Yang'aa kila dakika, na kuburudisha moyo, Wachache waaliofika, umewatoka uchoyo, Yeyote atamwalika, akaliwazike moyo, Hii taa ya labuka, kaiweka hapa kwetu, Ni kama kaisimka, na miale yake butu, Haitakuja zimika, wala kuja shika kutu. Kama mtu anacheka, meno yake ya kung’aa, Siku jua likiwaka, waweza ukazubaa, Wengi wameweweseka, kuiona hii taa. Ulaya na Amerika, sifa zake zasikika, Wametamani kufika, nao wakasuuzika, Wachache waliofika,wamependa Afrika, Nami nilihamanika, awali nilipoona, Homa iliyonishika, walai sikuiona Kweli niliweweseka, ile taa kuiona. Ndoto zilikamilika, kwa watu nilijivuna, Kuishika nilitaka, japo ipo juu sana, Nguvu ziliongezeka, kila nilipoiona. Picha ndani nimeweka, wanangu waje ziona, Yeyote akizitaka, nitampa kuziona, Na yeye nitamtaka, aende haraka sana. Twende bila ya kuchoka, ili iwe kumbukumbu, Hata wao wakifika, wasitwone mambumbumbu, Waijue Afrika, si bara la mbumbumbu, Hii t
MUNGU AKUPE HEKIMA Miaka mingi imepita,tangu uziache nepi, Hekima umezichota,na kuyaacha makapi, Na mengi umeyapita,sijui myaka mingapi, Mungu akupe hekima,kaka yangu Tumsifu. Kama vile jina lako,Mungu wetu twamsifu, Mema yote yaje kwako,na ujazwe utukufu, Pongezi za ndugu zako,kamwe zisije kukifu, Mungu akupe hekima,kaka yangu Tumsifu. Mama amepata mwana,mwana mwema naamini, Hasemi mtundu sana,bali unajiamini, Wewe kaka ndiwe shina,nduguzo twakuamini, Mungu akupe hekima,kaka yangu Tumsifu. Baba anajivunia,kuwa nawe kila siku, Kwa watu kujisifia,atamani uwe huku, Kakangu unatulia,huna papara za kuku, Mungu akupe hekima,kaka yangu Tumsifu. Mwisho njoo kalamuni,wataka vitu jamani, Wakutaka hadithini,ubuni picha jamani, Wasema uje ubuni,ukuze yako thamani, Mungu akupe hekima,kaka yangu Tumsifu