPISHAJI: HUDA PUBLISHERS
MWAKA: 2007
UTANGULIZI WA KITABU
Joka la mdimu ni riwaya iliyojengwa kwa visa tofautitofauti vinavojengana kukamilisha masimulizi. Ni riwaya inayosawiri au kuakisi mambo yaliyopita ya nyakati za nyuma ambapo kulikuwa na shida kama vile za mafuta ya petroli, Nguo, vyakula nk. Pamoja na hayo zipo pia dhamira au mawazo ambayo yanasawiri maisha ya Mtanzania wa leo kama vile masuala ya rushwa na uhujumu uchumi.
Kwa upande wa fani ni riwaya ambayo mwandishi amewaumba vyema wahusika wake kwa kuwavika uhalisia vyema, amepanga visa vyake na amejitahidi kutumia lugha yenye mvuto na vionjo vya kisanaa huku akiwaburudisha wasomaji kwa mtindo wa kipekee.
JINA LAKITABU
Jina la kitabu limewekwa katika lugha ya picha, JOKA LA MDIMU ni nyoka anayeishi katika miti ya kijani. Nyoka huyu hupendelea kuishi katika miti ya Minyaa na Midimu inayofanana na rangi yake. Nyoka huyu awapo kwenye miti hiyo si rahisi kumtambua kutokana na rangi yake kufanana sana na miti hiyo. Hivyo ni nyoka hatari sana kwa binadamu.
Mwandishi anatumia taswira ya Joka la Mdimu kufananisha na viongozi ambao ni wananchi wenzetu, wanafanana na sisi, ni ndugu zetu damu yetu. Lakini ni hatari mno kwani hutugeuka na kuwa mafisadi, wala rushwa, hawatimizi majukumu yao, ni walaghai nk. Badala ya kusaidia wananchi wao hujali maslahi yao kwanza na hivyo kusababisha mifumo ya kiuchumi kuendelea kuwa migumu kwa wananchi na kupelekea kuongezeka kwa kiasi kikubwa cha watu walio maskini au hohehahe. Hivyo jina la kitabu linasawiri yaliyomo ndani ya kitabu na katika jamii.
MUUNDO
Riwaya ya Joka la Mdimu imetumia muundo changamani yaani kwa kiasi fulani ametumia rejea au rukia pia ametumia muundo sahili au msago.
Mfano ametumia muundo warejeakatika sura ya Mindule ambapo anaanza kutueleza juu ya habari za Amani dereva wa taxi na adha anazopata kutokana na ukosefu wa mafuta na jinsi anavyoiendesha biashara yake hiyo. Lakini ndani ya sura hiyohiyo anaturudisha nyuma na kuanza kutuelezea namna Amani alivyopata kazi ya udereva Taxi na kutueleza juu ya mmiliki wa Taxi hiyo ambaye ni Shiraz Bhanj. Pia katika sura ya Boko anatueleza juu ya Safari ya Tino kwenda kumuona mwanae mgonjwa uk.73 ila hatuelezi inavyoendelea lakini anarukia kisa kingine cha Brown Kwacha na sura ya Kwale halafu badae anaturudisha nyuma na kuendelea kutuelezea juu ya habari za kuuguliwa kwa Cheche na Tino anapofika kumuona katika sura ya Dakta Makwati. Pia ametumia muundo wa moja kwa moja katika sura zingine kwani ameyapanga matukio yake katika usahili bila kuruka.
Pia mwandishi amegawanya visa na mtukio katika sura kumi ambapo kila sura ameipa jina kwa kutumia majina ya wahusika.
Sura ya kwanza, MINDULE:Hapa mwandishi anatueleza kuhusu habari za Amani dereva Taxi, masaibu anayopata katika kazi yake kutokana na uhaba wa mafuta katika vituo vya mafuta.
Sura ya pili, TINO:Hapa tunaelezwa kuhusu maisha ya Tino na kazi anazofanya ya kuvuta kwama. Tunaambiwa kuhusu hali ngumu ya maisha ya Tino na wakazi wengine wa Sega, hapa tunaelezwa pia kuhusu masuala ya uongozi jinsi ulivyo mbovu na ugawanywaji mbovu wa vyanzo vya uchumi na bidhaa.
Sura ya tatu, JINJA MALONI:Katika sura hii tunaelezwa kuhusu maisha ya Jinja Maloni, hapa anaibua dhamira kama vile za uvamizi, uhalifu na mauaji pia anaendela kutueleza kuhusu hali ngumu ya maisha.
Sura ya nne SEGA:Maisha ya wakazi wa Sega yanaelezewa hapa jinsi yalivyo ya dhiki, pia tunaelezwa kuhusu Tino na mkewe maisha yao yalivyo na familia yao, anaibua dhamira ya mapenzi ya dhati na upendo kwa familia.
Sura ya tano, BOKO:Hapa tunaelezwa kuhusu adha ya usafiri kwa watu, shida ya mafuta, ubovu wa miuondmbinu kama vile barabara, vinasemwa hapa.
Sura ya sita, BROWN KWACHA:Sura hii inaeleza habari za Brown maisha yake na tabia zake, anaibua dhamira kama vile uhujumu uchumi, biashara za magendo, suala la kutowajibika kwa watumishi, suala la kukosekana kwa uaminifu katika ndoa na mapenzi ya pesa ambapo sifa zote hizi alizibeba Kwacha.
Sura ya saba, KWALE:Hapa yanaelezwa mambo kuhusu hifadhi ya Kwale, safari ya Brown na Leila kwenda kutembea kwale. Hapa yanatajwa mambo ya udhalimu wa kuharibu mali za umma (maliasili za taifa) mfano pembe za ndovu, vipusa pia mapenzi yasiyo ya kweli.
Sura ya nane, DAKTA MIKWALA:Dakta Mikwala ndiye mhusika mkuu anayeelezwa hapa, tunalezwa juu ya ugumu wa upatikanaji wa huduma za afya kwani Cheche anashindwa kutibiwa kutokana na ukosefu wa fedha za kigeni.
Sura ya tisa, CHECHE:Tunaelezwa juu ya juhudi za Amani na Tino ili kumsaidia Cheche aweze kwenda kutibiwa Uingereza. Wanafanikiwa kupora benki na kupata pesa za kumtibu Cheche.
Sura ya kumi, MOTO:Hapa hatma ya visa vidogo vidogo imeelezwa kwa kutolewa hatma ya maisha ya Cheche na Brown Kwacha. Cheche alipata matibabu na kupona na Browna anafanikiwa kuirubuni serikali kwa kuipanga mahesabu ya uongo.
MTINDO
Mwandishi ametumia mitindo ya aina tofautitofauti ili kuweza kuipamba kazi yake ivutie.
Matumizi ya nafsi ya tatu Umoja. Imetawala: Mfanouk.5“Amani aliangalia…….” Uk.25 “Amani alijizuia” .Nafsi ya tatuwingi;mfano uk. 63“ wote walitoka nje kuelekea klabuni”.Piauk.53 “wale wanaume walimvamia”
Matumizi ya nafsi ya pili: Mfanouk.106 “ mmechoka kuangalia video?” “aa tumeshaziona mara nyingi tunaombaainanyingine.” Mazungumzo baina ya mke wa Brown na wanae.Pia mazungumzo baina ya Brown na Leila.Uk.113. “habari za asubuhi”“ Nzuri sijui wewe” alijibu“Uliota njozi njema?”"Wapi?""Kwa nini?"
Matumizi ya nafsi ya kwanza: Mfanouk. 39 “mimi nimemaliza” “….kuiba nimeiba sana….”
Matumizi ya nyimbo.Uk.70. wimbo wa Chaupele: “Chaupele mpenzi, haya usemayoKama ni maradhi, yapeleke kwa DaktariWanambia niache rumba,na mimi sikuzoeaSitaweza kuliacha rumba, kwa sababu yakoKama wanipenda, nenda kwa baba”Piauk.58 “sega! Sega! Sega!, usioogope” wimbo waliouimba washabiki wa michezo.
Masimulizi ya hadithi ndani ya hadithi: Hapa mwandishi amemtumia muhusika kusimulia kisa kingine kidogo ndani ya kisa kikuu. Mfanouk.39mhusika Tino anamsimulia mteja wake maisha yake ya mwanzo kabla hajaanza kazi ya kuvuta kwama.
MATUMIZI YA LUGHA
Mwandishi A. Safari ametumia lugha fasaha na inayoeleweka kwa wasomaji wake. Kuna matumizi ya lugha nyinginezo kama vile kiingereza.Uk.55 “city devils” uk.155 “I miss my family”, uk.24 “Hey man you will pay extra money”, uk.99 consignment”.Pia kuna matumizi ya lugha ya kiarabu, mfanouk.45 “Salaam aleikum mayitun” uk.42 “Inna Ilayhi Raajiunna!”, uk.13, “Insha Allah!”. Vilevile kuna matumizi ya lugha ya mtaaniuk.39 “msela”, “ndito”, “kashkash”.
Matumizi ya tamathali za semi.
Tashibiha:Uk.117 “ngozi yake nyeusi kama udongo wa mfinyanzi”Uk.122 “mweusi kama sizi la chungu”Uk.9 “Zepher 6 ile iliunguruma kama simba dume”Uk.10 “mteuzi mithili ya Mbega”Uk.35 “……miguu yake ikakazana mithili ya upinde uliotaka kufyatuliwa”
Sitiari:Uk.91 “Brown Kwacha alikuwa kinyonga”Uk.15 “sarahange wetu mboga kweli siku hizi”Uk.40 “huku twakaa vinyama vya mwitu”Uk.72 “sote ni kobe”
Tashihisi:Uk.109 “……gari lile zuri lilioondoka kwa madaha” Uk.143 “ kuta nyeusi za nyumba zaidi ya kumi zilisimama twe!kuomboleza” Uk.91 “pua zake zikalakiwa na riha na ashrafu ya manukato”;Uk.12 “utumbo ulimlaumu”; Uk.27 “mvua ikapiga kwa kiburi na kuviadhibu vibati vibovu”.
Tafsida:Uk. 49 “isijekuwa nimekukatiza haja!”,piauk.hohuo“kinyesi”.
Mbinu nyingine za kisanaa.
Takriri:Uk.151 “mwizi! Mwizi! Jambazi! Jambazi!”Uk.57 “shinda! Shinda! Shinda!”Uk.33 “karibu baba, kariibu kaka, karibu mkwe” Uk.72 “uhuru upi? Uhuru gani? Uhuru wa nini na nani?”
Mdokezo:Uk.149 “lakini……..”
Onomatopea au tanakali sauti:Uk. 1 “saa mezani niliendelea kugonga taratibu ta! ta! ta!”; Uk.10 “ikatoka sauti kali tupu ta nye nye”;Uk.67 “upepo wa stova uliolia shshsh”;
Tashtiti:Uk.113. leila anamuuliza Brown maswali ambayo anayajua majibu yake. Brown:“uliota njozi njema? Leila: Wapi?” Leila:Kwanini? Brown:Mwenywe unajua”
Nidaa:Uk.39 “Aaa! Limbukeni wa jiji anataka kunitia kashkash”: Uk 30 “nguo zangu Mungu wee!” Uk.42 “Inna Lillah wa Inna Ilayhi Raajiunna!” Uk.92 “Ah! Leila kwacha alimsalimia kwa furaha” Uk. 105 “Lahaula”
Matumizi ya Semi.
Methali:Uk.78 “asilojua mtu ni usiku wa kiza”Uk.83 “ukiona mwenzako anyolewa zako tia maji”Uk.98 “mtaka waridi sharti avumilie miiba”Uk. 99 “biashara haigombi”Uk.43 “ajizi nuksani huzaa mwana kisirani”
Misemo:Uk.10 “asiye na bahati habahatishi”Uk.47. “asiyezika hazikwi”Uk.64 “mmetupa Jongoo na mtiwe”Uk.98 “asali haichomvwi umoja”Uk.111 “ajali haina kinga”Uk.115 “mwenye macho haambiwi tazama”Uk.120 “matendo hushinda maneno”Uk.47. “asiyezika hazikwi”
Nahau:Uk.11 “sio unanilalia kila mara” –kunidhulumuUk.107 “alikonda akajipa moyo” –kujifariji moyo
Matumizi ya taswira
Taswira mwonekano imetumika, ambayo inatujengea picha kutokana na vitu tunavyovifahamu. Mfanouk.76 “alisema kijana mmoja wa kiume kavaa sketi, blauzi na sidiria iliyopachikwa juu yake. Kichwani alifunga kilemba.”Hii inatupa picha halisi ya huyo kaka kwani tunaposoma ni kama kweli tunamuona kutokana na jinsi mwandishi alivyoelezea. Piauk.135 “mwambie yule jamaa pale atayarishe kuku mzuri wa kukaanga”……… na kachumbari yenye pilipili”hii inamfanya msomaji ahisi ladha ya kuku na hiyo pilipili kwa maneno ambayo mwandishi ameyajengea taswira na hii ni taswira hisi.
Joka lamdimuni taswira ya nyoka mbaya ambaye amefananishwa na viongozi wabaya.
WAHUSIKA
AMANI
Ni dereva taxi
Ana upendo wa dhati
Ni mchapakazi
Ana hekima na busara
Ana huruma
Ni rafiki wa kweli wa Tino
Kutokana na hizo sifa amani ni mhusika bapa
Anafaa kuigwa na jamii
TINO (mhusikabapa)
Ni mchapakzi
Mlezi bora wa familia
Baba wa Cheche
Ana huruma
Ana upendo wa dhati
Ni makini
Ni jasiri
Ni mwanamichezo
Anafaa kuigwa na jamii
BROWN KWACHA
Ni mkurugenzi wa idara ya fedha za kigeni
Ni muhuni na Malaya
Fisadi na mla rushwa
Anafanya biashara haramu
Hana mapenzi kwa familia yake
Anapenda anasa
Si muaminifu kwa mkewe
Si muadilifu
Hafai kuigwa na jamii
Ni mhusika bapa
JINJA MALONI
Ni jasiri na mwenye nguvu
Ana huruma na upendo
Mchapakzi
Mlevi
Maskini
Ni mhusika duara
DAKTARI MIKWALA
Ni daktari bingwa wa mifupa
Anapenda rushwa
Si muwajibikaji katika kazi yake
Ni mlevi
Hafai kuigwa na jamii
Ni mhusika bapa
SHIRAZ BHANJ
Ni mfanyabiashara
Ni mtoa rushwa
Ana biashara za magendo
Rafiki wa Brown
Hafai kuigwa na jamii
Ni mhusika bapa
ZITTO
Ni mfanyakazi bandarini
Ni mwanamichezo
Ni jasiri ana kipato duni
Rafiki wa Tino na Aman
CHECHE
Ni mtoto wa Tino
Ana nidhamu na bidii
Ni mwanamichezo
Ana upendo kwa wazazi wake
Ni mtiifu na msikivu
Mcheshi na mudadisi
Alivunjika kiuno michezoni
Ni mhusika bapa
MWEMA
Ni mke wa Tino
Mvumilivu
Ana mapendo ya dhati kwa familia yake
Ni mchapakazi
Ni mhusika bapa
JOSEPHINE NA LEILA
Wasichana wahuni waliojiuza kwa Brown Kwacha
Hawafai kuigwa na jamii
MANDHARI
Mandhari aliyoitumia mwandishi ni ya mjini, anataja baadhi ya maeneo ya nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam kama vile Boko, Sega, Mindule. Mandhari hii ni sadifu kwa yale ambayo mwandishi ameyaeleza kwani masuala ya rushwa, upotevu wa haki, hali ngumu ya uchumi na maisha kwa ujumla, ni matatizo halisi ya jamii ya Tanzania.
Fani katika Riwaya ya Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe
Hakiki fani katika Riwaya ya Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe
JINA LA KITABU: NGOSWE PENZI KITOVU CHA UZEMBE
MWANDISHI: EDWIN SEMZABA
WACHAPISHAJI: NYAMBARI NYANGWINE PUBLISHERS
MWAKA:2006
UTANGULIZI WA KITABU
Ngoswe penzi kitovu cha uzembe ni tamthiliya maarufu sana ambayo imewahi kuigizwa katika redio Tanzania na katika majukwaa mbalimbali hapa nchini. Ni tamthiliya ambayo imeundwa vyema katika vipengele vya fani na maudhui. Ameteua lugha nzuri na yenye mvuto kwa wasomaji yenye mbinu za kifasihi zilizosheheni, muundo wenye mtiririko mzuri, unaoakisi kuanza kuchipuka kwa matukio mpaka kilele cha matukio. Wahusika wamebeba vyema uhusika wao mfano Ngoswe.
Ameibua dhamira kuhusu mambo yanayoigusa jamii ya leo kama vile uzembe, madhara ya ulevi, uzembe kazini, suala la matabaka kati ya mjini na vijijini. Mtazamo, falsafa na msimamo wake ni kulenga kuibadilisha jamii na kuleta maendeleo.
JINA LA KITABU
Jina la kitabu “Ngoswe penzi kitovu cha uzembe” ni jina ambalo limesawiri vyema yaliyomo ndani ya kitabu hicho, kwani Ngoswe ndio jina la mhusika mkuu anayebeba dhamira kuu ya tamthiliya. Pia penzi limeonekana kuwa ni kitovu cha uzembe kwani ndio yaliyopelekea kuteketezwa kwa karatasi za takwimu za sensa. Hivyo jina la kitabu si tu kwamba limesawiri yaliyomo katika kitabu bali pia katika jamii.
MTINDO
Mtindo alioutumia mwandishi ni dayalojia au majibizano. Mwandishi amepanga visa na masimulizi kwa kutumia majibizano ya wahusika.
Matumizi ya nafsi ya kwanza. Mwandishi ndiye ameyafafanua na kuelezea baadhi ya matukio. Katika karibu kurasa zote mwandishi ameonekana kuwa ndiye msimuliaji wa matukio.
Matumizi ya nafsi ya pili. Hapa watu wawili na zaidi wanajibizana. Tamthilya hii wahusika wanaojibizana kuibua dhamira na migogoro. Kuna majibizano baina ya mzee Mitomingi, Ngoswe na Mazoea nk.unaweza kupata mfano uk. wowote kwani ndio mtindo uliotawala.
MUUNDO
Muundo uliotumika ni muundo wa mojakwamoja au sahili. Kwani ameonesha tangu mwanzo wa mambo mpaka mwisho, anajenga visa vidogo mpaka visa vikuu au kileleni.Amepanga visa na matukio yake katika maonesho matano. Kila kichwa kina maelezo yaliyojadiliwa katika onesho hilo.
KIJITO:Hapa yanaeleza jinsi mambo yanavyoanza. Jinsi Ngoswe anavyoingia kijijini anavyopokelewa na kuanza kufahamiana na wenyeji wake.
VIJITO:Hapa Ngoswe anaanza kufanya kazi iliyompeleka kijijini na tunaanza kuoneshwa changamoto anazokumbana nazo.
MTO:Ni mwendelezo wa matukio ya mwanzo hapa visa vinazidi kukua.
JITO:Hapa Ngoswe anakumbana na changamoto nyingi zaidi katika kazi yake. Na hapa anazidi kuanguka kwani anajiingiza katika mapenzi na msichana Mazoea, anaendekeza ulevi na kuharibu kazi kabisa.
BAHARINI:Hapa inaoneshwa mwisho wa mambo jinsi yalivyokuwa. Yanaonekana mahojiano baina ya Serikali na Ngoswe na Mitomingi juu ya uzembe uliofanyika wa kupoteza takwimu na hapa ndipo suluhisho linapotolewa juu ya matatizo hayo.
WAHUSIKA
NGOSWE
Kijana wa kiume umri kati yamiaka 20-25
Ameelimika na amestaarabika
Anatumwa na serikali kufanya sensa kijijini
Anajihusisha na mapenzi na msichana mazoea
Ni mlevi
Hana umakini katika kazi
Aliharibu kazi ya serikali
Hafai kuigwa na jamii
MAZOEA
Ni msichana mwenye umri kati ya miaka 18-20
Ni binti wa Mzee Ngengemkeni Mitomingi
Hana elimu na hajastaarabika
Ana nidhamu ya woga
Ana tama
Hana msimamo alikubali kuchukuliwa na Ngoswe hali akijua alishatolewa mahari
Hafai kuigwa na jamii.
NGENGEMKENI MITOMINGI
Ni balozi katika kijiji chake
Ni baba mzazi wa Mazoea
Ameoa ndoa ya mitara, ana wake wawili
Hajaelimika
Anashikilia mila na desturi za kale
Mlevi
Mkali sana
Anateketeza karatasi za takwimu
MZEE JIMBI
Mwanakijiji
Hajaelimika kwani hajui hata umri wake
Ni mlevi
Ana wake wawili
Anashikilia ukale
MAMA MAZOEA
Mke mkubwa wa Mitomingi
Mama yake Mazoea
Mlezi wa familia
Hapewi nafasi ya kutoa maamuzi katika familia
MAMA INDA
Mke wa pili Mzee Mitomingi
Mama yake Huzuni
Hapewi nafasi ya kutoa maamuzi
Ni mlezi wa familia.
MANDHARI
Mandhari ya tamthiliya hii imechorwa katika mazingira ya kijijini. Mambo yanayoelezwa ni ya kijijini mfano kilimo, hali ya watu kimaisha, huduma duni sana za kijamii kama vile shule, umbali wa makazi toka nyumba moja hadi nyingine. Haya yanatudhihirishia vyema mandhari hiyo ambayo kwayo imeibua dhamira mbalimbali kama vile umaskini, ukosefu wa elimu, huduma duni za afya vijijini, masuala ya imani potofu nk.
MATUMIZI YA LUGHA
Lugha aliyotumia mwandishi ni lugha fasaha na rahisi kueleweka kwa wasomaji. Pia kuna matumizi ya lugha nyingine mfanouk. 1 “bell bottom”
Matumizi ya semi
Methali:Uk.22 “Penye nia pana njia”.Uk.27 “Waona vyaelea vyaundwa.”
Misemo:Uk.14 “Akuwaniae ujovu haji kweupe”
Nahau:Uk.11 “hebu keti tutupe mawe pangoni” –tule chakulaUk.7 “mbongo zimelala”-ana maarifaUk.14 “pombe na yeye ni pete na chanda”- anapenda pombe sana.
Matumizi ya tamathali za semi
Tafsida:Uk.21 “Wala hajarudi, kama ingekuwa ni kujisaidia si angekuwa amekwishamaliza?”
Tashbiha:Uk.1 “vumbi jekundu kama ugoro wa subiana”Uk.8 “sarawili yake miguuni kama kengele ya bomani”Uk.17 “wanaondoka huku wakitazamwa kama vile mizuka”
Sitiari:Uk.7 Mama Mazoea : “kiziwi mkubwa wee!”Uk.14 “pombe na yeye ni pete na chanda!”Uk.26. “karatasi? za takwimu? Ndio wanyama gani hao?”
Mubaalagha:Uk.11 Mama Mazoea : “kupeleka chakula ndio umefanya makao!”Mama mazoea : “Kujibu swali ndio ukachukua mwaka mzima!”
Mbinu nyingine za kisanaa
Mdokezo:Uk.22 Mazoea : “sijui….. siwezi….. namuogopa baba”Uk.16 Ngoswe : “huyo mtoto wenu wa kwanza anaishi hapa au…..”
Takriri:Uk.9 “Mama Masikio! We Mama Masikio!”Uk.13. “Hodi! Hodi!”Uk.2 “karibu karibu”
Tashtiti:Uk.5 Ngoswe: “hivyo waitwa nani?”Mazoea: “mie?”Uk.22 Ngoswe: “mchumba? Kwani mchumba ni kitu gani?”Uk.26 Mitomingi: “karatasi? Za takwimu? Ndio wanyama gani hao?Hapa wahusika waliuliza maswali ambayo majibu yake waliyaelewa ila kutokana na kutaka kudhihirisha hasira, msisitizo nk. Ndio maana wametumia tashtiti.
Onomatopea/tanakali sauti:Uk.7 Kifaruhande anacheka “Ha! ha! ha!
Ujenzi wa taswira
Mwandishi ametumia taswira ya mto kuelezea visa vyake. Sehemu ya kwanza ni sehemu ya kijito, kijito ni kimto kidigo mwandishi hapa anaanza kueleza mambo yakiwa machanga kabisa ndio yanaanza.
Sehemu ya pili ni vijito. Huu ni muunganiko wa vijito vidogovidogo hapa mwandishi anaanza kueleza visa vidogovidogo. Sehemu inayofuata ni sehemu ya Mto. Hii inaashiria mambo yameanza kuwa mazito, visa vinakua zaidi na Ngoswe anazidi kuingia katika changamoto kubwa zaidi.
Pia Jito ni taswira ambayo mwandishi ameitumia kuashiria hatari zaidi mambo makubwa zaidi na hapa ndipo tunaona Ngoswe anaanguka kabisa katika kazi yake kwani Jito ni lenye maji mengi na yanayoenda kwa kasi hivyo huhitaji umakini mkubwa zaidi.
Mwisho sehemu ya Bahari ambapo hapa ndipo hatima ya mambo inaelezwa Ngoswe anazama na kupotea kabisa! Hafanikiwi kutoa takwimu kwani karatasi zilichomwa moto.

Uhakiki wa Fani katika Tamthiliya
Fani katika Tamthiliya ya Kilio Chetu
Hakiki fani katika tamthiliya ya Kilio Chetu
MWANDISHI: MEDICAL AID FOUNDATION
WACHAPISHAJI: TANZANIA PUBLISHING HOUSE (TPH)
MWAKA: 1996
JINA LA KITABU
KILIO CHETU ni jina ambalo linaasadifu yaliyomo katika kitabu. Masuala yanayotajwa mule kama vile upotofu wa maadili kwa vijana wadogo kama Suzi na Joti, suala la mimba za utotoni, madhara ya gonjwa hatari la UKIMWI kwa jamii kweli ni kilio chetu ni kilio cha Taifa zima. Kwani katika mambo yanayoiyumbisha jamii kimaendeleo ni upotovu wa maaadili.
Jina hili ni sadifu katika jamii. Mwandishi amelitumia wakati muafaka kabisa kwani mambo anayoyaeleza ndio changamoto katika jamii ya leo. Hivyo kupitia hili jamii si budi kubadilika.
UTANGULIZI WA KITABU
Kilio chetu ni tamthiliya ambayo imejieleza vyema katika fani na maudhui. Tamthiliya hii inamuhusu mhusika Suzi na Joti ambao ni watoto wadogo sana. Wanajiingiza katika mapenzi katika umri mdogo kutokana na ukosefu wa elimu ya kijinsia. Inatueleza kuhusu athari za ugonjwa huu usiobagua. Pia tunafahamishwa kuhusu mtazamo wa wazazi na walezi kuhusu utoaji wa elimu ya jinsia kwa vijana wao. Wapo wanaolipokea kwa mtazamo chanya na wengine hasi.
Kwa ujumla ni tamthiliya nzuri kwani ina mtazamo wa kimabadiliko unaolenga kuwakomboa vijana wetu kutoka katika janga la ugonjwa hatari wa UKIMWI.
MUUNDO
Sehemu ya kwanza:Inaonesha jinsi gonjwa la UKIMWI linavyoikumba jamii. Mwandishi anaeleza kuhusu Dubwana linaloikumba jamii.
Sehemu ya pili:Mwandishi anaeleza kuhusu athari za UKIMWI, jambo ambalo lilipelekea kifo cha Fausta. Pia Suzi agundulika kujihusisha na mapenzi baada ya kukutwa na vidonge vya kuzuia mimba.
Sehemu ya tatu:Inaeleza juu ya watoto ambao wameshajiingiza katika suala la mapenzi licha ya kuwa na umri mdogo mfano ni Joti na Suzi. Pia madhara ya utandawazi yanaelezwa hapa mfano kuoneshwa kwa picha za ngono.
Sehemu ya nne:Tunaelezwa juu ya tabia hatarishi za Joti za kuwa na mahusiano na wasichana wengi mfano Chausiku, Yoranda, Gelda na Suzi. Hapa Joti anafanikiwa kumrubuni tena Suzi. Pia tunaoneshwa jinsi Ana anavopingana na vishawishi kutokana na kupata elimu ya jinsia.
Sehemu ya tano:Suzi anagundulika kuwa na mimba ya Joti, anajutia kosa hilo anajilaumu sana.
Sehemu ya sita:Inatuonesha jinsi Joti alivyokuwa magonjwa tayari kutokana na UKIMWI. Hapa ushauri mzuri unatolewa kuhusu namna ya kumtunza mgonjwa wa UKIMWI na kumfanya aishi kwa matumaini. Hapa mwandishi anapinga mila potofu kuhusu UKIMWI kuwa si kurogwa bali ni ugonjwa unaoambukizwa.
MTINDO
Tamthiliya hii imesheheni katika mitindo kadha wa kadha inayopamba kazi hii. Mtindo uliotumika ni dayalojia au majibizano.
Mwandishi ametumia mtindo wa mianzo na miisho ya kifomula ya usimulizi ambao ni mtindo wa usimulizi wa fasihi ya kiafrika. Mfanouk.1 mwandishi anasema “paukwa….. pakawaa…. Niendelee…. nisiendelee? ….. au mmechoka? Uk.113,piauk.36 mwandishi anasema “na hadithi yangu imeishia hapo”.Pia mwandishi ametumia mtindo wa utambaji kwani ndiye anayesimulia na kuelezea matukio.
Matumizi ya nafsi
Nafsi ya pili ndiyo iliyotawala, mwandishi ametumia majibizano ya watu wawili mfano Suzi na Joti, pia watu watatu n.k.Pia mwandishi ametumia tanzu nyingine za fasihi mfano wimbo uk.27
Wahusika
SUZI
Ni binti mdogo wa darasa la sita
Anajihusisha na mapenzi na Joti
Hana msimamo
Anapata mimba katika umri mdogo
Ana hatari ya kuwa na UKIMWI
Hakupewa elimu ya jinsia
Ana tamaa kwani alitamani vitu alivyohongwa na Joti.
JOTI
Ni kijana mdogo wa kiume
Ana mahusianao ya mapenzi na wasichana wengi Suzi, Gelda, Yoranda na Chausiku
Hana elimu ya jinsia
Ana makundi mabaya ya marafiki
Anaathirika na kufa kwa gonjwa la UKIMWI
Amechangia kuharibu maisha ya Suzi kwa kumrubuni
Ni mlaghai
Hafai kuigwa na jamii
MAMA SUZI
Ni mzazi wa Suzi
Anashikilia ukale hataki mabadiliko
Hampi mwanae elimu ya jinsia
Alichangia kuharibu maisha ya Suzi
Ni mkali sana katika malezi hatumii busara bali hasira
Hafai kuigwa na jamii
BABA JOTI
Ni mzazi wa Joti
Hayupo tayari kutoa elimua ya jinsia
Anashikilia ukale
Ni mkali anatumia viboko kuelimisha jambo ambalo si sahihi
Amechangia kuharibu maisha ya Joti
Ni muhuni, si muaminifu katika ndoa yake
Hafai kuigwa na jamii
ANNA
Ni binti mdogo wa shule
Ana elimu ya jinsia
Ana msimamo mzuri anashinda vishawishi
Anatoa elimu kwa vijana wenzake kuhusu athari za kujiingiza katika mapenzi katika umri mdogo
Ana tabia njema
Hana tama
Anafaa kuigwa na jamii.
BABA ANNA
Ni mzazi wa Anna
Anatoa elimu ya jinsia kwa wazazi na watoto
Ni mlezi bora
Alichangia maisha ya Anna kuwa ya mafanikio
Anafaa kuigwa na jamii
MJOMBA
Ni kaka yake Mama Suzi
Anaendana na wakati wa sasa
Anatoa elimu ya jinsia kwa vijana na wazazi
Ni mlezi bora ni mshauri bora
Anatoa elimu ya UKIMWI kwa Baba Joti anapinga mila potofu
Anafaa kuigwa na jamii
MAMA JOTI
Mzazi wa Joti
Ndoa yake ipo matatani kuingiliwa na mke mwingine
Anaelewa kuwa jamii imebadilika na wazazi wanapaswa kuwaelimisha watoto
JIRANI
Ni jirani wa Baba Joti
Ana imani potofu za kishirikina, anaamini Joti alilogwa
Haamini kuwa UKIMWI upo
CHAUSIKU
Ni msichana wa mtaani
Mfanyabiashara wa vitumbua
Ni jirani wa Suzi
Ana tabia mbaya ni muhuni
Alichangia kuharibu maisha ya Joti
Ana mahusiano ya kimpenzi na vijana wadogo mfano Joti na watu wazima pia, mfano Mpemba.
CHOGO, MWARAMI NA JUMBE
Ni marafiki wa Joti
Ni wanafunzi wadogo
Si marafiki wazuri
Wana tabia mbaya wanashauriana kuhusu mambo mabaya
Hawafai kuigwa na jamii
MANDHARI
Mandhari aliyoitumia mwandishi ni ya mjini, hii ni kutokana na maelezo ya mhusika jirani anaposemauk.32 “……mie toka siku ile nimwone hospitali sijakaa mjini. Nilikwenda zangu shamba kupambana na Nyani wala nafaka.”Pia lugha ya mtaani iliyotumiwa na vijana Joti, Mwarami na wenzake, masuala ya picha ya “X” yaani viashiria vya mambo ya mjini kwani yamekithiri sana mijini. Maeneo yanayotajwa kama vile uwanja wa Sabasaba ni uwanja uliopo mjini, masuala ya lifti kwa wasichana hasa wanafunzi yapo mijini. Mfano.uk.27 pia kuna mandhari ya nyumbani na mtaani.
Mandhari aliyotumia mwandishi inasawiri maudhui yake katika jamii. Kwani anaibua mambo yaliyo katika jamii.
MATUMZI YA LUGHA
Lugha iliyotumika ni lugha iliyo na ubunifu wa kipekee wenye mvuto wa kisanaa. Lugha ni rahisi na inayoeleweka vyema kwa hadhira lengwa. Pia kuna matumizi ya lugha nyingine mfano kiingereza na lugha za kikabila. Kiingereza mfanouk.21 “tuition” uk.16 “come”.Lugha za kikabila mfano wimbo uk.35“Joti afitwe sanda salauya; Ena ena salauya …………………….”
Matumizi ya lugha ya mtaani
Mfanouk.16 “mshefa” “mshikaji”-rafiki.Uk.17 “kamba” –kudanganya jambo;Uk.22 “vidosho” –wasichana;Uk.16 “kanitolea nje”– kukataa jambo fulani.
Matumizi ya tamathali za semi
Tashibiha:Uk.1 “wakapukutika kama majani”Uk.5 “mgumu kama mpingo”Uk.6 “miti inaungua kama mabua”Uk.13 “Dubwana limetanda kama utando wa Buibui”
Tashihisi:Uk.2 “vifo vikawazoa”kifo huua tu lakini kimepewa uwezo wa kuzoa
Sitiari:Uk.8 “We Mbwa mweusi”Uk.9 “Nyoka wee”Uk.21 “huyo kinyago wako anakimbia nini?”
Tafsida:Uk.4 “kafa kwa kukanyaga nyaya”– kafa kwa UKIMWI
Mubaalagha:Uk.4 “Mtu si mtu, kizuka si kizuka”
Matumizi ya mbinu nyingine za kisanaa
Tanakali sauti/ Onomatopea:Uk. Joti akasema“….acha moyo unipwite “Pwi! Pwi! Pwi!”Uk.25 “….hebu nitolee uchafu wako mie ptuu!”
Tashtiti:Uk.15 “….huyu ni Suzi kweli au nani?”Uk.36 “kwanini Joti……… kwanini Joti afe?”
Takriri:Uk.1 “watu wakapukutika, wakapukutika…..” “tunakwisha, tunakwisha”Uk.2 “vifo vikawzoa, vikawazoa .…. vikawazoa”Uk.16 “piga domo, piga domo”
Matumizi ya semi
Methali:Uk.6 “wembamba wa Reli Treni inapita”Uk.11 “mzazi usipomfunza walimwengu watamfundisha”Uk.19 “shukrani ya Punda ni mateke”Uk.24 ‘Ndege mjanja ananaswa na tundu bovu”
Nahau:Uk.6 “nimekuvulia kofia”-nakuheshimuUk.21 “anajigongagonga” –anajipendekeza
Misemo:Uk.4 “kuwa nyumanyuma kama koti”Uk.6 “kifua simkingii maana siwi naye”Uk.7 “makapera kibao Mume wangu wa nini?”Uk.22 “mapenzi ni tiba”Uk.26 “…..unakimbilia suti na nepi hujavaa”
Matumizi ya taswira
uk.1 “dubwana” –ugonjwa wa UKIMWI;Uk.7 “Nguru” –aina ya Samaki wabaya–amefananishwa na mtu mbaya;Uk.21 “kinyago”- Suzi.
Fani katika Tamthiliya ya Orodha
Hakiki fani katika tamthiliya ya Orodha
JINA LA KITABU
Jina la kitabu ORODHA ni sadifu kwa yaliyomo. Katika kitabu inatajwa orodha ya mambo ambayo yanaweza kusaidia kuepusha UKIMWI. Orodha hii inatolewa na mhusika Furaha ambaye aliomba isomwe katika mazishi yake. Mambo hayo au orodha hiyo ni pamoja na uwazi, ukweli, uadilifu, matumizi ya kondom, uelewa, upendo, elimu, uwajibikaji na msamaha. Mwandishi anaona kuwa endapo mambo haya yatazingatiwa hakika tutapunguza maambukizi zaidi ya virusi vya UKIMWI.
UTANGULIZI
Tamthiliya ya Orodha ni tamthiliya inayohusu suala zima la ugonjwa wa UKIMWI na madhara yake katika jamii. Mwandishi anaweka wazi kuhusu gonjwa hili. Mhusika mkuu Furaha anaathirika na gonjwa hili na kufariki dunia. Kimaudhui tamthiliya hii imesawiri maisha ya sasa ya jamii ya Watanzania kwani ugonjwa huu bado ni tishio. Kwa upande wa fani, mwandishi amewaumba vyema wahusika wake, muundo wake ni unaomvutia msomaji kujua ni nini kingeendelea mbeleni, ameteua lugha nzuri ya kisanaa. Haya yote yanajielekeza katika uchambuzi tutaoenda kuufanya.
MUUNDO
Mwandishi ametumia muundo changamano kwani katika sehemu ya 1 na 2 anatuonesha mazishini ambapo yanafanyika mazishi ya Furaha. Sehemu ya 3-20 anaanza kutuelezea juu ya maisha ya Furaha mpaka kifo chake ambao huu ni msago au muundo sahili. Halafu sehemu ya 17-19 na ishirini 20 anatuonesha juu ya mzozo wa orodha na hatma ya mazishi ya Furaha.
Mwandishi ameweka kazi yake katika onyesho moja. Na katika onyesho hilo ameweka sehemu ndogondogo ishirini zinazojengana kukamilisha tamthiliya nzima.
Sehemu ya kwanza:Inaanza kwa kuonesha vifani vinne vimeganda kifani cha kwanza, wahusika wameganda katika mikao inayotambulisha wasifu wa wahusika. Kifani cha pili kinaonesha wagonjwa wakiwa katika mateso. Kifani cha tatu kinaonesha wagonjwa wakiwa katika maumivu makali sana.
Sehemu ya pili:Hapa inaelezwa juu ya siku ya msiba wa Furaha. Mama yake Furaha anaeleza watu kuwa Furaha aliacha orodha ambayo alitaka isomwe hadharani katika mazishi yake. Suala hili linazua mgogoro na hofu kuu kwa watu. Padre James anaweka juhudi kuzuia barua isisomwe.
Sehemu ya tatu:Sehemu hii tunaoneshwa juu ya maisha ya Furaha nyumbani kwao, baba na mama yake na wadogo zake. Baba yake anaonekana kutofurahishwa na mwenendo wa Furaha kwani anamkanya kwa maneno makali ya laana. Kama vile hatopata mtu wa kumuoa. Anamuasa Furaha kuonesha mfano mzuri kwa wadogo zake.
Sehemu ya nne:Hapa Furaha kwa mara ya kwanza anatoroka nyumbani kwao usiku wa manane pamoja na Mery kwenda baa. Mdogo wake anabaini kitendo hicho na kutishia kushitaki kwa wazazi lakini Furaha anamtishia kumchinja.
Sehemu ya tano:Wanaonekana Mery na Furaha wako baa wakinywa pombe na kucheza na wanaume. Hapa Furaha anajifunza mambo mapya mabaya kama vile ulevi kupitia rafiki yake Mery. Pia anaanza mahusiano ya mapenzi na wanaume mfano Bw. Ecko.
Sehemu ya sita:Hapa Furaha anamwendea Padre James kwa ajili ya maungamo kwani alikunywa pombe na kulala na wanaume, lakini Padre James anamwambia Furaha aende kesho yake katika chumba chake cha kujisomea nyuma ya kanisa na taa zitakuwa zimezimwa kuficha utambulisho. Na hapa ndipo Furaha anapozini na Padre kwani Padre alishikwa na tamaa.
Sehemu ya saba:Baba na Mama Furaha wanamkanya Furaha kuhusu tabia yake ya umalaya na ulevi. Furaha anaomba msamaha.
Sehemu ya nane:Furaha anakutana na Kitunda aendapo sokoni, katumwa na mama yake. Lakini anamkuta Kitunda akisikiliza mziki Furaha anashawishika, Kitunda anamshawishi zaidi na hata avute bangi ila hakubali. Pia wanazungumzia juu ya jiji la Dar es Salaam. Habari hizo zinampagawisha Furaha na kutamani sana aende.
Sehemu ya tisa:Salim anarudi toka masomoni Dar es Salaam. Anaonana na mpenzi wake wa zamani Furaha. Wanasalimiana kwa hamu na furaha tele.
Sehemu ya kumi:Salim na Furaha wanakutana na kuelezana habari za kitambo kwani walitengana kwa muda mrefu, wanapanga mipango juu ya mahusiano yao.
Sehemu ya kumi na moja:Wanakijiji wanazungumzia juu ya tabia ya umalaya ya Furaha, pia wanazungumzia juu ya mahusiano ya Furaha na Salim. Hawapendezwi na tabia ya Furaha na kuamua kumtaarifu mama yake.
Sehemu ya kumi na mbili:Mama Furaha anachukua jukumu la kumhoji mwanae juu ya tabia yake. Furaha hakubaliani na lolote. Hali ya Furaha inaanza kudhoofu na mama yake anaaingiwa hofu.
Sehemu ya kumi na tatu:Furaha yupo sebuleni akisali. Baba yake anamuonya zaidi na kumshauri aolewe na Salim kwani ni kijana mzuri anayefaa.
Sehemu ya kumi na nne:Hapa hali ya Furaha inazidi kutetereka, anachukuliwa vipimo vya damu na kugundulika kuwa ana virusi vya UKIMWI. Hali hii inamshitua sana mama yake. Anamuhoji kama aliwahi kutembea na mwanaume yeyote, anamueleza njia za upataji wa UKIMWI na Furaha naanza kulia kwa kutambua kosa lake.
Sehemu ya kumi na tano:Wanakijiji wanapata habari juu ya kuumwa kwa Furaha na wanazieneza. Juma, Kitunda, Padre James, Salim, Bw. Ecko wanapata pia habari hizi. Wanaingiwa na hofu kubwa endapo watakuwa wameambukizwa UKIMWI au majina yao yamo kwenye orodha?
Sehemu ya kumi na sita:Salim anaamua kumtembelea Furaha nyumbani. Akiwa katika hali mbaya sana ya ugonjwa Furaha anamuweka wazi Salim juu ya kuathirika kwake kwa UKIMWI. Salim anaingiwa hofu anamuomba Furaha barua yenye orodha kwa shauku lakini hampatii. Hali hii inamuudhi Salim. Na hapa ndipo Furaha anapokata roho!
Sehemu ya kumi na saba:Hapa tunaelezwa juu ya juhudi za Bw. Ecko, na Juma za kutaka kuiba barua yenye orodha katika chumba alicholazwa maiti ya Furaha. Lakini hawafanikiwi. Familia ya Furaha wanaamini kuwa kuna mizimu katika chumba cha maiti kutokana na kelele za Juma na Bw. Ecko, na Kitunda.
Sehemu ya kumi na nane:Padre James anaomba kusomewa barua hiyo kabla ya mazishi lakini mama furaha anakataa. Anaamua kuitafuta mwenyewe sebuleni bila mafanikio.
Sehemu ya kumi na tisa:Asubuhi siku ya mazishi. Ecko, Juma na Salim wanaonekana wakitafuta suluhu ya namna ya kuzuia orodha isisomwe ila hawafanikiwi.
Sehemu ya ishirini:Ni siku ya mazishi ambapo Mama Furaha anaisoma barua ya orodha. Padre James anajitahidi kumpinga mama Furaha asiisome orodha lakini hafanikiwi. Salim anapora barua na kuchana baadhi ya sehemu lakini hiyo haiharibu kitu kwani anaunga vipande na kusoma mbele ya wanakijiji wote. Ndani ya orodha hakuna jina la mtu yeyote lililotajwa bali mambo yatakayosaidia kuuepuka UKIMWI.
MTINDO
Mtindo aliotumia mwandishi ni wa dayalojia au majibizano. Mwandishi ameunda visa na masimulizi yake kupitia majibizano ya wahusika. Pia kwa kiasi kidogo ametumia mtindo wa monolojia, mfano uk. 27 padre James anasema:
“Bwana natazamiwa kuiendesha sala hiyo! Ni kitu ambacho hakikubaliki! Shetani yu kazini kjijini hapa! Furaha anavuna mbegu ya kifo aliyoipanda! Oh! Njia ya mtumishi wa bwana ni ngumu. Imejaa majaribu! Mtu lazima awe na nguvu na kuileta kazi ya bwana kwa watu hawa wa kawaida. Nimepewa kazi iliyo rahisi lakini ni ngumu sana! ni kazi ya upweke!!! Mwili ni mdhoofu! Oh Bwana utulinde.”
Hapa padre James aliongea mwenyewe akifikiri kuwaza na kujutia kazi anayofanya. Pia uk. Huohuo tunaona maneno ya Salim anaongea mwenyewe, pia uk.10, 23,37 na 40.
Pia mwandishi ametumia mtindo wa barua katika kazi yake lengo ikiwa ni kuweka mkazo katika mambo muhimu ya kuzingatia ili kuiepuka UKIMWI. Barua yenyewe ilisema hivi, uk.44“Kwa Kijiji changu kipendwa,
Nawasukuru kwa kufika kwenu na kuyasikiliza maneno yangu ya mwisho. Msiogope kwani nadhani maneno haya yanaweza kuwasaidia. Katika hii miezi ya mwisho nimelala kitandani nikifa, nikizidi kuugua. Nilipata muda mwingi wa kufikiri, kubadilika kukua kama mtu; hata ninapokuwa nakufa. Katika ukurasa unaofuata kuna Orodha ya vitu amabvyo vilisaidia kuyafupisha maisha yangu, orodha ambayo inaonesha kwenu nyote ukweli juu ya kifo changu. Mama, tafadhali wasomee watu wote orodha hii.
Uepukaji
Kondomu,
uaminifu ,
elimu,
welewa,
uwazi,
uadilifu,
uwajibikaji,
ukweli,
upendo,
msamaha.
Ukosefu wa mambo yote haya ndio ulioniua. Ufuatiliaji wa mambo yote haya unaweza kuwaokoa ninyi nyote. Chukueni orodha yangu na muinakili. Ipelekeni kwenye vijiji vingine, miji mingine na majiji mengine katika nchi yetu hii nzuri. Wanusuruni watu wetu ili waweze kuyafaidia maisha kikamilifu .Wanusuruni watoto wetu ili wasiwe yatima. Muinusuru Afrika…. Afrika yetu nzuri
Kwa kijiji changu kiishi maisha marefu na kiwe na furaha! Msihukukumu mapema mno. Kwa Mama, baba dada zangu, nawapenda. Jaribuni kuwa wenye furaha wakati mnaweza kufanya hivyo.Wenu awapendae Furaha.”
Matumizi ya nafsi
Mwandishi ametumia nafsi mbalimbali na hii ni mifano:
Nafsi ya kwanza umoja na wingi:Uk.28 Salim: “nilidhani sitakuona tena sijakuona muda mrefu”Uk.42 “oh huwezi kuamini jinsi tulivyojaribu”.
Nafsi ya pili:Salim : usifurahi kupita kiasiSalim: hufai kuhukumu unalala kama…..Mama Furaha: usiwe hivyo wewe u mtoto mzuri.
Nafsi ya tatu:Mama Furaha: kabla Furaha hajafa alitaka niahidi kumfanyia kitu fulani hapa kwenye mazishi ingawaje alikuwa na maumivu na mateso aliandika barua hii hapa na kunipa.
MATUMIZI YA LUGHA
Lugha aliyotumia mwandishi ni lugha fasaha na inayoleweka kwa wasomaji wake.
Matumizi ya tamathali za semi
Sitiari:Uk.2 “Waridi changa” “Ua kavu” –Mama anamfananisha Furaha na waridi au ua.Uk.4 “Nyie Mbu mlolaaniwa” –Baba Furaha anawaita wadogo zake Furaha;Uk.6 “Ua” –Furaha.Uk.25 “Slim”- UKIMWI. Wanakijiji wanaufananisha ugonjwa huu na jina hili kutokana na sifa yake ya kukondesha mwili.
Tashibiha:Uk.18 “yeye ni kama Punda wa kijiji”.Mwanakijiji wa 1 anamfananisha Furaha na Punda kutokana na tabia yake ya kuwa na wanume wengi. Malaya.Uk.13. “kisura ni kama jiji la New York…”Uk.43 “…vipande vinaanguka kama theluji”.
Mubaalagha:Uk.13 “kisura ni kama Jiji la New York ya Afrika Mashariki. Kule kuna majengoMajengo makubwa kiasi kwamba unaweza kuona mlima Kilimanjaro kwaJuu” pia anasema“Ndiyo mpenzi na Maduka… wana moja linaloitwaShoppers Plaza…! Pengine ndilo eneo kubwa lenye maduka makubwaKuliko yote katika Afrika”Uk.20 Furaha: nani aliyesema mambo hayo?Mama Furaha: Nusu ya kijiji kizima badala ya watu wengi. Mama Furahaanazidisha chumvi Kuonesha ukubwa wa hilo jambo.
Tafsida:Uk.7 maongezi kati ya wahusika;Mary: hiyo ni bia yake ya mwanzo.Furaha: ni chunguMary: ladha yake utaizoea tuBw. Juma: kama ulivyizoea wewe mayai yangu madogo!Bw. Ecko: Unaona! Inashangaza jinsi ambavyo mtu unaizoea haraka ladha hiyo!Bw. Juma:(kwa mary) kama ulivyofaanya wewe, mishikaki yangu midogo….Mazungumzo haya yamepunguza ukali wa maneno, maneno kama vile “Mishikaki” na “Mayai” ni sehemu za siri.
Mbinu nyingine za kisanaa
Mdokezo:Uk.8 “ndiyo padre….. ni …..”Uk.9 “Furaha…..fur….tuta…..”Uk.20 “ame…..tuseme…..”Uk.36 “misamaha padre mi…”Uk.44 “uepukaji….”
Nidaa:Uk.15 “Ooo!”Uk.34 “Oh!”Uk.41 “Eee”
Takriri:Uk.28 “Hapana hapana hapana nitauona!” “mpumbavu mpumbavu mimi”Uk.9 “hili ni jambo zito sana… sanasana…..sana hasa…”Uk 44 na 45 maneno haya yamerudiwa kuonesha msisitizo.Mwanakijiji wa 2: kondomMwanakijiji wa 3: elimuMwanakijiji wa 4: elimuMwanakijiji wa 1: uwaziKitunda: uadilifuPadre James: ukweliMary: upendoSalim: msamaha.
Tashtiti:Uk.20 mama Furaha: wewe na marafiki zako wa kiumeFuraha: marafiki gani wa kiume?Furaha anauliza swali ambalo majibu yake anayo ila tu anataka kuupindisha ukweli.Uk.38 baba: msalaba wako, padri. Uko shingoni mwako!Padre James: kweli?Baba: padre!Padre James: hakika?Padre James alijua wazi kuwa msalaba ulikuwa shingoni lakini kutokana na kutaka kuuficha ukweli alipokutwa katika pilika za kutafuta barua na kusingizia amedondosha msalaba. Alijifanya kuuliza kama vile hajui.
Onomatopea au tanakali sauti:Uk.33-34 “Myaau!” Uk.35 “Oooowww!”
Matumizi ya semi
Misemo:Uk.27 “Furaha anavuna mbegu ya kifo aliyopanda”
WAHUSIKA
FURAHA
Ni binti mdogo wa miaka kati ya 13-19
Ni Malaya
Anaathirika kwa ugonjwa wa UKIMWI
Alikuwa na bidii na mwenye kujituma
Ana tama
Ni mlevi
Ni mkweli na muwazi
Ni jasiri
BABA
Ni baba yake Furaha
Ni mkali
Ana upendo
MAMA FURAHA
Ni mama yake Furaha
Ni mkweli na muwazi
Ana upendo
Ni jasiri
Ni mchapakazi
Ni mpole
Ana msimamo
Anafaa kuigwa na jami
MARY
Ni binti mdogo
Ni Malaya
Si rafiki mwema
Anachangia kuharibu maisha ya Furaha
Ni mlevi
Anapenda anasa
Ana tama
Hafai kuigwa na jamii
BW. ECKO
Ni mwanaume mtu mzima
Ni Malaya
Si muaminifu katika ndoa yake
Ni mrubinifu kwa mabinti wadogo
Ni mlevi
Ni mfanyabiashara
Ni muathirika wa UKIMWI
JUMA
Ni mwanaume mtu mzima
Ni Malaya
Ni laghai kwa mabinti wadogo
Ni mlevi
Anapenda anasa
Ana tama
Ni rafiki wa Bw. Ecko
PADRI JAMES
Ni mtumishi wa Mungu katika kanisa katoliki
Si muadilifu
Anaogopa ukweli na uwazi
Ni dhaifu kwa wanawake
Anaweza kuwa ni muathirika wa UKIMWI
KITUNDA
Ni kijana wa mtaani
Anapenda anasa
Ana tama
Ni mlaghai kwa wasichana
Ni muhuni
Ni mlevi na mvuta bangi
Ana lugha ya kihuni
SALIM
Ni kijana wa kiume
Ni msomi
Ni mchumba wa Furaha
Anaweza kuwa ni muathirika wa UKIMWI
Si mkweli na muwazi
Si muadilifu
Wanakijiji 1,2 na 3
Ni wanakijiji katika kijiji cha Furaha
Hawana elimu juu ya UKIMWI
Ni wambea
Wana imani potofu
DADA MDOGO
Ni mdogo wake Furaha
Ana tabia njema
Ni mkweli lakini muoga
Hapendezwi na tabia ya dada yake
MANDHARI
Mandhari aliyotumia mwandishi ni ya vijiji vya Afrika Mashariki kwa ujumla wake. Mwandishi ametumia mandhari hii makusudi kwani imeendana na yale anayoyazungumza katika kitabu. Suala la ujinga na upotofu wa dhana kuhusu UKIMWI lipo zaidi vijijini. Wanakijiji hawaelewi juu ya UKIMWI. Mambo anayoyaibua mwandishi yanaendana na jamii ya watu wa vijiji hivyo mandhari ni sadifu.
Fani katika Tamthiliya ya Watoto wa Mama N’tiliye
Hakaiki fani katika tamthiliya ya Watoto wa Mama N’tiliye
MWANDISHI: EMMANUEL MBOGO
WACHAPISHAJI: HEKO PUBLISHERS
MWAKA: 2002
JINA LA KITABU
Jina la kitabu WATOTO WA MAMA NTILIE limesadifu yaliyomo ndani ya kitabu, kinaeleza kuhusu maisha ya watoto wa mama ntilie. Maisha ya dhiki, umaskini uliokithiri, maisha yasiyo ya faraja yaliyokosa malezi bora, chakula bora, elimu, huduma ya afya nk. Jina la kitabu linaakisi yaliyomo ndani ya kitabu na katika jamii yetu ya leo kwani akina mama wengi hawana kazi nzuri za kuwaingizia kipato kikubwa na bado wanategemewa katika malezi. Mwandishi ametumia jina hili ili kibua kero na matatizo yaliyoko katika jamii.
UTANGULIZI WA KITABU
Riwaya ya Watoto wa Mama N’tilie ni riwaya ambayo inasadifu maisha ya Mtanzania wa leo. Inaangazia suala la umaskini na hali ngumu ya maisha, wimbi la watoto wa mitaani, masuala ya uhalifu wizi na ujambazi, malezi nk. Mwandishi Mbogo amejitahidi sana. Pia katika fani ametumia muundo na mtindo wenye kuwavutia wasomaji pia kawaumba wahusika wake kwa usadifu wa hali ya juu huku mandhari yake ikiwa ni halisi inayosawiri maisha ya Tanzania.
MUUNDO
Muundo uliotawala katika riwaya hii ni muundo wa rukia au rejea. Mfano sura ya tatu mwandishi anatuelezea juu ya safari ya Mama ntilie kwenda matombo uk.34. Lakini anaacha kisa hicho ndani ya sura hiyohiyo anaanza kutuelezea juu ya kuzaliwa kwa watoto Kurwa na Doto na asili yao. Pia uk.80 mwandishi anatudokeza juu ya safari ya kwenda kwa Musa na hatuoneshi hatma ya safari yake bali anarukia kisa kingine na kuanza kutuelezea juu ya Zita kupandwa na kichaa uk.81. Vilevile uk.85-86 anatusimulia juu ya safari ya Mama Zita na Zenabu kuelekea hospitali kumwona Zita lakini hatuoneshi hatma ya safari yao bali anarukia kisa kingine na kuturudisha nyumbani kwa Mzee Lomolomo na jinsi anavyofakamia pombe alafu anaturudisha tena kutuambia juu ya kifo cha Zita hospitalini Muhimbili.
Mwandishi amegawa visa na matukio katika sura tano. Sura hizi zimejengwa katika muundo unaotegemeana ili kukamilisha kilele cha masimulizi.
MTINDO
Mtindo aliotumia mwandishi ni wa masimulizi ya mjazo au lugha ya nathari ameeleza visa mwenyewe na vingine wahusika wamevielezea. Pia ametumia mitindo kadha wa kadha. Mfano;Matumizi ya nafsi.
Nafsi ya tatu wingi na umoja:Uk.15 “Peter aliokota kipande cha muhogo” “alisafisha kipande cha muhogo”Uk.27 “walisaidiana wakaubeba” uk.26 “watu walisongamana walisukumana…..”.Kwa kiasi kikubwa matumizi ya nafsi ya tatu ndiyo yaliyotawala.
Nafsi ya kwanza umoja na wingi:Uk.58 “nitasema nitasema!”Uk.58 “njoo tuongee”Uk.56 “twende tule”.
Matumizi ya nafsi ya pili au dayalojia:Uk.89 pale Mama ntilie alipokumbuka majibizano yake na Zita.MAMA NTILIE: na hiyo nguo namna gani? Mbona chafu hivyo na leo ndio kwanza.Jumanne.PETER: mbwa Mama……ZITA: amenikwaruza kidogo na makucha yake.
Matumizi ya tanzu nyingine za kifasihi, mfano wimbo;Uk.78 “Jua ni moto,Tena ni mwangazaWa Dunia,Nadina yooNadina mama,Tumwombe Mungu Baba”Uk.10 wimbo alouimba mzee Lomolomo. “Kuleni nae,Hata bangi vuteni nae,Lakini ni kazi bure,Mwenzenu nimezaa naye,Pepepe kijani cha mbaazi,Kijaluba na msondoKiboko yao”.
Hivyo mwandishi ametumia mitindo hiyo ili kutomchosha msomaji mfano wimbo unamburudisha msomaji, majibizano yanavuta umakini zaidi na matumizi ya nafsi mbalimbali.
MATUMIZI YA LUGHA
Riwaya ya Watoto wa Mama Ntilie imetumia lugha rahisi, fasaha na inayoeleweka kwa wasomaji. Kuna matumizi ya lugha ya kiingereza mfano.Uk.36 “chloroquine”, “RosewinenaQueenElizabeth”,Uk.83 “faster faster mama” uk.1 “landrover”. Pia kuna matumizi ya lugha ya miitaaniuk.41 “kudeku…..”
Matumizi ya tamathali za semi
Tashibiha:uk.10 “mdomo wake ulio kaa kama bakuli la pombe”Uk.12 “mama ntilie alikaa kama kapigwa na radi”Uk.15 “miguu kama ya mamba”Uk.46 “aliinamisha shingo nayo ikapinda kama mforosadi” “kichwa kama stafeli”Uk.40. “kitovu chake kama jicho chongo”Uk.23 “Kurwa aliruka nyuma kama Chui”Uk.45 “akaruka kama Paa”
Tashihisi:Uk. 10 “mabega yenyewe tayari yalikuwa yamechongwa kwa pombe ya gongo.Yameangalia juu karibu yakutane na masikio”Uk.17 “aliziona nywele za kipilipili za Musa ngumu kama katani hazijaonja maji walasabuni”Uk.19 “ moshi wenye harufu ya kuudhi ulilelea hewani na kumlaki mtoto Peter.”Uk.35 “…… visogo vitatu vilikata kona na kupotea”Uk.46 “koo lilimsaliti”Uk.40 “miguuni raba zinazocheka kwa huzuni”Uk.46 “mlango ule wa kuungwa na gundi ulitika labeka”
Sitiari:Uk.10 “Nyama nyie”Uk.86 “…… wakatembea mwendo wa Farasi”
Ritifaa:Uk.38 “Mama? Mama yuko wapi, Baba yuko wapi? Mapenzi yao yako wapi?”Uk.92 “Zita! Zita! Zita! Zita umekwenda! Umenitoroka, Zita mwanangu”Uk.93 “Baba! Baba watoto? Mwenzangu! Ee! Amka, simama! Usiniachie tanzia hii peke Yangu”
Tafsida:Uk.91 “haja kubwa”
Matumizi ya mbinu nyingine za kisanaa
Onomatopea /tanakali sauti:Uk.5 “….. aliupinda mgongo kwa mbele akausikia unalia ka-ka-ka-ka, alitema mate tena Phuuuu”Uk.11 “alikohoa ukho! okho!”Uk.19 “…. Kwa kupiga chafya mbili au tatu Tcha! Tcha! Tcha!”Uk.50 “Bwee! Bwee! Bwee! Mbwa ….”Uk.50 “Hali … vicheko Woo! Woo! Weee! Weee! Heheheee! Leooo!”
Takriri:Uk.12 “twende! Twende! Nakuwacha nakauwacha!”Uk.58 “ Nivione! Nivione! Nivione vya kazi gani!”Uk.60 “ Nipishe! Nipishe! Nipishe!Uk.61 “kukurukakara, kukurukakara,kukurkakara”Uk.91 “ Baba! Baba! amka Baba”
Mjalizo:Uk. 40 “… akapata pesa, akala, akashiba”
Mdokezo:Uk.58 “usiseme hivyo! Unasikia ee! Usi……”Uk.71mara akaanza kuimba tena uleule wimbo wake wa “siwezi kuuwa mtu mama”Uk.73 “lakini…….”Uk.79 “ alikumbuka jaa laa jiji na ………”
Nidaa:Uk.44 “ Oh! Mungu wangu!”Uk.91 “ Mama wee!”Uk.90 “Hamadi! Mtume!”
Matumizi ya semi
Nahau:Uk.43 “…. Kupiga usingizi”
Methali:Uk.34 “ kamba hukatikia pembamba”Uk. 69 “fadhila za Punda”
Misemo:Uk.35 “ mtu wa maji” – mlevi.Uk.13 “kwake pombe ya mataputapu na gongo alivifanya dini”.
Matumizi ya taswira
Taswira mwonekano mfano:Uk.1 “ Mbwa huyu mweusi mwenye mkia mweupe, alionekana akitembea mwendo wa polepole. Ulimi wake mrefu ulionekana ukidondoka mate ya utelezi” hii inatufanya tupate picha halisi ya jinsi Mbwa huyo alivyo kupitia maneno ya msanii”.Uk.5 “….. hatua tatu mbele yake Sufuria, Vikombe na Sahani chafu zilizagaa pale nje zikimtazama. Akawaona nzi wakitembea na kurukaruka juu ya vyombo vichafu.Uk.10 “ mabega yenyewe tayari yalikuwa yamechonngoka kwa pombe ya gongo yameangalia juu karibu yakutane na masikio.”Uk.69 “Zenabu alibaki pale mlangoni kavaa gauni aina ya shifti, kitambaa cha Hariri”
Taswira hisi:Uk.91 “ Mzee Lomolomo alilala mdomo wazi Nzi wakubwa wa kijani kibichi wamejaa tele mdomoni mwake”.Hii inamfanya msomaji ajisikie kinyaa kutokana na hali hiyo ya Mzee Lomolomo anaposema nzi wa kijani kibichi, kwani hao ni nzi wanaokaa sana chooni na kwenye uchafu.
WAHUSIKA
Mama Ntilie
Ni mama mzazi wa Peter na Zita
Ni mke wa Mzee Lomolomo
Mlezi mzuri wa familia
Ni mvumilivu sana
Ana huruma
Ni mchapakazi na anayejituma
Ana hali ngumu kimaisha
Mzee Lomolomo
Ni mme wa mama ntilie
Baba wa Peter na Zita
Mlevi
Mvivu
Si mlezi bora hajali familia
Anakufa kwa sababu ya kunywa sana pombe
Peter
Mtoto wa mama ntilie
Anakosa elimu kwa sababu ya umaskini
Ana bidii na mchapakazi
Ana huruma
Anafungwa jela sababu ya kufanya biashara haramu ya madawa ya kulevya
Zita
Mtoto wa kike wa mama ntilie
Anakosa elimu sababu ya umaskini
Ni mchapakazi
Anagombana na Kurwa hakupenda aje kwao, roho mbaya
Anakufa kwa ugonjwa wa kichaa cha mbwa
Doto
Ni mtoto yatima
Mtoto wa mtaani
Doto anauawa baada ya kujiingiza katika uhalifu wa wizi
Ni mgomvi na katili
Kurwa
Ni ndugu yake Doto
Anaishi mtaani
Ni yatima
Ana huruma
Ana nguvu na jasiri
Ni mchapakazi
Anaishia jela kwa sababu ya makosa ya Musa na Peter
Musa
Ni mtoto aliyekosa elimu baada ya kukosa sare na ada
Alikosa malezi mazuri ya wazazi
Mhalifu, anafanya biashara haramu za madawa ya kulevya
Ana tamaa ya pesa
Ni rafiki mbaya kwani alimshauri Peter kuuza madawa ya kulevya
Mwalimu Chikoya
Ni mwalimu wa akina Peter na Zita
Aliwafukuza Peter na Zita shule sababu ya kukosa ada
Si mwalimu mzuri
MANDHARI
Mandhari iliyotumika katika riwaya hii ni mandhari ya jiji la Dar es Salaam. Hii ni kutokana na kutajwa kwa maeneo ya jiji mfano, Manzese, Tabata, Kiwanda cha Urafiki, Kisutu, Muhimbili nk. Pia ametumia mandhari ya nyumbani mfano nyumbani kwa Mama Ntilie uk.5, mandhari ya hospitali ya Muhimbili uk.89, mandhari ya jaani-jaa la Tabata uk.20.
Kwa hiyo mwandishi ametumia mandhari inayosadifu aliyoyaeleza anaibua dhamira halisi zinazosawiri maisha ya Mtanzania wa leo kwa mandhari hiyo mfano suala la umaskini na wimbi la watoto wa mitaani.

Uhakiki wa fani katika Ushairi
Fani katika Ushairi wa Wasakatonge
Hakiki fani katika Ushairi wa Wasakatonge
MWANDISHI: TAASISI YA KISWAHILI, ZANZIBAR
WACHAPISHAJI: OXFORD UNIVERSITY PRESS
MWAKA: 2001
JINA LA KITABU
Jina la kitabu linasadifu yaliyomo katika kitabu. Kwa upande wa maudhui mambo yanayoelezwa mengi yanaigusa jamii ya sasa. Masuala ya maadili, siasa, uchumi, ukombozi wa kiutamaduni changamoto na suluhisho ya matatizo yanayoikumba jamii yanaendana na wakati wa sasa. Hivyo upya wa malenga wapya ni kweli. Kifani pia Malenga wapya wameweka muundo na mtindo wa kisasa.
MUUNDO
Tunapohakiki muundo katika ushairi tunaangalia idadi ya mistari katika ubeti. Ubeti huweza kuwa na mistari miwili, mitatu, minne na kuendelea. Aina za muundo zimepewa istilahi maalum kuutofautisha aina moja na nyingine mfano mashiri yenye mistari miwili katika ubeti ni Tathnia. Imetumika miundo tofautitofauti katika diwani hii. Mfano:
Tathlitha:Haya ni mashairi ambayo yana mistari mitatu kwa kila beti, mengi ya mashairi haya ni ya kisasa. Mfano ni shairi la“Hali halisi”, “Puuzo”, “Ua”, “Kuunge”, “Tunzo”.Shairi la Ua.“Ua limejituliza mtini laning’inia,Mwenyewe laniliwaza, furahani lanitia, Ua sasa limepea, macho walikodolea.”
Tarbia:Haya ni mashairi yenye mistari mine. Mfano ni shairi la“Kitendawili”, “Mkulima”, “Majonzi”, “Bahari”, “Samaki mtungoni” “Kifungo”,na mengine mengi.Shairi la“Kifungo.” “Miaka imeshapita, sasa najiamkia,Naanza bila kusita, bahati kujitafutia,Hapo nitapoipata, mola jishukuria,Kifungo kimenichosha, minyororo nafungua.
Takhmisa:Haya huwa na muundo wa mistari mitano katika kila ubeti. Mfano ni mashairi ya“Siharakie maisha”, na “Israfu”.Shairi la“Israfu”. “Mali ulojichumia,Ni yako nakubalia,Lakini kiangalia,Vipi unaitumia,Mwenzangu nakuusia israfu haifai.”
Sabilia:Haya ni mashairi yenye mistari kuanzia sita na kuendelea. Mfano ni shairi la“Punda”na “Pasua uwape ukweli”.Shairi la“Punda”. “Toka ulipozaliwa, maishayo ni kizogo,Hujapata kuenziwa, waishi tiriigivyogo,Nawe hujajielewa, u kiumbe hu kigogo,Kama ungefadhiliwa, usingebeba mzigo, Hakika ulionewa, hustahili kipigo,Haki umeitambua, idadi japo kidogo.”
MTINDO
Imetumika mitindo ya aina zote mbili. Kwanza wametumia mtindo wa kisasa. Huu ni mtindo ambao haufuati kanuni za urari wa vina na mizani katika beti pia huitwa mashairi huru. Mtindo mwingine ni mtindo wa kimapokeo, huu hufuata kanuni na sheria zote za vina na mizani katika utunzi wake. Mara nyingi huwa na mistari minne katika kila ubeti.
Mfano wa mashairi yaliyotumia mtindo wa kisasa ni mashairi ya“Pasua uwape ukweli”, “Haki” “Payuka

Pia mfano wa mashairi ya kimapokeo ni shairi la“Mkulima”, “Bahari”, “Tuyazingatie haya” “Nipate wapi mwingine”.
MATUMIZI YA LUGHA
Diwani ya malenga wapya imetumia lugha yenye ubunifu bora wa kisanaa.Vilevile ni lugha rahisi na sanifu inayoeleweka kwa hadhira lengwa.
Tamathali za Semi
Tashibiha:“Nizikwe kama wezangu, nisitupwe kama paka” -Shairi la“Nini wanangu”.“Hata pamoja muweko, ubaguzi umezama,kama nguzo” -Shairi la“Tunzo ubeti wa nne”.“Mfanowe kama radi, chini inapoanguka”.-Shairi la“Nipate wapi mwingine”.“Nikabaki kama ng’onda” -Shairi la“Nipatieni dawa”.“Maisha ni kama njia”-Shairi la“Maisha ni kama njia”.“Yameotewa na kombe, mithili gome la mti”-Shairi la“Bahari ubeti wa pili”.
Tashihisi:“Ewe ulimi sikia” -Shairi la“Ulimi”.“Haki wa tutisha,tusikuandame,kwa matendo yetu” –Shairi la“Haki ubeti wa kwanza”.“Njiwa ameishanitoka, nipate wapi mwingine”-Shairi la“Nipate wapi mwingine”.“Samaki wasikitika, kudai walikotoka, Wote wamekasirika, uhuru wanachotaka,”-Shairi la“samaki mtungoni”.
Sitiari:“wamejipa uwezo wa Rabuka” – “Mpaka lini”“Paka shume jigeuza” – “Kwanini?”“mshumaa ” – “Hali halisi”
Mbinu nyingine za kisanaa
Onomatopea/ tanakali sauti:“kokoriko”- “Mkulima”“Parakacha” – “kwanini”.
Takriri:“Charuka” – “charuka”
Tashititi:“Nasikia mnatunga mwatungani washairi?” “mwabwaja mwasema nini”
Matumizi ya semi
Methali:“Simwamshe asilani aliyelala usingizini” – “Payuka”“Fahali wapiganapo, nyasi ndio huumia”- “Sokomoko baharini”“Subira yavuta heri”- “Siharakie maisha”
Matumizi ya taswira
“Samaki” – wanyonge – “samaki mtungoni”
“Ua” – mpenzi – “Ua”
“Punda”-wanyonge – “Punda”
“Mvuvi” – wanyonyaji – “Samaki mtungoni”
“Njiwa” – mpenzi – “Nipate wapi mwingine”
“Baharini” – nchi – “Sokomoko”
“Abiria”- wananchi –“Sokomoko”

Fani katika Ushairi wa Mashairi ya Chekacheka
Hakiki fani katika Ushairi wa Mashairi ya Chekacheka
MWANDISHI: THEOBALD A. MVUNGI
WACHAPISHAJI: EDUCATIONAL PUBLISHERS AND DISTRIBUTORS LTD.
MWAKA: 1995
MUUNDO
Mwandishi ametumia muundo wa tarbia, mashairi yake yote yamefuata muundo huu. Beti za mashairi yake zina mistari minne. Mengi ya mashairi yake, mistari imegawanyika katika vipande viwili yaani mistari ina vina vya kati na vya mwisho. Mfano katika shairi la “Mashairi ya “Ngulu”;

Pia katika baadhi ya mashairi yake ameyaumba katika kipande kimoja, yaani yana kina cha mwisho tu. Mfano ni mashairi kama vile ya“Dhahabu ya fahari”, “Utu umekuwa kima”,“Seng’enge”mfano katika shairi la“Utu umekuwa kima”

MTINDO
Mtindo aliotumia mwandishi ni mtindo wa kimapokeo kwani amezingatia vigezo vya vina na mizani katika utunzi wa mashairi yake. Mfano katika shairi la”“Tuambae ukasuku”

MATUMIZI YA LUGHA
Tashibiha:“Mshairi jihadhari, usishikwe kama fimbo.” – “Tuambae ukasuku.”“Na wasiothaminiwa, wapimwao kama nyasi”- “Raia si mali kitu”“Mapenzi yasinadiwe, kama shati dukani” – “Penzi lisilo heshima”“Utaliwa kama pumba” – “Utaliwa kama pumba”“Kaburu si mtu hata, kwake sisi sawa punda” – “Utumwa huru”.“Pungufu akili yake, mla punje kama kuku” – “Tuambaeukasuku”
Tashihisi:“Mejaribu kujongea, ndege awe mkononi,Yeye juu hurukia, namuomba samahani.” – “Njiwa kiumbe mtini”“Moyo nimeshauri, lakini umekaidiMoyo kiburi hatari, mfanowe kama radiMoyo mefumbata shari, unayakwepa marudi,Moyo u mwilini mwangu, jirudi tuwe pamoja.” – “Moyo”Nipishe wewe senge’nge” – “Seng’enge”.“Kijiji kisichoringa” – “Mashairi ya Ngulu”.“Akili yamsaliti, kikongwe haoni kweli.”- “ Ni wapi ushauri?”
Sitiari:“Mshairi awe Nyati”- “Tuambae ukasuku”“Sisi ni miamba gogo”- “Raia si mali kitu”“Ile chai kikombeni, rangi yake Mwafrika” – “Chai”.“Kwetu ulikuwa mama” – “Indira”“Utu umekuwa kima” – “Utu umekuwa kima”“Uroho umekujaa, watu mefanya kondoo” – “Utaliwa kama pumba”
Matumizi ya semi
Misemo:“Fedha fedheha” – “Chanzo cha huo uozo”
Methali:“Akishaoza samaki, busara ni kumtupa” – “Chatu mmeza matonge”
Nahau:“Wabunge waote meno, wasivilambe viatu” –wawe na mamlaka– “Tuambae ukasuku”Mbinu nyingine za kisanaa
Takriri:“Chai ninaipa hati, kwa kutukidhia haja,Chai imewekwa kati, kwetu sisi sote waja,Chai majani ya miti, hii miti yenye tija.” – “Chai”Neno“njiwa” limejirudia katika kila ubeti –“Njiwa”Neno “moyo” limerudiwa katika kila ubeti. – “Moyo”Neno “mauti” limejirudia katika ubeti wa kwanza – “Utaliwakamapumba”Neno “Ngulu” katika mashairi ya “Ngulu”.
Ujenzi wa Taswira
“Matonge”- madaraka-“Mwinyi umewasha moto”“Nyati”– watawala –“Tuambae ukasuku”“Mfugaji”– mwananchi – “Tuambae ukasuku”“Jiko”– madaraka “Kuna nini huko jikoni”“Chatu”– watawala –“Chatu mmeza matonge”“Chura”– mtu asiye na msimamo - “Chura umegundulika”
Fani katika Ushairi wa Malenga Wapya
Hakiki Fani katika Ushairi wa Malenga Wapya
MWANDISHI: TAASISI YA KISWAHILI, ZANZIBAR
WACHAPISHAJI: OXFORD UNIVERSITY PRESS
MWAKA: 2001
JINA LA KITABU
Jina la kitabu linasadifu yaliyomo katika kitabu. Kwa upande wa maudhui mambo yanayoelezwa mengi yanaigusa jamii ya sasa. Masuala ya maadili, siasa, uchumi, ukombozi wa kiutamaduni changamoto na suluhisho ya matatizo yanayoikumba jamii yanaendana na wakati wa sasa. Hivyo upya wa malenga wapya ni kweli. Kifani pia Malenga wapya wameweka muundo na mtindo wa kisasa.
MUUNDO
Tunapohakiki muundo katika ushairi tunaangalia idadi ya mistari katika ubeti. Ubeti huweza kuwa na mistari miwili, mitatu, minne na kuendelea. Aina za muundo zimepewa istilahi maalum kuutofautisha aina moja na nyingine mfano mashiri yenye mistari miwili katika ubeti ni Tathnia. Imetumika miundo tofautitofauti katika diwani hii. Mfano:
Tathlitha
Haya ni mashairi ambayo yana mistari mitatu kwa kila beti, mengi ya mashairi haya ni ya kisasa. Mfano ni shairi la“Hali halisi”, “Puuzo”, “Ua”, “Kuunge”, “Tunzo”.

Tarbia
Haya ni mashairi yenye mistari mine. Mfano ni shairi la“Kitendawili”, “Mkulima”, “Majonzi”, “Bahari”, “Samaki mtungoni” “Kifungo”,na mengine mengi.

Takhmisa
Haya huwa na muundo wa mistari mitano katika kila ubeti. Mfano ni mashairi ya“Siharakie maisha”, na “Israfu”.

Sabilia
Haya ni mashairi yenye mistari kuanzia sita na kuendelea. Mfano ni shairi la“Punda”na “Pasua uwape ukweli”

MTINDO
Imetumika mitindo ya aina zote mbili. Kwanza wametumia mtindo wa kisasa. Huu ni mtindo ambao haufuati kanuni za urari wa vina na mizani katika beti pia huitwa mashairi huru. Mtindo mwingine ni mtindo wa kimapokeo, huu hufuata kanuni na sheria zote za vina na mizani katika utunzi wake. Mara nyingi huwa na mistari minne katika kila ubeti.
Mfano wa mashairi yaliyotumia mtindo wa kisasa ni mashairi ya“Pasua uwape ukweli”, “Haki”. “Payuka”. Mfano shairi la Pasua uwape ukweli

Pia mfano wa mashairi ya kimapokeo ni shairi la“Mkulima”, “Bahari”, “Tuyazingatie haya” “Nipate wapi mwingine”.
MATUMIZI YA LUGHA
Diwani ya malenga wapya imetumia lugha yenye ubunifu bora wa kisanaa.Vilevile ni lugha rahisi na sanifu inayoeleweka kwa hadhira lengwa.
TAMATHALI ZA SEMI
Tashibiha:“Nizikwe kama wezangu, nisitupwe kama paka” -Shairi la“Nini wanangu”.“Hata pamoja muweko, ubaguzi umezama,kama nguzo” -Shairi la“Tunzo ubeti wa nne”.“Mfanowe kama radi, chini inapoanguka”.-Shairi la“Nipate wapi mwingine”.“Nikabaki kama ng’onda” -Shairi la“Nipatieni dawa”.“Maisha ni kama njia”-Shairi la“Maisha ni kama njia”.“Yameotewa na kombe, mithili gome la mti”-Shairi la“Bahari ubeti wa pili”.
Tashihisi:“Ewe ulimi sikia” -Shairi la“Ulimi”.“Haki wa tutisha,tusikuandame,kwa matendo yetu” –Shairi la“Haki ubeti wa kwanza”.“Njiwa ameishanitoka, nipate wapi mwingine”-Shairi la“Nipate wapi mwingine”.“Samaki wasikitika, kudai walikotoka, Wote wamekasirika, uhuru wanachotaka,”-Shairi la“samaki mtungoni”.
Sitiari:“wamejipa uwezo wa Rabuka” – “Mpaka lini”“Paka shume jigeuza” – “Kwanini?”“mshumaa ” – “Hali halisi”Mbinu nyingine za kisanaa.
Onomatopea/ tanakali sauti:“kokoriko”- “Mkulima”“Parakacha” – “kwanini”.
Takriri:“Charuka” – “charuka”
Tashititi:“Nasikia mnatunga mwatungani washairi?” “mwabwaja mwasema nini”Matumizi ya semi
Methali:“Simwamshe asilani aliyelala usingizini” – “Payuka”“Fahali wapiganapo, nyasi ndio huumia”- “Sokomoko baharini”“Subira yavuta heri”- “Siharakie maisha”
Taswira:Matumizi ya taswira“Samaki” – wanyonge – “samaki mtungoni”“Ua” – mpenzi – “Ua”“Punda”-wanyonge – “Punda”“Mvuvi” – wanyonyaji – “Samaki mtungoni”“Njiwa” – mpenzi – “Nipate wapi mwingine”“Baharini” – nchi – “Sokomoko”;“Abiria”- wananchi –“Sokomoko”

Uhakiki wa Maudhui katika Kazi za Fasihi Andishi
Maudhui katika riwaya ya Takadini
Hakiki Maudhui katika riwaya ya Takadini
DHAMIRA
Suala la imani potofu na ushirikina:Wanakijiji wa kijiji cha Sekai na wanakijiji wa kijiji cha Mtemi Makwati, wana imani potofu juu ya binadamu aliye na ulemavu wa ngozi yaani albino “sope” wanaamini kuwa kuzaliwa kwa mtoto wa aina hiyo ni laana na hapaswi kabisa kuishi. Hawaamini kuwa ni binadamu wa kawaida. Mfano uk.8Ambuya Shungu anasema“mtoto ni Musope.Ni wajibu wetu kumuharibu”.Mwandishi amelionesha suala hili makusudi ili jamii iweze kupinga na kuacha mila hizi potofu mara moja! Anaiasa jamii kuwapenda, kuwajali na kuwasaidia watu wenye ulemavu wa ngozi na si hivyo tu bali pia anaona upo umuhimu wa jamii kuwapa nafasi watu wa aina hiyo kwani wanaweza kuwa na umuhimu mkubwa na mchango katika jamii.
Ubaguzi kwa watu wenye ulemavu:Hii ni dhamira nyingine ambayo imejadiliwa ndani ya riwaya hii. Mwandishi anaonesha kuwa ubaguzi si mzuri kwani huwafanya watu wenye ulemavu wa ngozi wajisikie vibaya na kujiona si sehemu ya jamii wanayoishi. Tunaona jinsi Nhamoalivyombagua nakumtenga Takadini, uk. 62 “huwezi kukimbia na huwezi kupigana…..tena hata huoni vizuri. Ha! Wala hufanani hata na mmoja kati yetu, watu wanasema una laana, sitaki kuwa rafiki yako....anaendeleakumwambia“wewe ni sope, sope, sope!”kumbe tunapaswa kuwapenda na kuwajali watu wote bila ubaguzi.
Ndoa za mitara:Wanaume wa kijiji cha Sekai wana desturi ya kuoa mke zaidi ya mmoja. Mfano Makwati alikuwa na wake wanne ambao ni Sekai, Pindai, Dadirai na Rumbdzai. Wake hawa si wote walipendana bali walijitenga na kuoneana wivu mfano Dadirai na Rumbdzai hawakumpenda kabisa Sekai walimsimanga na kumsengenya. Mfano uk.15 Dadirai alisema kwa chuki “lazima atimuliwe hapa…. arudi kwao” “Ha! Atimuliwe tena? Ni mchawi!”hivyotunaona kuwa ndoa za mitara ni tatizo katika jamii kwani huweza kusababisha migogoro na ugomvi tena huweza kusababisha hata kuambukizana magonjwa hatari hasa katika kizazi cha leo ambapo magonjwa ni mengi ya hatari.
Mapenzi ya dhati na huruma:Mzee Chivero ni mzee aliyeonesha mapenzi ya dhati kwa Sekai na mwanae kwani aliwapokea na kuishi nao, pamoja na hali waliyokuwa nayo bila kuwabagua. Alimhurumia Takadini akampenda, kumsaidia na kumshauri vyema siku zote. Pia tunaona Sekai alikuwa na mapenzi ya dhati kwa mwanae Takadini kwani aliweza kumkinga na kumuokoa asiuawe. Mfano uk.10 Sekai anasema“hapana Ambuya mtoto lazima aishi. Hapana Ambuya mtoto ni wangu na sitamwachia mtu”…… sitamwachia mtu yeyote mwanangu”.
Nafasi ya mwanamke
Mwanamke amechorwa katika nafasi mbalimbali katika riwaya hii kukamilisha ujumbe wa mwandishi kwa jamii kuhusu wanawake.
Mwanamke amechorwa kama kiumbe jasiri: Sekai ameonekana kuwa na ujasiri wa hali ya juu kwani aliamua kupingana na mila za jamii yake na kuamua kutoroka na kitoto bila kujua alipoelekea ili tu kumuokoa mwanae. Hivo anapaswa kuigwa na jamii.
Amechorwa kama mwanamapinduzi:Sekai na Shingai wamechorwa kama wanawake wanamapinduzi kwa kuubadilisha mtazamo wa wanajamii wenzao kuhusu baadhi ya mila potofu. Mfano Shingai aliamua kuolewa na Takadini bila kujali ulemavu wake. Hakuogopa wazazi wake wala hakuogopwa kutengwa na ndipo badae jamii ilimkubali. Pia Sekai ni mwanamapinduzi kwa kuzikataa mila potofu ya kuwaua albino, alimtunza mwanae na kumlea mapaka akakua.
Amechorwa kama chombo cha starehe: Mwanamke katika jamii hizi alionekana kama chombo cha starehe tu kwani waliolewa wanawake wengi kwa mwanaume mmoja na lengo nikumburudisha tu na kumzalia watoto.
Amechorwa kama kiumbe dhaifu asiyeweza kusema chochote wala haki yoyote: Wazazi wa Shingai hawakumpa kabisa Shingai uhuru wa kuchagua mwanaume aliyempenda. Walimlazimisha kuolewa na mwanaume waliyemtaka. Mfano uk.118 Shingai anasema“huyu ndiye mtu ninayeteka anioe. Hakuna aliyeniuliza kama nampenda Nhamo. Wewe na baba mlikuwa na hamu ya kuniozesha katika familia ya Manyamombe hata matakwa yangu hayakusikilizwa. Sasa nimechagua”.
Amechorwa kama mtu mwenye mapenzi ya dhati: Sekai alikuwa na mapenzi ya dhati kwa mwanae Takadini. Pia Shingai alikuwa na mapenzi ya dhati kwa Takadini na hata kuamua kuolewa naye.
Amechorwa kama mtu mvumilivu: Mfano mzuri ni Sekai alivumilia kwa muda mrefu bila kukata tamaa kukosa uzazi, masimango ya wake wenzake na hatimaye alipata mtoto. Pia alivumilia kumlea Takadini wala hakuthubutu kumtenga hata mara moja bali alimvumilia mpaka alipokua.
MIGOGORO
Mgogoro kati ya Sekai na Rumbdzai na Dadirai: Sababu ya mgogoro huu ni kwamba, wanawake hawa wawili hawakumpenda kabisa Sekai na walimuonea wivu kwa kitendo cha kupendwa sana mumewe. Walimsimanga na kumsengenya muda mwingi na hasa kutokana na tatizo la Sekai la kukosa mtoto kwa muda mrefu. Walimwita mchawi.
Mgogoro kati ya Sekai na Makwati mumewe:Sababu ya mgogoro huu ni Sekai kujifungua mtoto mwenye ulemavu wa ngozi ambapo katika jamii yao ni laana. Mumewe hakumwamini alimgombeza na kumtishia kumuua akidhani Sekai ni mchawi. Sekai na mwanae anaamua kutoroka ili kuondokana adha ile.
Mgogoro kati ya Nhamo na Takadini:Sababuni kuwa Nhamo alimpiga na kumdhalilisha Takadini mara kwa mara mbele ya vijana wengine kwakuwa ni Sope. Alimkejeli na kumdhihaki mfanouk.62 “wewe ni sope umelaaniwa”Nhamo alimwambia Takadini. Pia sababu nyingine ni kutokana na Shingai mchumba wa Nhamo kuwa na mapenzi ya dhati kwa Takadini na kumkataa yeye. Takadini alivumilia na kutolipiza kisasi na baadae alifanikiwa kumuoa Shingai na kuzaa naye mtoto wa kiume.
Mgogoro kati ya Nhariswa na mkewe:Nhariswa alimpiga na kumgombeza mkewe kwa kitendo cha kutomfuatilia binti yao na kumwacha aanzishe uhusiano na kijana aliyeaminiwa kuwa amelaaniwa.
Mgogoro kati ya Shingai na mama yake:Mgogoro huu ulitokana na Shingai kuamua kuolewa na Takadini jambo ambalo hawakulitaka kabisa kutokana na hali ya Takadini. Mama yake anaamua kumkana Shingai hadharani kuwa si mtoto wake tena.
Mgogoro kati ya Nhamo na Tapfumaneyi.Vijana hawa walipigana ili kumtafuta mshindi na shujaa bingwa wa mapigano. Vijana walipigana sawia na walitoka sawia.
Mgogoro wa nafsi kwa Sekai.Sekai alisumbuliwa na mgogoro wa nafsi kwa muda mrefu juu ya mwanae ambaye alitengwa na kubezwa kutokana na hali yake. Alilia na kuhuzunika mara nyingi akiilaumu Miungu yao kuwa “Sisi tumefanya nini” hatimaye mgogoro wake uliisha baada ya Takadini kujenga heshima yake upya mara alipomuoa Shingai na kubahatika kupata mtoto wa kiume tena asiye Sope. Na hapo ndipo ilirejea faraja na furaha mpya.
Mgogoro wa nafsi kwa Takadini:Huu ulisababishwa na hali yake ya ulemavu wa ngozi iliyopelekea yeye kutengwa na kubaguliwa na wanajamii na mara kadhaa kutishiwa kuuawa. Hali hii ilimtesa ka muda mrefu kwani alitengwa na hakuwa na rafiki toka utotoni hadi ujana wake. Lakini mgogoro huu unaisha baada ya kupata mke aliyempenda kwa dhati na kumzalia mtoto wa kiume. Hii inampa faraja na kujiona mwanaume halisi na kuithibitishia jamii kuwa alikuwa sawa na wanajamii wengine.
FALSAFA:Falsafa ya mwandishi Ben Hanson, anaamini kwamba watu wenye ulemavu wa ngozi wana haki ya kuishi kama binadamu wengine kwani wana akili, utashi, uwezo wa kufanya kazi kama binadamu wengine na ni sawa na binadamu wengine.Wao kuwa na ulemavu wa ngozi si kigezo cha kuwaua na kuwabagua. Hana imani juu ya mila potofu kwani katika masimulizi yake anaonesha kushindwa kwa mila potofu kama vile kuamini kuwa albino ni viumbe waliolaaniwa na hawatakiwi kuishi. Anaamini kuwa wakipewa nafasi ya kuishi na kushirikishwa katika shughuli za kijamii, kupewa elimu na mahitaji yote wanaweza kuwa ni watu muhimu sana katika jamii na hili analidhihirisha kupitia Takadini.
MTAZAMO:Mtazamo wa mwandishi ni wa kiyakinifu. Tunaweza kusema hivyo kwa sababu ya mambo ambayo mwandishi anayamulika katika kazi yake. Mambo kama vile kuzaliwa kwa albino haoni kuwa ni laana bali ni kawaida tukutokana na masuala tu ya kimaumbile. Haoni kuwa kuna haja ya kuwatenga au kuwabagua albino kwakuwa ni binadamu sawa na sisi.
MSIMAMO:Msimamo wa mwandishi ni wa kimapinduzi kwani analenga kuyapindua mawazo na imani potofu za baadhi ya jamii kuwa albino hafai kuishi. Anakemea suala la kuwatenga na kuwabagua albino, anakemea pia suala la ndoa za lazima na mila zingine potofu. Anataka jamii ibadilike na kuendana na wakati kuwapa usawa watu walio na ulemavu wa ngozi, anatetea haki za wanawake anataka wapewe nafasi sawa katika jamii wasibaguliwe. Hivyo msimamo wa mwandishi ni mzuri na unatakiwa kufanyiwa kazi katika jamii.
UJUMBE
Albino au watu wenye ulemavu wa ngozi wanatakiwa kupewa haki ya kuishi, kupendwa kusaidiwa na kulindwa.
Mila na desturi potofu si budi kupigwa vita katika jamii.
Upendo na huruma ni mambo ya msingi katika jamii.
Wanawake wapewe uhuru wa kuchagua wanaume wanaowapenda kuishi nao katika ndoa.
Wanawake wapewe nafasi na kushirikishwa katika masuala ya jamii.
Maudhui katika Riwaya ya Joka la Mdimu
Hakiki maudhui katika Riwaya ya Joka la Mdimu
DHAMIRA
Ugumu na hali ngumu ya maisha:Suala la ugumu wa maisha limejadiliwa katika riwaya hii kwa kiasi chake. Mwandishi ameonesha jinsi wananchi wanavyopata shida ya vyakula, mavazi nk. Yote haya yakisababishwa na mfumuko wa bei za bidhaa kutokana na uhaba wa bidhaa. Mfano. Uk.1“jiji la Mindule lilikabiliwa na uhaba mkubwa mno wa petroli, dezeli na mafuta ya taa nyumba nyingi zisizo na umeme zilibaki kiza usiku maana mishumaa ilikuwa ghali na adimu kupatikana, usafiri ulisimama isipokuwa kwa wale wachache waliojua mbinu za kupata dizeli na petrol”.Mwandishi ameonesha jambo hili ambalo linaakisi maisha ya hali ya kiuchumi miaka ya 80, ambayo kwa upande mwingine inaangazia maisha ya mtanzania wa leo ambapo bidhaa ni nyingi maasokoni lakini tatizo ikiwa ni mfumuko wa bei na upatikanaji mgumu wa fedha.
Suala la utabaka:Utabaka uliojadiliwa ni kati ya walionacho na wasionacho (matajiri na maskini). Hili limeoneshwa pale ambapo wananchi wanaishi maisha ya dhiki na makazi duni mfano uk.29 mwandishi anaeleza,“nyumba yenyewe ya Tino ilikuwa bondeni juu tu kidogo ya mtaro mkubwa uliokuwa ukipitisha maji machafu”.Hii inatuonesha wazi hali mbaya ya makazi ya Tino na wakazi wengine, wakati hawa maskini wakiteseka na kuhangaika hata katika suala la huduma za kijamii kama matibabu ya gharama kubwa, matajiri wao walinufaika kwa kuwa na fedha nyingi, mali za kujilikimbikizia na za magendo. Mfano uk. 103 – 104 mwandishi anaeleza kuhusu makazi au nyumba ya Brown“ilisimama na kuzibeza nyumba zote jirani na hapo kwa haiba yake na bwawa lake la kuogelea”.
Ufisadi: Suala la ufisadi limeoneshwa na mwandishi kwani amejadili kuhusu viongozi ambao wanahujumu mali za umma kwa maslahi yao binafsi, viongozi mfano wafanyakazi wa serikali kama vile Brown Kwacha amechorwa kuwa ni mtumiaji mbaya wa mali za umma, anasafiri safari za nje kwa pesa nyingi za serikali na kwa matumizi binafsi. Licha ya hivyo anafanya biashara ya magendo na pesa za kigeni katika ofisi yake. Alimudu kujenga nyumba za kifahari kwa pesa za serikali. Mfanouk.102“gharama ya nyumba iliyokuwa ikijengwa na Wafaransa ilikuwa shilingi milioni mia mbili na nusu na ile nyingine milioni mia tatu”.Hizi ni pesa nyingi ambazo zote alizichukua serikalini.Hili ni tatizo kubwa kwa jamii yetu ya leo. Viongozi wetu wa serkali wanatumia pesa vibaya za serikali kwa manufaa binafsi, hivyo kusababisha umaskini usioisha kwa Watanzania wa hali ya chini. Mwandishi amelionesha hili ili wanaohusika wabadilike.
Biashara haramu na uharibifu wa mali za taifa:Suala hili limejadiliwa katika riwaya hii. Mhusika Brown ambaye ni mfanyakazi wa serikali anajihusisha na biashara za magendo mfano uuzaji na uwindaji wa wanyama na kuchukua pembe, ngozi na meno. Mfano uk.122-123 muwindaji kinara wa Brown anasema“sawa ziko pembe ishirini za faru na sitini za ndovu, unaweza kuzichukua zote maana vitu hivi ni hatari”.Wanyama muhimu katika hifadhi za taifa wanazidi kupungua na kutoweka kabisa kutokana na biashara hii. Mwandishi ameliangazia ili mamlaka husika na jamii viweze kuweka mikakati na sheria madhubuti za kuangamiza suala hili kwani hupelekea nchi kuendelea kuwa maskini.
Rushwa na kutowajibika:Mambo ya hongo na rushwa na kutowajibika kwa viongozi ambao wamepewa mamlaka na wananchi ili wafanye kazi kwa maslahi ya taifa yamejadiliwa. Mfano mhusika Brown si mfanyakazi bora kwani hakutimiza wajibu wake bali alifanya kazi kwa upendeleo mkubwa bila kujali haki. Alipokea rushwa na kutoa pia. Mfano uk.100 anasema“……lakini Brown Kwacha alikuwa mtu wa nyendo akajua karata gani acheze na ipi aibakishe. Alisema kwa kiburi suala si kupata kiwanja ila mahali panapofaa kuporomoshwa kasri la kifahari”. Hivi ndivyo hali ilivyo, wenye uwezo wa kutoa rushwa ndio waliopatiwa huduma haraka. Pia anatuonesha jinsi Brown Kwacha alivyofanya kazi kwa upendeleo uk.97 mwandishi anasema “katibu wa Brown Kwacha alimtazama mkuu wake wa kazi akastaajabia namna alivyoweza kukaidi kuwahudumia wengine ila alivyolainika mbele ya wasichana kama jani la mboga au bufalo ndani ya maji.” Suala hili ni tishio kwa Wananchi kwani hupoteza wa haki, mwandishi anakemea suala hili vikali, na viongozi wanashauriwa kuenenda kwa mujibu wa maadili ya kazi zao.
Mapenzi: Mapenzi aliyoyajadili mwandishi katika riwaya hii ni ya sura mbili tofauti.Mapenzi ya dhati;Hili limeoneshwa na mhusika Amani kwa rafikiye Tino, kwani alibeba suala la Tino kuuguliwa na mwanae kama lake, alimsaidia katika shida na raha, hakumuacha peke yake mfano uk.145. mwandishi anasema Tino akawaza“akawaza dunia hii ya leo nani atajitoa kwa hali na mali kumsaidia kapuku kama yeye. Nitamlipa nini Amani?”hii inaonesha fadhila alizokuwa nazo Amani. Pia mapenzi ya dhati yameoneshwa kwa Tino kwa mwanae Cheche na familia yake. Tino aliipenda sana familia yake hata kuhangaika kwa hali na mali kumtibu mwanae Cheche kwa kila gharama kwani alidiriki kuiba fedha benki ili amudu kumpeleka mwanae nje kwa ajili ya matibabu. Mwandishi anatufundisha kuwa na mapenzi ya dhati kwani ni ishara ya mafanikio na amani. Kwa upande wa pili amejadili juu ya mapenzi yasiyo ya dhati au ya kweli. Mhusika Brown amechorwa kutokuwa na mapenzi ya dhati na kukosa uaminifu kwa mkewe na watoto kwani ni muhuni sana. Alikuwa na mahusiano ya mapenzi na wanawake wengi hakujali familia yake kabisa. Hakuonesha hata chembe ya upendo kwa familia yake. Mfano uk.109“mabinti zake walitamani sana kusafiri na baba yao. Lakini licha ya safari zake nyingi mno hawakupata fursa hiyo.”Pia uk.106 anasema watoto walikosa upendo“walitapia mno, lau kungekuwa na maelewano na upendo mkubwa baina ya baba na mama yao!fauka ya hayo baba yao alikuwa mkali”.Pia mapenzi yasiyo ya uaminifu kwa Brown na wapenzi wake kama vile Leila, Josephine. Mapenzi haya yalikuwa ya pesa tu! Uk 112 mwandishi amemzungumiza Leila “badala ya kumfikiria zaidi Brown Kwacha akatarajia zaidi faraja kuangalia nwanyama kwenye hifadhi ya Kwale”.Piauk.99Josephine anaomba fedha kwa Brown“.. cha kutosha kununua vitu vya harusi kama paundi alfu sita hivi”Mapenzi yasiyo ya dhati na ukosefu wa uaminifu katika ndoa ni janga katika jamii za sasa kwani wazazi hujisahau na kukiuka maadili ya ndoa jambo ambalo ni hatari mno kwani husababisha migogoro na ugomvi katika familia (mafarakano) na hata kuambukizana magonjwa hatari.
Nafasi ya mwanamke katika jamii
Amechorwa kama chombo cha starehe: Mfano ni Josephine na Leila, Brown Kwacha aliwatumia kujiburudisha kwa uasherati, pia wanawake walijiuza katika moja ya sehemu ambazo Amani alipenda kwenda.
Amechorwa kama kiumbe mwenye upendo: Mwema mke wa Tino ni mwanamke ambaye alikuwa na upendo wa dhati kwa mumewe na watoto kutokana na matunzo aliyowapa.
Amechorwa kama mlezi: Mfano mzuri ni Mwema na mke wa Brown ambaye yeye alikuwa ndiye mwangalizi mkuu wa familia kwani mumewe hakuwa na muda huo zaidi ya kuponda starehe na anasa kwa mda wa ziada aliopata badala ya kukaa na familia yake.
Amechorwa kama mtu mvumilivu: Mke wa Brown alivumilia sana mateso ya mmewe, hakuamua kumuacha bali alivumilia pamoja na kumdharau kote, kumdunisha na kutomthamini kama mke.
Amechorwa kama kiumbe duni: Brown hakumshirikisha mkewe katika maamuzi yoyote yale wala hakutaka ushauri wowote kutoka kwake alimdharau na kumpuuza tu.
Kama mtu jasiri na mwenye msimamo: Pamela anaoneshwa kuwa ni mwanamke jasiri kwani aliweza kumkataa Brown kimapenzi pamoja na vishawishi vya kila aina. Mfano uk.99 mwandishi anasema“lakini Pamela kama mwanariadha stadi, aliviruka viunzi vyote vya Kwacha…… mwanzo alimchukia lakini taratibu alianza kumheshimu”.
MIGOGORO
Mwandishi Safari pamoja na kujenga visa vyake vya kusisimua pia hakuacha kuibua migogoro ili kukamilisha masimulizi ya visa vyake.
Mgogoro baina ya pande mbili
Mgogoro baina ya Josephine na mke wa Brown: Sababu ya mgogoro huu ni Josephine kujihusisha na uhusiano wa kimapenzi na Brown Kwacha na kufumaniwa na mke wa Brown. Walipigana na kuumizana lakini Josephine hakuacha mahusiano hayo.
Mgogoro kati ya wafanyakazi wawili wasukuma makwama: Sababu ya mgogoro huu waligombaniana matenga ya kubeba na mwishowe kuishia kupigana.
Mgogoro baina ya Jinja Malon na vibaka: Jinja Malon aliwapiga vibaka baada ya kutaka kumkwapulia mwanamke mmoja hereni, mkufu na hata kutaka kumbaka kichochoroni. Uk 51-52.
Mgogoro kati ya Katibu Mkuu wa Wizara ya mila na utamaduni na kijana mmoja: Walipigana kugombania mwanamke ambaye alikuwa na mahusiano na wanawaume wote wawili. Uk.102.
Mgogoro wa nafsi wa Tino
Tino alisumbuliwa na mgogoro wa nafsi kutokana na hali ya ugonjwa wa mwanae Cheche. Hakujua apate wapi pesa za kumtibia kwani hakuwa na pesa na alitakiwa kupelekwa nje kwa ajili ya matibabu. Lakini baada ya kushauriwa na Amani akaibe pesa alifanya hivyo na kufanikiwa na ndipo alipata amani baada ya kumudu gharama za matibabu ya mwanae.
FALSAFA: Mwandishi anaamini kuwa chanzo cha matatizokatika jamii ni upotofu wa maadili, kutowajibika, mifumo mibovu ya uchumi, rushwa, ufisadi na biashara haramu na mengine mengi. Anaamini kuwa endapo jamii itabadilika basi hayo matatizo hayatakuwepo. Anatoa suluhu ya matatizo hayo kama vile kupinga utabaka, rushwa, matumizi mabaya ya mamlaka na kuwa na usimamizi mzuri wa mali za umma.
MTAZAMO: Mtazamo wa mwandishi ni wa kiyakinifu. Ameonesha matatizo ndani ya jamii na kuonesha suluhu ya matatizo hayo. Anaonesha matatizo ya uhujumu uchumi, ufisadi, kutowajibika kwa viongozi, ukosefu wa huduma za jamii, matabaka na hali ngumu ya maisha. Anaona kuwa sababu ya matatizo haya si ya kidhanifu tu au ni mipango ya Mungu tu! Ila anonesha sababu za matatizo hayo kama vile kukithiri kwa rushwa, mifumo mibaya ya kiuchumi na anatoa suluhu kwa kuwapiga vita viongozi wasowajibika. Mifumo mibovu ya uchumi inayoendelea kutengeneza utabaka katika jamii.
MSIMAMO: Mwandishi A. Safari ana msimamo wa kimapinduzi, hili linajidhihirisha wazi kutokana na mambo anayoyaeleza ambayo yanalenga kuibadili jamii. Analeta mapinduzi kwa viongozi wasiowajibika, mifumo mibovu ya uchumi inayoendelea kusababisha umaskini na kuwakweza wachache.Anatoa suluhu ya matatizo mbalimbali. Anakemea malezi mabaya kama ya Brown pia anasa na starehe na mengine mengi.
UJUMBE
Viongozi na watumishi wa umma wanapaswa kuwajibika kulingana na majukumu yao.
Rushwa, ufisadi na biashara za magendo ni vikwazo vya maendeleo hivyo si budi kupigwa vita.
Serikali na mamlaka husika vinapaswa kusimamia vyema sheria na taratibu ili kuwawajibisha wanaoenda kinyume kama vile wahujumu uchumi.
Uaminifu katika ndoa na mapenzi ya dhati ni jambo la msingi kwani huongeza Amani katika familia.
Jamii inapaswa kutambua nafasi ya mwanamake na kumshirikisha na sio kumdunisha bali apewe nafasi ya kuamua na kushiriki katika shughuli mbalimbali za kimaedeleo.


M

Comments

Popular posts from this blog

KISWAHILI FORM 1: FASIHI SIMULIZI

KISWAHILI Form 1 Topic 4 FASIHI SIMULIZI Fasihi simulizi ni moja kati ya tanzu za fasihi inayohifadhiwa na kurithishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine kwa njia ya mdomo. Katika mada hii utajifunza na kisha utaweza kubainisha tanzu na vipera vya fasihi simulizi pamoja na ufafanuzi wake. Na pia utaweza kutofautisha kati ya kipera na kipera au kati ya utanzu na utanzu. Ubainishaji wa Tanzu za Fasihi Simulizi Tanzu za Fasihi Simulizi Bainisha tanzu za fasihi simulizi Fasihi Simulizi ni kazi ya fasihi inayohifadhiwa na kurithishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine kwa njia ya mdomo kama vile; hadithi, ngoma na vitendawili. Tanzu za Fasihi Simulizi ni pamoja na hizi zifuatazo: Masimulizi/hadithi Semi Ushairi Mazungumzo Maigizo Ngomezi Ufafanuzi wa Vipera vya Tanzu za Fasihi Simulizi Vipera vya Hadithi Fafanua vipera vya hadithi SIMULIZI/ HADITHI Masimulizi ni fasihi yenye kusimulia habari fulan...

MBINU ZA KUFUNDISHIA

Mbinu za kufundishia , ni miongozo mbalimbali atumiayo mwalimu wakati wa kufundisha somo aliloliandaa kwa wanafunzi wake. Walimu wanapaswa kuamua kwa kuchagua kwa makini njia na mbinu bora za kufundishia ili wanafunzi wake waweze kujifunza kwa ufanisi. Ziko njia nyingi za kutengeneza mazingira ya mtoto aweze kujifunza na pia ziko mbinu nyingi za kufundishia. Pamoja na wingi huo tunaweza kuzigawa katika makundi makuu mawili kadri ya jinsi zinavyowashirikisha watoto katika tendo la kujifunza, ambazo tunaweza kuziita shirikishi na zisizo shirikishi . Zifuatazo ni baadhi ya mbinu shirikishi na zisizo shirikishi za kufundishia pamoja na faida na hasara zake:- Njia ya majadiliano , njia hii imekuwa ikitumika katika ufundishaji kwa muda mrefu. Katika kujadiliana mwanafunzi mmoja mmoja hupata nafasi ya mawazo aliyonayo kuhusu suala linalojadiliwa na yeye pia huweza kupata mawazo yaw engine. Katika majadiliano mwanafunzi hupata ujuzi mpya nje na ule aliokuwa nao kabla hajashiriki kat...

DHANA YA USHAIRI ILIVYOFAFANULIWA NA WATAALAMU MBALIMBALI

Ushairi kama moja kati ya tanzu za fasihi inayowasilishwa katika namna zote aidha kwa lugha ya maandishi au kwa lugha ya masimulizi una mchango au nafasi kubwa sana katika kunufaisha au kustawisha maisha ya binadamu kwa kumuelimisha, kumsisimua, kutunza na kuhifadhi amali zake pamoja na kukuza na kuendeleza lugha yake kama moja kati ya vipengere muhimu maishani mwake. Ushairi kama nudhumu katika fasihi simulizi hujumuisha nyimbo, ngonjera, tenzi na mashairi yenyewe. Ushairi wa Kiswahili waweza kuainishwa katika tanzu au katika kumbo mbalimbli kama asemavyo Mulokozi (1996) kuwa zipo kumbo kuu tatu ambazo ni ushairi wa kijadi au kimapokeo, ushairi wa mlegezo au huru na ushairi wa maigizo. Wanazuoni wafuatao wa mashairi ya kimapokeo wametoa maana za ushairi kama ifuatavyo:- Shaaban Robert (1958:37). “Ushairi ni sanaa inayopambanuliwa kama nyimbo, mashairi na tenzi. Zaidi ya kuwa na sanaa ya vina, ushairi una ufasaha wa maneno machache au muhtasari…, mawazo, maoni na fikra za ndani zi...