3. K.K. Kahigi na M.M. Mulokozi: Malenga wa Bara SURA YA TATU Kitangulizi Majina ya K.K. Kahigi na M.M. Mulokozi si mageni katika uwanja wa iasihi ya Kiswahili. Kati ya kazi zao mbalimbali zilizokwishachapishwa za Mashairi ya Kisasa. (TPH, 1973) Malenga wa Bara (EALB, 1976) na Kunga za Ushairi na Diwani Yetu (TPH. 1982) ndizo ambazo zimewapa nafasi muhimu katika dunia ya ushairi wa Kiswahili. Pamoja na hizo, MuIokozi pia amechapisha tamthilia ya kihistoria inayotumia mawanda ya kiepiki kueleleza maisha ya shujaa Mkwawa, Mukwawa wa Uhehe (EAPH, 1979) naye Kahigi akishirikiana na R.A. Ngemera wamechapisha tamthilia ya Mwanzo wa Tufani ( TPH, 1977) yenye kuchambua masuala mabalimbali ya kitabaka katika jamii. Katika kazi zote hizi waandishi hawa wanashughulikia dhamira kadhaa zinazohusu nyanja za utamaduni, saisa na uchumi katika maisha ya Watanzania na Waafrika kwa jumla. DHAMIRA KUU Katika diwani yao ya...